ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Eti mpo bungeni mnasema mnapanga na kujadili bajeti ya serikali , mnapanga ni maeneo yepi fedha ya serikali ielekezwe .
Sasa naomba mnijibu maswali yafuatayo na kama mkishindwa mrudi majimboni kwenu mkasaidie wapiga kura wenu.
1: Ni lini mliwahi kukaa bungeni kujadili na kupanga ununuzi wa ndege zilizonunuliwa. Na kama hamkukaa ni nani aliyeidhinisha fedha hizo
2: Ni lini mlikaa bungeni kuidhinisha fedha kwa ajiri ya utengenezwaji wa viwanja vya ndege vya chato, mwanza ,n.k. Kama hamkukaa ni nani aliyeidhinisha mabilioni hayo kuelekezwa huko,
3: Nyinyi wabunge ndio mliokuwa mmepanga mabilioni ya shilingi kwa ajiri ya sherehe mbalimbali za kitaifa , lakini serikali ikafuta maadhimisho hayo na serikali ikaelekeza fedha hizo kwenye maeneo mengine, uamuzi ambao ulifurahiwa na wananchi wenu walio wapigia kura. Je wakati mnapanga hamkuona kwamba sherehe hizo hazina tija hadi mtu mmoja aje atuonyeshe mwanga , ina maana kwamba mtu mmoja ana akili kuliko nyie mia tatu mnao kaa hapo bungeni.
4: Kwanini muendelee kukaa bungeni miezi miwili huku mkijilipa posho kwa fedha ya walala hoi wakati mnachokipanga si ndicho serikali itakacho tekeleza, inahitji mtu afike darasa saba ili kugundua kwamba nyie mnapanga yenu na serikali inatekeleza yake? .
5: Kwa nini bunge hili la awamu ya tano msibaki na kazi moja tu ya kutunga sheria , sera na miongozo ya nchi ambapo vikao vyake ni vya wiki mbili tu na kazi ya kujadili, kupanga na kuidhinisha matumizi ya fedha ya serikali muiachie serikali ambayo ndiyo mkusanyaji na tayari wanachi tumeshaona tija yake leo hii uamuzi wa mtu mmoja wa kuamua kununua bombadier umefurahiwa na kila mtu .
Kuendelea kukaa bungeni ni kutumia fedha ya mlalahoi ovyo, kwa sababu watanzania wanaona uamuzi wa raisi wetu kuchukua fedha za serikali kuelekeza kwenye mambo anayo yaona yana tija kwa wananchi ni mzuri kuliko yale mnayompangia nyie huko na watanzania tumeridhika .lakini jambo la pili fedha zenu mnazo zipangia matumizi zina mlolongo mrefu wa kupatikana na kuzifanyia matumizi, lakini hiyo kazi kwa kipindi cha miaka miwili tumeshaona faida yake raisi akifika sehemu akakuta kuna matatizo ya maji , barabara hapo hapo anaagiza tu barabara itengenezwe wiki mbili hakuna longolongo inatengenezwa bila kujali fedha itatoka wapi.
Ushauri wangu kusiwe na bunge la bajeti kuwe tu na vikao vya bunge vya kawaida vya wiki mbili ili fedha itakayo okolewa ikafanye kazi nyingine za kimaendeleo. Kwa sababu kwa serikali ya awamu hii ya tano inaweza kwenda bila hata bunge na shughuri zikaendelea kama kawaida kwa sababu kila mtu anajua raisi ni mkali hivyo watu wanaogopa kufanya kazi kwa mazoea.
Kwangu mimi bunge ni mzigo mwingine kwa serikali unaotumia fedha nyingi halafu tija yake haionekani kwa wananchi , bunge halina tofauti na mwenge yote ni ni mizigo tu tofauti yake ni kwamba mwenge ni mzigo unaotembea wakati bunge ni mzigo uliotulia unaotafuna fedha kimya kimya.
Wabunge mjitafakari wenyewe kama mnapaswa kuendelea kuwa bungeni au la. Lakini mjue Mungu anawaona.