Topical,
..sasa kama alikuwa na hoja nzuri mbona CCM walipinga kila kitu?
..kama alikuwa amezungumza masuala mazuri kuhusu muungano mbona hata wabunge wa Znz hakuna hata mmoja aliyemuunga mkono?
..hivi wewe umefurahishwa na matusi na mipasho iliyoendelea ndani ya bunge? mbona hilo ni la kusikitisha kuliko hawa CDM waliojiamulia kuondoka ukumbini?
Godfrey Dilunga-Raia Mwema
Kwa hiyo, Watanzania kupitia Bunge, wameshindwa kujua maoni ya wananchi wa majimbo ya wabunge wa CHADEMA, ambayo kwa mujibu wa malalamiko yao, Bunge limeshindwa kuwapa fursa ya kusema. Hili ni kosa la kiufundi, linalohitaji mkakati mkubwa wa kisiasa kulifunika.
Binafsi ni mpiga kura wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam. Nimuulize Mnyika; je, kitendo chake cha kukwepa kutumia kanuni za Bunge kupigania maoni yetu ambayo yeye na wenzake CHADEMA wanasema hatukusilizwa, kinatulinda kwa namna gani katika taswira hii ya uovu wa Serikali?
Nilifikiri uliomba mtizamo wangu kumbe wa wabunge CUF mimi sijui kwanini? huo ni msimamo wangu..
Alizungumza vizuri kuhusu muungano kwa mtizamo wangu mimi sijui wa wabunge zanzibar..
Hiyo mipasho ndio pre planned na zimekuja kwasababu ya behaviour ya uongozi mbovu wa kambi ya upinzani
Nikupe mfano, kina tundu wakingekuwa sober cool wakajadili leo tungewaumbua wanasiasa hasa kwenye hili la katiba
Sasa chadema wameingia kwenye siasa ambazo ccm wanazipenda porojo..personality attacks siku zimeiisha badala ya hoja kujadiliwa tunajadili watu..
ndio maana nawalaumu chadema (mbadala) wangelata hoja mbadala kabla ya kutoka, kwasababu kama waziri kivuli alikuwa akijua hayo yote prior to kikao cha bunge upo???
Godfrey Dilunga-Raia Mwema
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
Mkuu,
Wabunge wa cdm wanalifahamu bunge vizuri hasa lilivyo kwa sasa. Wabunge wa ccm wanatumia idadi yao kupitisha miswada mingi tu licha ya kupingwa tena kwa hoja na wabunge wa upinzani na hata wenzao. Ndio maana waliamua kuondoka maana ingekuwa ni kupoteza muda tu! Wamechagua kwenda kuongea na wapiga kura kuwaeleza ubovu wa mswada badala ya kumweleza spika ambaye hana anachoweza kufanya. Wameona ni bora kutokutoa maoni kuliko kuyatoa yakapuuzwa! Na kwa maoni yangu, wamechagua jambo zuri kwao na wameonesha hisia zetu. Hata mimi ningetoka maana hakuna sababu ya kuongea na mtu asiyesikiliza unachamwambia!