Sijui kama nimeifahamu vizuri hoja yako, lakini kwa kutilia maanani kuwa lengo la kuwa na wabunge majimboni ni kupeleka na kutetea maendeleo ya majimbo yao, kuwazuwia wasifanye hivyo, kutakuwa na haja gani ya kuwa na wabunge? Kuwazuwia wabunge wasitoe misaada kunaweza kulazimisha mabadiliko kwa njia gani?
Ni kweli kuwa wengine, na ni wengi, hufanya hivi zaidi kwa maslahi ya kisiasa kuliko nia ya kuleta maendeleo, lakini kwa wananchi ambao wana shida, misaada hii huwasaidia sana, hasa pale ambapo serikali kuu imeshindwa kufanya hivyo.
Bahati nzuri kwa sasa wananchi wameamka kidogo, kwa hivyo ikiwa mbunge au mgombea ubunge anafanya hayo kama rushwa, ninawashauri wananchi wapokee "mlo" huo halafu siku ya uchaguzi ikifika wachague wale ambao wanahisi wana maslahi kwao na kuwatelekeza watoa rushwa.