Wabunge Uganda wamekataa pendekezo la serikali la kuruhusu wasichana wenye umri wa miaka 15 kupata tembe za kupanga uzazi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Wabunge nchini Uganda wamekataa pendekezo la serikali la kuruhusu wasichana wenye umri wa miaka 15 kupata tembe za kupanga uzazi ili kupunguza viwango vya juu vya mimba.

Naibu Spika Thomas Tayebwa aliliita wazo hilo "Ushetani", akisema "Litarasimisha unajisi" wa wasichana.

Afisa mkuu wa wizara ya afya alisema "Unyanyapaa" unaowazunguka vijana wanaotumia uzazi wa mpango unapaswa kukomeshwa.

Takriban robo ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 nchini Uganda wana mimba au tayari ni akina mama, utafiti unasema.

Kiwango kiliongezeka sana wakati wa Covid wakati shule zilifungwa kwa karibu miaka miwili.

Wakati wa mjadala mkali wa bunge siku ya Jumanne, Mbunge Lucy Akello alihoji iwapo umri wa kuwa na idhini unapunguzwa kutoka miaka 18 ya sasa hadi miaka 15, gazeti la serikali la New Vision liliripoti.

Alielezea pendekezo la kutoa uzazi wa mpango kwa wasichana wenye umri wa miaka 15 kama la "Kutisha".

Bi Akello alisema hakutumia njia za uzazi wa mpango. "Ninatumia njia ya asili, ambayo Mungu alinipa."

BBC
 
Ukiruhusu kupunguza uzao katika taifa jua baadae mtaangukia katika umasikini usiomithirika hasa kwa mataifa yanayoendelea na ndiyo maana ulimwengu huko majuu wanapambana sana na África ipunguze uzao ili izidi kutawalika, Ukimruhusu binti awe na uhakika wa kutoharibu maisha yake endapo atajihusisha na ngono zembe utakuwa umetengeneza taifa la ajabu sana,hivyo nawapongeza Wabunge wa Uganda kwa hilo
 
Siku za nyuma hapa nchini kulikua na kampeni ya kuwapeleka wasichana waliovunja ungo hospital wapewe elimu ya uzazi wa mpango!,sijui iliishia wapi ile kampeni ya kishenzi!!!
 
Back
Top Bottom