Wabunge CHADEMA kortini leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CHADEMA kortini leo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Oct 10, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,239
  Likes Received: 414,667
  Trophy Points: 280
  Wabunge CHADEMA kortini leo Na Moses Mabula, Tabora KESI inayowakabili wabunge wawili wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) na mjumbe mmoja wa Baraza la Vijana la chama hicho leo itatajwa katika Mahakama ya Mkoa wa Tabora wakikabiliwa na mashtaka manne. Wabunge hao ni Bw. Sylvester Kasulumbai wa Jimbo la Maswa- Mashariki na Bi. Suzan Kiwanga, Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Morogoro na Bw. Anwar Kashaga ambaye ni mjumbe wa baraza la vijana CHADEMA wilaya ya Igunga. Septemba 19 mwaka huu watuhumiwa hao walisomewa mashtaka yao na kuyakana mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa mkoa wa Tabora, Bw. Thomas Simba.Akisoma mashtaka hayo, Mwendesha Mashtaka Bw. Juma Masanja akisaidiwa na Mugisha Mbonea alidai kuwa mnamo Septemba 15, mwaka huu majira ya mchana huko katika Kijiji cha Isakamaliwa wilaya Igunga, mshtakiwa wa kwanza, Bw. Kasulumbai alitoa lugha ya matusi kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatuma Kimario. Aliendelea kwamba mshtakiwa huyo alisema: "Malaya mkubwa, huyu ndiye niliyetaka kuzaa naye mpumbavu mkubwa, DC gani huyo hana akili?. Ilidaiwa kuwa huko katika Kijiji cha Isakamaliwa Wilaya ya Igunga washtakiwa kwa pamoja walimshambulia Bi. Kimario na kumsababishia maumivi ya kichwa.Katika kosa la tatu washtakiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kumshikilia Bi. Kimario bila uhalali na kinyume cha Sheria kifungu namba (253) kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Kosa la nne wanalodaiwa kutenda watuhumiwa hao kumwibia Bi. Kimario dimu ya mkononi aina ya Samsung yenye thamani ya sh. 400,000. Upande wa utetezi unaongozwa na mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lisu akisaidiwa na wakili wa kujitegemea, Bw. Musa Kwikima. Wote walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa huru hadi leo. Watuhumiwa hao walikamatwa na polisi mjini Igunga wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo Septemba 16 na kuhojiwa, na siku iliyofuata walikamatwa tena na kuhamishiwa mjini Tabora ambako walifikishwa mahakamani.
   
 2. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Naamini haki itafuata mkondo wake na mwisho wa siku pumba na mchele vitajitenga. Naamini pia mahakama itatenda haki kama ilivyo kawaida yake! Na napendekeza pia kuwa kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, basi hata D.C naye ashitakiwe kwa kuvunja sheria ya uchaguzi yeye akiwa kada wa Sisiem!
   
Loading...