Wabunge hawa mishahara yoa isimamishwe

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,920
Kazi ya Mbunge bila shaka iko bungeni. Hivi mbunge anayeingia kwenye vikao vya bunge bila ya kuchangia kwa kuongea ama kwa kuandika jee anastahili kulipwa mshahara?

Mbunge anayechangia kama chizi ama asiyejua kilichoko mezani kinachotakiwa kuchangiwa naye anastahili kulipwa mshahara?

Kama kazi ya mbunge ni kuwa Bungeni kusema kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake, mawaziri nao wanalipwa mishahara ya kibunge kwa kazi gani wakati wao wako upande wa serikali? Yaani analipwa mshahara wa kufanya kazi za serikali kama waziri na hapo hapo analipwa mshahara wa kibunge wa kufanya kazi ya kuisimamia serikali!?

Wakati Spika anashughulika na wabunge asiojua wapo wapi kama Tundu Lissu, asimamishe pia mishahara ya wabunge hawa wasiofanya kazi za kibunge!!
 
Afadhali hao wanahudhuria na hawaongei labda wanaomba msaada kwa wenzao.
Kuna Mzee Nimrodi Mkono.
Na Prof Sospeter .
Hawa nasikia hawaingii kabisa bungeni wala kushiriki vikao vya kamati.
Wanakula bata tu na kupiga ishu zao binafsi
 
Ingekuwa tunaenzi tafsiri ya "the government of people, for people and by people", wakwanza kunyang'anywa mishahara ni akina Ndugai, Jiwe, na wakubwa wenzao.
Ile definition ya Civics form one kuna haja ya kuibadilisha kiukweli.
 
Afadhali hao wanahudhuria na hawaongei labda wanaomba msaada kwa wenzao.
Kuna Mzee Nimrodi Mkono.
Na Prof Sospeter .
Hawa nasikia hawaingii kabisa bungeni wala kushiriki vikao vya kamati.
Wanakula bata tu na kupiga ishu zao binafsi


Ndugu kwani Nimrod bado ni mbunge? Muhongo Sospeter ama? najiuliza pia kwani yule mtoto wa Marehemu Kigoda nae bado ni mbunge? kuna wabunge wengi sana hata Mtulia nae katulia kama kafika laooooo
 
Lkn siyo maadui ya Tanzania yetu!
Ni maadui kwa kuwa fedha wanazolipwa hawazifanyii kazi. Waulize wanaojua Kifaransa ambako ndiko hasa kwenye asili ya neno la kiingereza "Parliament" wakueleze kwa ufasaha nini maana ya neno "Parler".

"Parler" ambalo ni neno la kifaransa lilozaa neno la kiingereza "Parliament" limaanisha kuongea ama kusema. Kama mtu yupo kimya tu bungeni basi anapoteza sifa ya kuitwa mbunge kwani ni bungeni peke yake ndiko anakotakiwa afanyie kazi yake!!
 
Musukuma ,kibajaji na nkamia kwa kweli wanakula pesa za bure kabisa ni empty set za kutupa ,hata hao wananchi wanaowachagua watakuwa wa ajabu sana ila hayachaguliwi yanaiba kura kwa msaada wa chama cha kijani ,wananchi sio wa kuwalaumu .
 
Back
Top Bottom