Wabunge Nyota!

Wabunge Nyota!

natamani enzi za hamad rashid.mbowe kung'aa kazidiwa na mrema?!!

Hao ndugu zako wasahau waambie wasubiri next time may be 2015 or 2020 vyama vyao vitakapokuwa kambi rasmi ya upinzani.
2015/2020 watafika Quinine?
Hii ndoa ni ya 2010-2015, baada ya hapo kambi rasmi ya upinzani itakuwa inaongozwa CCM sijui watmuweka zuzu gani.
 
Dah wakuu wote mnaosema nime sahau kumtaja Lissu mnasahau haya ni maoni yangu tu. Ila siyo mbaya kwa vile na nyie wenzangu mmemtaja basi ina maanisha mchango wake una thaminiwa. Au lazima wote tuone mambo sawa?
 
Sugu namshauri ile bendi yake ya matusi aliyoizindua pale kwenye ukumbi wa musizi wa mheshimiwa Mbowe baada ya kupewa ridhaa na wanambeya auendeleze kama anadhani utalijenga taifa ambalo lina dimbwi la mafisadi. sisi kule kwetu tunasema "Umufa wi mbwebwe unyobwa wugishushe" hii sentensi Zitto huifanyia kazi mara nyingi ndio maana hatoisha kung'aa bungeni.

Sugu kauza mitumba, kasukuma mkokoteni na katoa mchango mkubwa katika ukuwaji wa fani ya sanaa-Bongo flava. Hakuingia bungeni kwa umaarufu wa jina la ukoo ila kwa nguvu zake mwenyewe na kukubalika kwake kwa wanambeya. Nadhani mpaka hapo alipofikia ni role-model tosha kwa vijana wengi hasa kipindi hiki shule zetu za kata zina-produce mass-failures, kwamba wasikate tamaa. Sasa, kama kuna mtu/kikundi/taasisi inayoweza kumsaidia huyu kijana wetu Sugu ili asonge mbele zaidi nadhani lingekuwa jambo la heri. Lakini kauli za kejeli na madharau dhidi ya kijana huyu (Sugu) si tu zinalenga kumdhoofisha na kumkatisha tamaa yeye Sugu bali zinatoa ujumbe kwa vijana wengi ambao (si kwa makosa yao) hawana 'hadhi fulani' kwamba wao ni bure (nothing) & hawana mchango wowote kwa Taifa! Hivi ni lini nchi hii imekuwa na matabaka kiasi hiki?
 
Mkuu MwanaFA1;

Za siku Mkuu?

Good to read from you again. Nice post.

Wako akina Lisu pia. Tutajua kadiri siku zinavyokwenda hasa Bunge lijalo la bajeti.

Respect.

Nipo mkuu wewe ndiyo ume potea.
Naona wengi wame kasirishwa na Lissu kuto kuwepo kwenye list ila haya yalikua maoni na kama unavyo jua opinion siyo fact. Nilikua naleta mtazamo tofauti tu ila Lissu nae ana jitahidi sana tu.
 
..Godbless Lema.

..Tundu Lissu.

..hao ndiyo wamelitikisa bunge.
 
Nipo mkuu wewe ndiyo ume potea.
Naona wengi wame kasirishwa na Lissu kuto kuwepo kwenye list ila haya yalikua maoni na kama unavyo jua opinion siyo fact. Nilikua naleta mtazamo tofauti tu ila Lissu nae ana jitahidi sana tu.[/B]


Correction hapo kwenye red... anafunika🙂 Hauridii mtu kuleta mswada uliojaa mawenge!
 
Najua sasa hivi tupo kwenye kikao cha tatu tu cha Bunge na kwamba mpaka ikifika miaka mitano (2015) mengi yata jitokeza.

Baadhi yenu mnaweza kusema nimapema mno kutafakari wabunge gani mpaka sasa wame jitokeza kama nyota wa Bunge ila kwa maoni yangu mpaka sasa ni hawa wawili.

Freeman Mbowe:

Kama kiongozi wa upinzani nilitegemea amake headlines zaidi ila so far kama mkinya kuliko nilivyo tarajia. Ina wezekana ni mbinu yake ila kadri siku zinavyo enda nategemea sauti yake ita sikika zaidi.


Zitto Kabwe:

Mpende mchukie huyu bwana anajua kupanga hoja na una ona uwepo wake bungeni iwe positive au negative. Pia ameonyesha uelewa mzuri wa kanuni za Bunge (zaidi ya hata speaker) pale alipo mtetea mbunge mwenzio wa Chadema wiki iliyo pita.

Halima Mdee:

Mdada anae onyesha kwamba wanawake wanaweza bila upendeleo maalumu. Ana pangilia hoja vizuri na ana pick her fights vizuri.

January Makamba:

Najua wengi humu ndani wanaweza wasikualiane nae au hata kumpenda. Ila siyo siri ni mmoja wa vijana wanao sikika bungeni na ana jitahidi kadri iwezekanavyo uwepo wake Bungeni uonekane.

Wale niliyo tegemea impact kubwa zaidi toka kwa Bungeni lakini mpaka sasa wame kuwa kimya:

John Mnyika:

Huyu jamaa siyo siri ana hulka ya kupendwa ila inaelekea approach yake ni ya ukimya zaidi yaani yeye ni mtu wa behind za scenes zaidi. Nili tegemea makeke zaidi toka kwake kwenye vikao vya bunge.

Regia Mtemi:

Huyu ni mwanaJF mwenzetu wa muda mrefu. Ali pambana sana mpaka kuja kuishia kupewa ubunge wa viti maalumu. Ila tokea apate ubunge naona kuna makosa ya kisiasa ana fanya ambayo yata kuja kumcost baadae na hata kupunguza nafasi yake ya kurudi Bungeni.



Ni january yupi, yule aliyebwabaja hoja ya kiswahili kutumika katika mabunge ya nje akijaribu kupinga maelezo ya Mdee, kisha waziri wa Chama chake akamnyamazisha!
Haina maana ya kwamba lazima kila hoja wabunge wote wasikike wameongea kama manyanya aliyejaribu kudandia Gali kwa mbele?
 
Mpaka hapo hujamtaja Tundu Lisu nina wasiwasi kama huwa unaangalia bunge la tz au la somalia! Huyu makamba naye sijui umemtoa wapi! Yeye ana maslahi yake flani asikudanganye, ametumwa huyoooo!

Ameona hafagiliwi hapa janvini akaamua kujifagilia mwenyewe, hongera
 
Sijamsikia akiongea kwenye vikao vya bunge la kumi ila kihistoria mimi huwa namzimia sana Mh. Ole Sendeka wa CCM. Hao wengine wote waliotajwa pia nawakubali ila kama ni pointi wa kwanza nampa Mungumbariki Lema
 
Hivi huyu mwanafalsafa na zitto ni ndg??au zitto mwenyewe ndo anatumia jina hilo humu ndani??kwa nini kila kitu unaanza na zitto?who is zitto anyway, the corrupted young man in opposition politics?! Badala ya kutamka tundu lissu unatutajia huyu ccm-b why?? Sioni la maana alilolifanya bungeni kipindi hiki zaidi ya kujidai kukaa karibu na tundu lissu ili naye aonekane!
 
Bila unafiki Tundu lisu anatisha na hata thithiem wanalitambua hilo.

Mungumbariki Lema anakuja juu kwa kasi ndani na nje ya Bunge pia. Hii ndyo mifuniko yangu ya zege mpaka bunge lilipofikia.
 
kumbe wabunge ni wale wa chadema tuuu.hongereni wabunge wa chadema kwa kufanya kazi ya uwakilishi vzr kama wabunge. sasa nimegundua mbunge ni kutoka cdm wengine ni maamuma
 
Anaona kwa miguu na kusikiliza kwa mdomo na kutafakari kwa makengeza ndio maana hakuona mchango wa waheshimiwa wafuatao: lisu, Mnyika, Sugu na wengineo. Kila anaposikiliza akili yake huchuja asiyoyataka na kuweka yale anayoyawaza yatokee ndiyo maana yupo kinyume na wengi kwani ukweli alionao ni ule ambao akili yake imeukoroga
 
Yeye aendelee kumsifia JM wake lakini huku site tunauliza na huyo nae? halafu tunasema hatoshi|
 
Ninapata mashaka kwa tathmini yako iliyokupa jumuisho hilo, mashaka ya kwanza ni kama kweli unafuatilia bunge la 2010-2015, unaposema mh Mnyika amekuwa kimya unamaanisha nn, je ulifuatilia wakati wa uchangiaji wa mambo ya famasia!? nadhani ulitaka kumrusha makamba tu
Hapa tuangalie wabunge wanaopewa dk10 kutoa hoja na wanazitumia dk8 kumshukuru jk, hawa wanajumuisha na j.makamba, simbachamwene, chilolo, manyanya na kina bulaya.
Hawa huwezi kuwalinganisha na kina sanya, sakaya na owenya
 
Inakwaje unamsahau Godbless Lema????????????????????????
 
Ninapata mashaka kwa tathmini yako iliyokupa jumuisho hilo, mashaka ya kwanza ni kama kweli unafuatilia bunge la 2010-2015, unaposema mh Mnyika amekuwa kimya unamaanisha nn, je ulifuatilia wakati wa uchangiaji wa mambo ya famasia!? nadhani ulitaka kumrusha makamba tu
Hapa tuangalie wabunge wanaopewa dk10 kutoa hoja na wanazitumia dk8 kumshukuru jk, hawa wanajumuisha na j.makamba, simbachamwene, chilolo, manyanya na kina bulaya.
Hawa huwezi kuwalinganisha na kina sanya, sakaya na owenya

Nadhani una changanya mambo mkuu. Mnyika hakuwepo Bungeni 2010-2015.
 
Hadi sasa
Tundu, M'nyika, Zitto, Lema, Mdehe wako njema i hope Bunge lijalo watatisha zaidi.
 
Back
Top Bottom