Imeshadhihirika kuwa migomo hiyo siyo utatui wamatatizo ya wanafunzi, je ni kwanini wanafunzi hawa hawalioni hili. Kama wasomi kwanini hawabuni solution ya kudumu .Na kama wao wanafunzi hawawezi kufanya hivyo ni kwanini wakufunzi wao wasiwasaidie kubuni solution ya kudumu. Nitawaambia kitu kimoja tu wanafunzi wa UDSM na vyuo vingine Tanzania: msidhani wanafunzi wa vyuo vya Ulaya na vingine Tanzania kama Tumaini ambao hawagomigomi wanaridhika na kila linalofanyika nchini, lakini wanatambua kuwa kugoma kusoma ni kudhirisha kutoheshimu thamani ya elimu.Kingiine ninachoshindwa kuelewa ni kwamba nyinyi mnagoma kusoma huku mkidai kusomeshwa, sasa nyinyi kweli madai yenu ni kusomeshwa au jambo jingine. Ushauri kwa uongozi wa chuo ni huu: hicho chuo msikiendeshe kisiasa. Jiulizeni swali moja,je ni nini kitawatokea wanafunzi wa Tanzania wanaosoma oxford Uingereza iwapo leo hii watagoma kuingia darasani kwa sababu hawajapewa mikopo na serikali yao toka Tanzania? Hicho kiendesheni kama taasisi inayojitegemea na ipeni taaluma heshima yake inayostahili, yeyote anayeidhalilisha taaluma ni adui wa mankind na mshughulikieni ipasavyo bila kukumbatia siasa.