Wabunge Chadema wataka Mbowe alipwe fedha zote anazokidai chama ili uchaguzi wa Mwenyekiti uwe Huru na wa Haki

Baadhi ya wabunge wa Chadema wameiomba kamati kuu ya chama chao kuhakikisha Mbowe analipwa madeni yake.

Wabunge hao wamedai japo haijulikani kwa uhakika ni kwa vipi Mbowe anadai wakati fedha za kuendesha chama zilikuwa zinatolewa na Lowassa na rip Ndesamburo lakini bora alipwe tu ili uchaguzi wetu uwe huru.

Mbunge mmoja ( jina kapuni kwa sasa) amedai kuwa mara zote Mbowe amekuwa akipata kura za " huruma" kwa madai kuwa amekikopesha Chadema fedha nyingi sana na chama hakina uwezo wa kumlipa.

Tunataka tuingie kwenye uchaguzi tukiwa sawa kwa maana ya hakuna anayedai wala kudaiwa na chama halafu tuone muziki wake hapo, wamemalizia wabunge hao.

Maendeleo hayana vyama!
Pumba
 
Hivi hamjashtukia kuwa hizi propaganda zenu mfu hazina effect yoyote zaidi ya kudhihirisha upunguani wenu?
 
Jina la Mbowe limewatajirisha sana uvccm maana kila anayeandika ugoro wake akilitaja tu dau linaongezeka.
 
Lakini muda wake wa uongozi ulishakwisha tangu mwezi Septemba! Na sasa tuko Oktoba. Ameshakuwa Mwenyekiti wa chama kwa vipindi vitatu mfululizo!

Ni wakati wake sasa na yeye kupumzika na hivyo kuwaachia wengine waendeleze pale alipoishia, kama ilivyokua kwa watangulizi wake akina Mzee Edwin Mtei, Bob Makani, nk.

Au unaonaje Kamanda?
"Tatizo si kuondoka je kuna mtu atafanya na kuviendeleza vitu anavyovisimamia? " Alisikika fundi Maiko akiwa anaziba expansion joint
 
Bwashee hapo kuna maoni ya jumla ya wabunge...... na nukuu ya mbunge mmoja usichoelewa ni nini au mbege haijatoka kichwani hadi muda huu!

Bwashee,.....,vilabu vya mbege...
Inawezekena maendeleo hayana vyama lakini kwako wewe mkuu, naona yana ukabila.
 
"Tatizo si kuondoka je kuna mtu atafanya na kuviendeleza vitu anavyovisimamia? " Alisikika fundi Maiko akiwa anaziba expansion joint

Nimeifuatilia Chadema tangu mwaka 2000! Chini ya uongozi wa Mbowe, chama kimeimarika sana, kuanzia vijijini mpaka mjini. Hilo sikatai.

Ila kwa sasa mambo yamebadilika. Maana kila kitabu, na zama zake. Anahitajika aje Mwenyekiti mpya atakayeweza kupambana na Mwenyekiti wa ccm, aliyehodhi kila kitu ndani ya nchi yetu kwa manufaa ya chama chake.

Mabadiliko hayakwepeki ndani ya Chadema hasa wakati huu.
 
Kuna wajumbe wengine wamempania mbowe kwenye ripoti Yake ya mapato na matumizi ya chama.Sasa hivi yeye na mweka mkurugenzi wake wa fedha Mrema Wana haha kupika hiyo ripoti wajumbe wamejipanga kuikataa
 
Mnataka kugeuza CDM kama CUF ya Prof Lipumba??
Lumumba mna dhida saana, Mnakosa usingizi pamoja na Mtungi mmnaota CHADEMA??
 
Baadhi ya wabunge wa Chadema wameiomba kamati kuu ya chama chao kuhakikisha Mbowe analipwa madeni yake.

Wabunge hao wamedai japo haijulikani kwa uhakika ni kwa vipi Mbowe anadai wakati fedha za kuendesha chama zilikuwa zinatolewa na Lowassa na rip Ndesamburo lakini bora alipwe tu ili uchaguzi wetu uwe huru.

Mbunge mmoja ( jina kapuni kwa sasa) amedai kuwa mara zote Mbowe amekuwa akipata kura za " huruma" kwa madai kuwa amekikopesha Chadema fedha nyingi sana na chama hakina uwezo wa kumlipa.

Tunataka tuingie kwenye uchaguzi tukiwa sawa kwa maana ya hakuna anayedai wala kudaiwa na chama halafu tuone muziki wake hapo, wamemalizia wabunge hao.

Maendeleo hayana vyama!
Fanyeni Proaganda ongeeni Sana lakini Mjue sisi wananchi ndio Mahakama yenu
 
Back
Top Bottom