Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

igihumbi

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
441
350
Habari za kutwa wanajamvi poleni na majukumu.

Leo naomba msaada kwa wale waliowahi au wanaendelea kutengeneza faida ya Tsh 30,000 na kuendelea kila siku.

Tafadhali zingatia kueleza yafuatayo:

1. Aina ya biashara
2. Mtaji unaotumia kuzalisha faida ya 30,000

Kumbuka waliofanikiwa sio wachoyo, wanapenda na wengine wafanikiwe.

============================

Linapokuja swala la biashara mtandaoni ni wazi kuwa kila mtu ana upeo wake pamoja na uzoefu unaomsaidia kupata pesa mtandaoni, lakini pia kufanya biashara mtandaoni hasa ukiwa Tanzania unahitaji kuangalia aina fulani za biashara ambazo hizo pengine zinaweza kukusaidia zaidi kupata pesa mtandaoni hasa ukiwa afrika na Tanzania kwa ujumla.

Kupitia makala hii nitaenda kukujuza aina tano za biashara ambazo zinalipa zaidi mtandaoni hasa kwa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, kutu cha msingi ni kuwa na uvumilivu kusoma makala hii hadi mwisho na uhakika utapa mambo kadhaa ya kujifunza.

Kumbuka aina hizi za biashara zimechaguliwa kutokana na udogo wake wa mtaji, huku tukiwa na fikra kuwa wote tunataka kuanzia chini. Hivyo basi unaweza kuanza biashara hizi wakati wowote kitu cha msingi ni uvumilivu na adabu ya kufanya mambo hayo kwa umakini.

5. Anzisha Tovuti au Blog
Ukweli ni kwamba, Google bado inauhitaji wa tovuti hasa tovuti za kiswahili. Lakini hapa sina maana kuwa na tovuti ni tovuti hapana, bali hapa nina maana tovuti zenye kuleta maana na kutoa mchango wa thamani kwa wasomaji kila siku na sio kuangazia maswala ya kipato pekee. Lakini wazo hili la biashara mtandaoni limekuwa ni la mwisho kwa sababu kuwa na tovuti pekee sio chanzo cha mapato bali unahitaji kuwa na vyanzo vya ziada kuweza kuhakiksha tovuti hiyo inakuingizia faida.

4. Anzisha YouTube Channel
Sambamba na kuanzisha tovuti unaweza pia uka anzisha YouTube channel lakini ni muhimu kuwa na picha pana ya unapokwenda kwani watu wengi wamekuwa wakianzisha channel bila kuwa na muelekeo wakiwaza kwamba unaweza kuwa tajiri kwa haraka kwa kuchapisha habari au video zisizokuwa na maana. Ukweli ni kwamba kuwa na channel hasa hapa Tanzania unahitaji kutengeneza ubora wa video zako pamoja na mada zako ziwe na mchango lakini pia unatakiwa kujua unapokwenda kwani asikudanganye mtu yoyote matangazo ya Google Pekee hayatoshi.

3. Kutafuta Masoko Kwa Niaba ya Makampuni (Affiliate Marketing)
Ukweli ni kwamba hakuna kampuni ambayo haina kitengo cha kutafuta masoko, kama kwa namna yoyote umefanikiwa kutengeneza jina mtandaoni au unaweza kutoa ushawishi mtandaoni basi unaweza kufanya biashara ya affilate marketing. Lakini kama zilivyo biashara nyingine kwenye listi hii pia nayo hii inakuja na changamoto zake. Kama unafanya kazi hii kwa hapa Tanzania ni lazima kuwa na jina kubwa sana ndipo uweze kufanikiwa kwani watu wanahitaji mtu muaminifu na uaminifu hauji kwa maneno bali kazi na muda mrefu wa kujituma bila kuwaza faida.

Vilevile kama unafanya kazi hii na kampuni za nje ya Tanzania bado kuna changamoto kubwa sana ya njia za malipo hasa kwa wanunuaji pamoja na njia za kuweza kupokea fedha zako baada ya kutengeneza faida.

2. Ushawishi Kwenye Mitandao ya Kijamii (Social media influencer)
Kwa sasa kama umekuwa ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram lazima unajua kuwa kuna baadhi ya watu wanafanya matangazo ya makampuni fulani kupitia akaunti zao hii ndio inaitwa social media influencer, hapa sisemi matangazo ya vipodozi au matangazo madogo madogo bali mara nyingi watu hawa hupewa bidhaa na makampuni makubwa kuweza kujaribu au kutumia na baadae kutangaza kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii. Lakini biashara hii kama zilivyo biashara nyingine nayo pia inakuja na changamoto.
Ili kuweza kufanya biashara hii unahitaji kuwa na wafuasi wengi na pia unahitaji kuhakikisha wewe mwenyewe unajiweka kwenye mazingira bora ya kushawishi kampuni kuweza kufanya kazi na wewe, akaunti yako isiwe yenye kuvunja sheria za nchi au kukiuka maadili kwa namna moja amba nyingine lakini kikubwa kabisa unatakiwa kuwa na ushawishi mkubwa kupitia mitandao yako hiyo.

1. Kuwanunulia Wateja Bidhaa Kutoka Mtandaoni (Drop shipping)
Kama wewe ni mpenzi wa biashara mtandaon basi lazima utakuwa kwa namna moja ama nyingine umeshawahi kuwaza kununua kitu kutoka mtandaoni, lakini kutokana na sababu kama njia rahisi za malipo pamoja na njia za kufanya mzigo kukufikia kwa urahisi basi unakuta hatua hii ya kununua kitu inakuwa ni ngumu sana.

Ndio maana biashara ya kununulia watu vitu kutoka mtandaoni ni moja ya biashara bora sana kwa sasa hapa Tanzania. Biashara hii inahusisha kununua bidhaa kwenye tovuti kubwa kama vile Amazon, Ebay na nyingine kama hizo na kusafirisha bidhaa hizo moja kwa moja kwa mteja bila mteja kuwa na mawasiliano na kampuni husika, mteja hukulipa wewe kiasi fulani cha pesa ambacho hichi hutosha kulipia gharama zote pamoja na wewe kupata faida kwa kiasi fulani.

Mara tu mzigo unapofika mteja huja kuchukua kwenye ofisi zako au huletewa na kampuni za usafirishaji ambazo unakuwa unafanya nazo kazi, uzuri wa biashara hii unaweza kufanya bila hata ya kuwa na ofisi lakini unahitaji kuwa na uaminifu mkubwa ambao huu unapatikana kwa kuwa na jina kubwa pamoja na kufanya biashara hiyo kwa muda mrefu kidogo.

Na hizo ndio baadhi ya biashara ambazo ukweli unaweza kufanya na kuona faida hasa ukiwa hapa Tanzania. Kitu cha msingi unatakiwa kujua kuwa kila biashara inakuja na changamoto zake na pia kila biashara inahitaji uvumilivu pamoja na adabu ya kuendelea kufanya kila siku bila kutegemea faida kubwa hasa pale unapokuwa una anza. Kama unataka kujua zaidi soma hapa kujua mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya kuanza biashara yoyote mtandaoni.

=================

Mwaka huu 2019 ni mwaka ambao moja ya malengo ambayo kila mtu anapaswa kuwa nayo ni malengo ya kibiashara. Kama bado hujawa na biashara basi unapaswa kuanza biashara yako mwaka huu. Na kama tayari una biashara, basi unapaswa kuikuza zaidi biashara yako mwaka huu 2019.

Hivyo unapofikiria biashara gani uanzishe, au unapokuwa na mawazo ya biashara lakini hujui uchagueje, angalia wapi uhitaji wa watu upo, na wewe toa uhitaji huo.

Nyakati zinapokuwa ngumu, usikazane kuwa na biashara ya kipekee, ambayo unahitaji kuanza kumshawishi mteja kwa nini anapaswa kununua unachouza. Ukishaona biashara unayofanya au unayotaka kufanya inakubidi uanze kumshawishi mteja kwa nini anapaswa kununua, hapo upo njia mbaya. Mteja anapaswa kujua tayari kwa nini anapaswa kununua, na avutiwe kununua kwako kwa huduma nzuri unazotoa.
1. Bidhaa za chakula.

Kwa kuwa watu bado wanakula, na wataendelea kula siku zijazo, kuanza biashara ya kuuza bidhaa za chakula ni hatua sahihi kwako kuchukua. Hapa unaweza kuuza na kusambaza bidhaa za chakula kama nafaka, mafuta na bidhaa nyingine muhimu.

Angalia uhitaji wa bidhaa za vyakula kwa wale wanaokuzunguka au unaoweza kuwafikia kisha wapatie bidhaa hizo kwa kiwango na gharama ambazo wanaweza kumudu huku wewe ukipata faidia ili biashara iweze kuendelea.

Uzuri wa biashara ya bidhaa za chakula unaweza kuanza na mtaji kidogo, ukatafuta bidhaa zilizo bora na kuweza kuwasambazia watu kule walipo.

Biashara ya mchele, mahindi, maharagwe na nafaka nyingine zina uhitaji mkubwa kwa watu.

2. Huduma za chakula.

Biashara nyingine unayoweza kuanza kwa mafanikio mwaka huu 2018 ni biashara ya utoaji wa huduma za chakula. Hapa unatengeneza na kuuza chakula bora ambacho watu wanaweza kukimudu.

Uzuri wa biashara hii ni kwamba, watu wengi wanabanwa na kazi au biashara zao na hivyo hawawezi kuandaa vyakula vyao, hasa vya mchana. Hivyo kwa kuwajua watu wa aina hii na namna unavyoweza kuwafikia, unaweza kuwapatia chakula ambacho ni bora kwa gharama wanazoweza kulipia.

Kingine muhimu ni kwamba watu kwa sasa wanajali sana afya zao, hivyo wanakula mlo bora, unaweza kutumia nafasi hii kutoa vyakula bora kiafya badala ya vyakula vya haraka ambavyo siyo bora.

Unaweza pia kutoa huduma ya matunda, juisi na huduma nyingine za chakula kwa wale wenye uhitaji.

3. Bidhaa za mavazi.

Kama ambavyo tumeona, watu wanaendelea kuvaa nguo, bila ya kujali mambo ni magumu au la. Hivyo unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa bidhaa za mavazi. Hapa unauza mavazi kama nguo, viatu na mengineyo.

Unachohitaji hapa ni kujua uhitaji wa watu kwa wakati mbalimbali. Kwa mfano kipindi cha mwanzo wa mwaka bidhaa nyingi za mavazi zinazotoka ni zile zinazohusiana na mavazi ya shule. Pia katika kipindi cha sikukuu, watu wanajibana wawezavyo ili wavae nguo mpya.

Unapochagua kuingia kwenye biashara hii ya bidhaa za mavazi, angalia aina ya watu ambao ni wanunuaji wazuri. Mfano mavazi ya wanawake na watoto yanatoka zaidi kibiashara kuliko mavazi ya aina nyingine.

Uzuri wa biashara ya bidhaa za mavazi ni kwamba, unaweza kuianza kwa hatua ndogo sana, huhitaji hata kuwa na eneo la biashara. Unaweza kuchagua wateja unaowalenga, ukachagua bidhaa zao kisha kuwasambazia au kuwatangazia kwa njia ya mtandao.

4. Biashara ya huduma za mavazi.

Huduma za mavazi ni aina nyingine ya biashara unayoweza kuanza, ambayo itakuwezesha kupiga hatua kubwa. Kama una ubunifu wa mavazi, au unaona uhitaji wa mavazi ya aina fulani, unaweza kutoa huduma ya kuandaa mavazi hayo.

Hapa tunazungumzia kutoa huduma ya kuwaandalia watu mavazi kwa namna wanavyoyataka. Pia kuwasaidia watu kurekebisha mavazi yao. Biashara hii unaweza kuifanya kama unao ufundi wa kutengeneza mavazi. Lakini hata kama huna, unaweza kupata mtu mwenye ufundi ukawa unampa maelekezo na wewe kuwa na kazi ya kutafuta masoko au kusambaza yale mavazi yanayotengenezwa.

Siku hizi zipo mashine ambazo ni rahisi kutumia kushona mavazi ya aina mbalimbali ambazo unaweza kuwa nazo na kuanza kiwanda chako kidogo cha mavazi.

5. Ufugaji wa kibiashara – kuku.

Hakuna familia ya asili ya kiafrika ambayo haijawahi kufuga kuku. Na kuku ni moja ya biashara ambayo soko lake halijawahi kuyumba. Zimekuja biashara za ndege wa aina mbalimbali kama kware lakini zimepita na kuacha biashara ya kuku ikiwa imara. Huhitaji kumshawishi mtu kwamba anahitaji kula nyama ya kuku, au kula mayai, ni kitu ambacho kwa wengine ni ufahari.

Unaweza kuingia kwenye ufugaji wa kibiashara na kufuga kuku ambao utaweza kuuza mayai, kuuza vifaranga na hata kuuza kuku wenyewe. Unaweza kufuga kuku wa kienyeji, kuku chotara na hata kuku wa kisasa kabisa. Unachohitaji kuangalia ni uwezo wako na uhitaji wa soko unalolenga.

Uzuri wa ufugaji wa kuku ni kitu unaweza kuanza kwa hatua ndogo na kukuza. Pia unaweza kufanya huku ukiendelea kufanya vitu vingine. Pia itakuhitaji uwe makini ili ufugaji wako ukue.

6. Ufugaji kibiashara – samaki.

Samaki ni chakula kingine ambacho kina uhitaji mkubwa sana kwenye jamii zetu. Ni mboga ambayo ina uhitaji mkubwa na hivyo ukiweza kuzalisha kwa kiwango kizuri, ni biashara nzuri kwako kufanya.

Ufugaji wa samaki kwa sasa umerahisishwa kutokana na upatikanaji wa huduma muhimu za samaki. Huduma kama vyakula vya samaki, ujenzi bora wa mabwawa ya kufugia samaki zimefanya ufugaji wa kibiashara wa samaki kuwezekana.

Japo ufugaji wa samaki unahitaji mtaji mkubwa, inawezekana pia kuanza kidogo na ukafanya vizuri.

7. Kilimo biashara – mbogamboga na matunda ya muda mfupi.

Hata kama uchumi ni mgumu kiasi gani, watu hawatakula chakula bila ya kitunguu, bila ya nyanya, bila ya bamia. Watu wataendelea kula mchicha, matembele na mboga nyingine. Na muhimu zaidi matunda kama matango, matikiti maji na hata ndizi ni vyakula ambavyo kila mtu ana uhitaji navyo.

Hivyo eneo unaloweza kuingia kibiashara mwaka 2018 kulingana na nafasi na uwezo wako ni kilimo biashara cha mbogamboga na matunda ya muda mfupi. Ninaposema kilimo biashara namaanisha ulime kwa lengo la kuuza, hivyo kulima kwa viwango vizuri na ubora ambao unakubalika na soko unalolenga.

Unaweza kulenga wanunuaji wa rejareja au kuuza kwa wanaonunua jumla, kama mahoteli au maduka makubwa.

8. Kilimo biashara – mazao ya chakula.

Mazao ya chakula kama nafaka, mahindi, maharagwe na mpunga ndiyo mazao yanayoongoza kwa kuliwa sana kwenye jamii zetu. Hivyo hili ni eneo ambalo unaweza kuingia kibiashara na ukafanya vizuri kwa mwaka huu 2018. Unaweza kuingia kwenye kilimo moja kwa moja na ukalima kibiashara, kwa njia ambayo utazalisha kwa kiwango kikubwa na kwa ubora wa kuweza kuuza.

Lakini pia kama huwezi kulima, kwa kukosa nafasi au usimamizi mzuri, unaweza kununua mazao hayo kwa wingi kwenye msimu wa mavuno, kuyaongeza thamani na kuyauza kwa wahitaji. Mfano kununua mpunga wakati wa mavuno, kuukoboa, kuuhifadhi kwenye vifungashio vizuri na kuuza kwa watumiaji ni biashara ambayo inaweza kukupeleka kwenye mafanikio makubwa 2018.

9. Biashara ya vyakula vya mifugo na huduma zake.

Watu sasa wanafuga, kuanzia kuku, mbuzi, ng’ombe, sungura, samaki na kadhalika. Unaweza kuingia kwenye biashara kwa kutoa huduma mbalimbali za kuwezesha wafugaji kupata mafanikio kwenye ufugaji wao.

Hapa unaweza kuingia kwenye biashara ya kuuza vyakula vya mifugo, kuuza madawa na virutubisho vya mifugo na hata kutoa huduma za vyakula mbadala kwa wafugaji.
Na kama wewe ni mfugaji au una utaalamu kuhusu mifugo, unaweza kutoa ushauri kwa wafugaji kibiashara pia.

10. Huduma za ushauri wa kitaalamu.
Kwa jambo lolote ambalo umesomea, au umeshakuwa na uzoefu nalo, kuna watu ambao wamekwama na hawajui wafanye nini. Hapa unaweza kuingia kwenye biashara ya kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa lile eneo ambalo una utaalamu au uzoefu nalo.

Kama umesomea mambo ya afya unaweza kutoa ushauri wa kiafya kwa watu na wakakulipa. Kama umesomea au una uzoefu kwenye biashara, unaweza kuwashauri watu kuhusu biashara na wakakulipa.

Angalia kipi unajua na watu hawajui, kisha wape ushauri kwa njia ambayo watakulipa.
 
Kama unataka mtaji wa 30k-50k means kwa mwezi unakusanya 900k-1.5M
Basi jua iyo biashara ni kubwa inahitaji capital ya kuanzia 5M-10M na kuendelea

Kumbuka pikipiki kama boda boda na bajaji zinauzwa bei mkasi sana mfano boda boda 2.5M na wanarejesha kila siku 8000-10,000
Hivyo hivyo Bajaji inauzwa 7M wanarejesha kila siku 15,000-18,000

Uber yaani gari kama IST au tufanye vitz inacost approximatel 9M-13M
Wanarejesha 25k-30k

Hivyo unaweza ukachanganua ulicho nacho mfukoni kwako utaelewa iyo faida ya kila siku 30-50 unahitaji kuweka pesa kiasi gani

Na log out
 
Biashara ya kukuingizia hiyo faida na inaweza kuzidi

Ila sio chini ya 30k

Ni BODA BODA ila tu hiyo piki piki iwe yako na Uendeshe wewe mwenyewe.

Biashara nyingine ni

Biashara yangu ya kuingiza nyimbo kwenye memory card na kuwafungulia

whatsapp kina mama na kina baba wasio jua tumia simu zao.

Nakuja tena subiri nifikirie zingine.
 
Salooon local ya kunyoa watu,usiweke zile mbwembwe

Sijui akimaliza kunyoa aoshwe then apakwe mafuta,hakikisha kazi yako ni kunyoa tu

Mtu akishamaliza kunyoa Asepe zake akaoge kwao huko

Nyoa mtu mzima 1500, mtoto 1000

Wakija watu wazima wakikuomba uwanyoe kwa 1000 usikatae Wanyoe

Jioni unaondoka na zaidi ya 40k

ILA TU

Saloon iwe yako na wewe kinyozi ndio uwe boss
 
Kibanda simple cha kuuza vinywaji naongelea vinywaji kama

Mo energy, azam colla, Twist, mango juice, nk

Maji ya uhai, masafi, vocha (kukwangua na kurusha), kuchajisha simu, sigara, vipombe pombe

Hasa konyagi ya kupima, nk

Hakikisha muuzaji BOSS ni wewe mwenyewe na usiajiri mtu.
 
Ngoja niwape udaku huu,nakumbuka miaka ya 2007 sikuwa na mtaji wa keshi isipo kua nilikua na ufundi wa simu,ambao nilifundishwa na jamaangu mmoja anaitwa masasi alikua fundi mzuri sana asie na uchoyo....

Wakati nikijifunza kazi hiyo ofcn kwake alikua akiingiza sio chini ya laki 1 mbaka zaidi hii ilini fanya nijitume kujua kazi hiyo vema.nilipo jua ndipo nikakopa vitendea kazi nikaanza kazi mdogo mdogo kwa kwwli elf 20 paday mbaka 40 sikukosa hapo ndipo nilipo tokea.
 
Sema mara nyingi ukiwa na ka elimu fulani hivi unakuwa unachagua kazi na hii ni kwasababu jamii inayotuzunguka ndio inatuaharibu kwa mtazamo wao.

Kwani unakuta ukifanya kazi fulani wanakusimanga kwamba unafanya kazi ambayo hata mtu wa darasa la saba angefanya na wanakuuliza sasa shule ulienda kufanya nini.

Mimi niliwahi kufanya kazi ya kuendesha bajaj ya kwangu na naingiza kuanzia 20k+ lakini sikufichi kipindi naanza ile kazi ndugu,marafiki na jamaa walinichukulia simple sana na hii ni kwasababu ya elimu niliyokuwa nayo. lakini nilikomaa na kweli ilinitoa mpaka nikaamua kubadili upepo.

Ushauri wangu kwa vijana kama una mtaji wa ml 2 hadi tatu angalia fursa zilizopo mazingira yako piga kazi bila kuangalia elimu yako. Utashangaa maisha yanavyokuwa mepesi japo mwanzo ni mgumu.
 
Back
Top Bottom