Wabunge,nini maana ya kutumia busara kudhibiti mihadarati? Watajeni mapapa

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
16,003
Sakata la mihadaratI limezua mjadala mzito huku wabunge baadhi yao wameonakana kutetea watuhumiwa huku wakisema "busara itumike" wakati huo huo wakitaka "vifagaa" kuachwa na "mapapa" wakamatwe.

Kama wabunge wanashindwa kuwataja "mapapa" wakiwa na kinga nani atawataja?

Je wabunge watu wana maslahi gani na biashara ya mihadarati?
 
Nadhani issue ya msingi ni kuwachukulia hatua za kisheria na kuona Biashara hii inatokomea na sio kuwataja.
Kama ikibidi kutajwa basi watajwe mapapa(dons) na sio watumiaji ambao kimsingi wanahitaji tiba Muhimbili.
Ukitaja watumiaji wa mwisho na kuacha Wafadhili,Wasafirishaji,Wasambazaji na Wauzaji wengi tutakuona kama unapiga siasa nyepesi na huna malengo ya kudhibiti madawa.
 
Umesahau ile list tulioambiwa ipo ikulu kwenye awamu ya nne Imepotelea wapi?.Ni vema wakaanza nayo hiyo list .
 
Nadhani issue ya msingi ni kuwachukulia hatua za kisheria na kuona Biashara hii inatokomea na sio kuwataja.
Kama ikibidi kutajwa basi watajwe mapapa(dons) na sio watumiaji ambao kimsingi wanahitaji tiba Muhimbili.
Ukitaja watumiaji wa mwisho na kuacha Wafadhili,Wasafirishaji,Wasambazaji na Wauzaji wengi tutakuona kama unapiga siasa nyepesi na huna malengo ya kudhibiti madawa.
Kati ya 112 waliokamatwa hakuna wauzajI na wasafirishaji?
 
Kinga wanazo wakiwa ndani ya eneo la bunge wakitoka nje ya habari nyingine...
 
Sakata la mihadaratI limezua mjadala mzito huku wabunge baadhi yao wameonakana kutetea watuhumiwa huku wakisema "busara itumike" wakati huo huo wakitaka "vifagaa" kuachwa na "mapapa" wakamatwe.

Kama wabunge wanashindwa kuwataja "mapapa" wakiwa na kinga nani atawataja?

Je wabunge watu wana maslahi gani na biashara ya mihadarati?
Suala sio vidagaa wala mapapa hapa jamani wote wanatakiwa kukamatwa na kuacha mara moja huu ushetani..unapokuwa unafanya usafi huwezi kusema unasafisha uchafu mkubwa mkubwa tu na unaacha uchafu mdogo still hiyo sehemu haitokuwa safi,kamata wote.
 
Kaka nadhani inakupasa kuitathimini na kuiangalia Kauli ya wabunge kwa kina, Kwa sasa Makonda anaonekana kama ndio Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba , amekuja kuingilia haya mambo kwa mbali na hii yote inatokana na uendeshaji wa Serikali yetu ilivyo sasa, madaraka ya Makonda ni "makubwa sana".

Busara inayozungumziwa ni hii, Nchi ina vyombo ya Usalama kila kona (Polisi, Usalama, Polisi jamii nk), kama wabunge na wanajamii wanawajua wauza unga iweje Serikali isiwajue? Rais aliyemaliza muda wake JK, alisema ana majina yote ya wauza Unga, Amina Chifupa alishatoa list ya wauza unga wote sasa iweje Serikali haiwajui? Na badala yake inawafata mateja ambao ni wagonjwa?

Yaani Raisi anasema Papa anayeleta Unga Tanzania aanze kujulikana kutoka kwa Chidi Benzi au Wema, yaani Chidi ataje yeye kanunua kwa nani?, huyo nani nae aseme kanunua kwa nani?, na nani naye aseme kaupata wapi? Na huyo wapi ndio awapeleke kwa mletaji hivi hapo kuna Busara kweli? Hiyo chain ilipaswa kuanzia juu kuja chini na sio vinginevyo

Nadhani kama mawaziri wangekuwa na uwezo wa kuomba kubadirishiwa wizara?, nadhani Mwigulu Nchemba angekuwa wa kwanza kuomba apelekwe fedha, amekuwa sidelined kabisa kwenye hii issue, Issue ni ya Makonda, Sirro, Mangu na JPM
 
Kama RC anawajibika na ulinzi wa Dar.....Kwani kuna ubaya
 
Suala sio vidagaa wala mapapa hapa jamani wote wanatakiwa kukamatwa na kuacha mara moja huu ushetani..unapokuwa unafanya usafi huwezi kusema unasafisha uchafu mkubwa mkubwa tu na unaacha uchafu mdogo still hiyo sehemu haitokuwa safi,kamata wote.
Kuntu
 
Back
Top Bottom