Najua sasa hivi tupo kwenye kikao cha tatu tu cha Bunge na kwamba mpaka ikifika miaka mitano (2015) mengi yata jitokeza. baadhi yenu mnaweza kusema nimapema mno kutafakari wabunge gani mpaka sasa wame jitokeza kama nyota wa Bunge ila kwa maoni yangu mpaka sasa ni hawa wawili.

Zitto Kabwe- Mpende mchukie huyu bwana anajua kupanga hoja na una ona uwepo wake bungeni iwe positive au negative. Pia ameonyesha uelewa mzuri wa kanuni za Bunge (zaidi ya hata speaker) pale alipo mtetea mbunge mwenzio wa Chadema wiki iliyo pita.

Halima Mdee- Mdada anae onyesha kwamba wanawake wanaweza bila upendeleo maalumu. Ana pangilia hoja vizuri na ana pick her fights vizuri.

January Makamba- Najua wengi humu ndani wanaweza wasikualiane nae au hata kumpenda. Ila siyo siri ni mmoja wa vijana wanao sikika bungeni na ana jitahidi kadri iwezekanavyo uwepo wake Bungeni uonekane.

Wale niliyo tegemea impact kubwa zaidi toka kwa Bungeni lakini mpaka sasa wame kuwa kimya:

John Mnyika- Huyu jamaa siyo siri ana hulka ya kupendwa ila inaelekea approach yake ni ya ukimya zaidi yaani yeye ni mtu wa behind za scenes zaidi. Nili tegemea makeke zaidi toka kwake kwenye vikao vya bunge.

Regia Mtemi- Huyu ni mwanaJF mwenzetu wa muda mrefu. Ali pambana sana mpaka kuja kuishia kupewa ubunge wa viti maalumu. Ila tokea apate ubunge naona kuna makosa ya kisiasa ana fanya ambayo yata kuja kumcost baadae na hata kupunguza nafasi yake ya kurudi Bungeni.

Freeman Mbowe- Kama kiongozi wa upinzani nilitegemea amake headlines zaidi ila so far kama mkinya kuliko nilivyo tarajia. Ina wezekana ni mbinu yake ila kadri siku zinavyo enda nategemea sauti yake ita sikika zaidi.

Mkuu,Inawezekanaje ukawa Umefanya Oversight ya kutomtaja Mheshimiwa TUNDU ANTIPACE LISSU,LISSU NI MASHINE AMBAYO IMEJIPAMBANUA WAZI NDIYO MAANA HATA JAKAYA ANAMGWAYA! Siamini kwamba haujaliona hilo,something isnt right here!!
Kuhusu Mbowe,Mbowe anaongoza Timu ya Watu Mahiri kupindukia ndiyo maana kuongea na hoja wanazozitoa Vijana wake kunau-preempty!! Ukiwa mtu unaongoza kambi ya watu vilaza utajikuta unalazimika kuongea sana,Mbowe anaongoza kambi ya watu with fine brains,hana haja ya kupiga kelele nyingi!!
Hata siku ya mwisho ya Bunge lililopita(kama uliaangalia) bungeni,aliipaza sana sauti yake bungeni wakati wanajadili Budgeti ya Mahakama,he was very informed,rhetoric,patriotic and eloquent,need i say more!!
Mbowe is Great,ndiye mwenyekiti wa Chama kinachoinyima Ccm usingizi,lazima ana mkono mrefu katika kuifanya Chadema iwe hivyo ilivyo leo!!!
Ni matusi Kumfananisha Mbowe na ndugu Hamadi ambaye anaongozwa na Tumbo na ndiyo maana alifanya kila hila kutaka kupindishwa kwa kanuni za Bunge ili iundwe kambi ndogo ya Upinzani ili yeye awe kiongozi wake apate Benefits zake!!!
Nawaza tu kwa sauti kuu!!!