Wabunge 3 (CCM) waisaliti Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge 3 (CCM) waisaliti Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 23, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  WABUNGE 3 (CCM) WALIOISALITI BAJETI YA SERIKALI YAO
  KWA MANUFAA YA WAPIGA KURA WAO.
  Dalili ya mvua ni mawingu. Inyeshe isinyeshe kutakucha tu. Mwenye masikio haambiwi sikia na mwenye macho haambiwi tazama. Usemi wa wahenga kwamba mbio za sakafuni huishia ukingoni si dhihaka bali ni ukweli wenye maana ya lisemwalo lipo na kama halipo laja.

  Kinyongo cha serikali ya CCM kubana bajeti ya maendeleo majimbo ya wabunge machachari wanaoinyoshea vidole serikali ili iwe na ari ya uwajibikaji ni dalili tosha ya CCM kuishiwa pumzi, na kwamba sikio la kufa halisikii dawa. Hakuna ajabu wengi wako mguu pande kwa sasa kusubiria muda ufike, kwani ukombozi wa vyombo mahsusi kama hivyo ni kuyakumboa majimbo yao. Tunajua fika hawa walivyozikonga nyoyo za wapiga kura wao na baadhi kusema kokote mbuge wetu utakakoamua kwenda tutakufuata tu maana yake mbunge huyu akiamua kwenda anakoona kunamfaa ataenda na wapiga kura wake.

  Mchezo wa karata za siasa Tanzania ndo unazidi kukomaa. Wenye kuendekeza kujikomba kwa chama na serikalini ni wale wenye mwono mfupi sana, kwani wenye upeo mkubwa wapo kwa wananchi waliowapigia kura, kwani chama na serikali vitapita lakini wapiga kura watabaki wale wale wenye kuunda chama wakitakacho na serikali wanayoiridhia.

  [​IMG]
   
 2. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Nimepita hapa!
   
 3. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hao wabunge wa ccm walioikataa bajeti nawasifu sana, hiyo ndio democracy. yale mambo ya unaambiwa jump unasema how high hakuna tena. endeleeni na moyo huo huo hakuna kukubali hongo kutoka serikalini kama wengine wanavyochukua ili mradi tu waipitishe kitu ambacho kila mtu anajua hakina maslahi kwa wananchi.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wabunge waoga ndio wanaobembeleza urafiki wa kaisari. Msuto wa dhamiri zao huweka kando. Hawa watatu wametii dhamiri zao na hivyo kutokukubali wananchi wao kuwa punda wa kuendelea kubeba mizigo isiyobebeka.
   
 5. MALUNGU

  MALUNGU JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wameisaliti nyinyiem ila wamewatetea wananchi waliowachagua.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kumbuka kwamba mfumo uliopo CCM ni bado katika sera za chama kimoja kushika hatamu. Walioko ndani ya CCM wanatakiwa kwa ari na nguvu yote kutetea yote yaliyomo ndani ya serikali yao kwamba yanafaa au hayafai kwano ni lazima kushabikia vinginevyo ni msaliti.
   
 7. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Wameisaliti wapiiiiiiiiiii jamnaaa kituuuu hapo ni mavuvuzela tuu wengine hao kuonesha ni wazalendo baadae wanaachaaku sign kama yule vuvuzela aliyejifanya mzalendo akakaataaa kusign akapewa unaibu waziri.

  Kama wangekuwa serious kwannn watoroke bungeni Si wangebaki wakakataa livee.....

  Kila siku nawambia fikirini kwa hatuma mbili mbele wana siasa hawa wengi waiziiiiiiiiiiii wa mawazooo yenu
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Waliounga bajeti wanaishi kwa tabu sana.Wanajua walichofanya ni ukandamizaji kwa kizazi hiki na kijacho na hasa vijana
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna mbinu mpya iliyotumika kuwavuna wabunge wa CCM wasisaliti serikali yao, kwani mbinu ya Mwakajana wasingeirudia tena. Na papo wabunge walio kinyume cha uozo ndani ya serikali wanafahamika, hao wanawekwa kando. Lakini hatima itawaumbua tu.
   
 10. Lenja

  Lenja Senior Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa Wabunge wa CCM ndio wawakilishi halisi wa wananchi. Nikinukuu maneno ya Filikunjombe.....tatizo kubwa la Wabunge humu ndani ni WOGA ...." Wabunge kama hawa wapo wengi ndani ya CCM, NGOMA IKIKOLEA ndo mtatambua kumbe wasaliti ni wengi.......wapo....wengi tu....ila...tatizo woga...
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Yeah utamaduni wa CCM wanaotumia hauna Tofauti na utamaduni wa CPC ya China na ni kwamba CCM wanashindwa kutofautisha (intra-party mechanism) katika mfumo wa kisiasa ambao ni tofauti sana kati ya Tanzania(mfumo wa kisiasa na kiuchumi) na wa China.

  Leo hii Wabunge wapambanaji wanaonekana maadui wa chama.Akina Esther bulaya,Deo Filikunjombe n.k wanaonekana maadui.Hawa wasiopate shida waendelee kuisimamia serikali yao.Nilikuwa ninajiuliza mbona wakati wa kupiga kura hawa wapambanaji hawakuwepo?kumbe inawezekana walikuwa sidelined kwenye mkakati wa chama.Wabunge hawa wamejiandikia historia kwa ncha kali ya kalamu hata kama watajiunga na upinzani.

  It is unfortunate that Mr. president is not getting the right advice,he is not truthful or both.He is putting the cart b/4 the horse.For starters Tanzanians have been deceived,lied upon and cheated in the past by "OUR RULERS".What he could have done on resumption of office to date is to try "bring confidence".Though dauting a task.mind you I did not say "restore" because the confidence has never been there.though "worse of" at the moment if my memory does not fail me.

  Now someone somewhere will ask,how can he "bring confidence"?.fix our dilapidated infrastructures for starters,show "serious" fight against corruption,build and allow institutions work as they ought to.Then i can take a vacation and mobilze for support for him in any new policy he brings to the table.

  Otherwise,Aendelee kushindwa CHADEMA ijiandae kufanya radical reform>Maandalizi inabidi yafanyike sasa huku tukiendelea kudhibiti wezi hawa wasiendelee kufanya damage kwani kazi ya kujenga itakuwa ngumu mno kwetu huko baadae

  Prof.Wangu kwenye somo la Intelligence and defence strateggies alinifundisha kwamba ndani ya Taifa lolote ukitaka kuandaa taarifa ambazo ni reliable and durable ni lazima ujaribu kuangalia nature,trend ya policies za vyama vya siasa,makundi ya kijamii na National priorities.Prof.Ben De'mour(Hebrew University)

  Ili kuepuka udhaifu huu CHADEMA inabidi tuanze kuandaa Sera nzito kabisa na durable hasa kwenye sekata ya nishati na Madini,Gesi n.k. Taifa halina sera ya gesi hadi sasa.Nimejaribu kusoma source mbalimbali nikagundua gesi hii itachukua miaka 8 hadi tunufaike.Chadema tutakuwa kwenye position nzuri zaidi .

  Wabunge wa CCM wanaojaribu kukiamsha chama chao wanawaona maadui,Wabunge viajna kama akina Deo wangekisaidia chama hicho kuliko hata akina Nape wanachofanya nje ya chama.Adui Muombee njaa....waendelee hivyo hivyo
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka kauli hiyo, na ndio ukweli, mtu kama January Makamba na Kingwangala si waoga, wanaonekana kuwa na itikadi nzuri, lakini inapotokea kuonyesha ukweli wa wanachokiongea hadharani wanajificha ndani ya kundi la wengi.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  You know, the problem wabunge wengi wa CCM wameingia bungeni kwa sababu za kiuchumi na njaa ya vyeo kuliko maana ya uwakilishi wa wananchi. Hoja hiyo inatokana na kile ambacho pamoja na wananchi kulalamikia madai ya wabunge wao kuzidi kudai posho bila kuwaangalia wapiga kura wao, wao wametia pamba masikioni.

  Pesa za mikopo ya magari milioni 900 wabunge wengi wamezitumia kununulia magari hayo ya kifahari na kutamba nayo mitaani wakati gharama za kuyaendesha na matengenezo ni makubwa na hivyo kuwatoboa mifuko.

  Wabunge wenye kuona mbali na kujali wapiga kura wake kama Mgunge Filikunjombe, aliamua pesa hizo za mkopo kununulia ambulance za wagonjwa jimboni mwake kwa sababu serikali imeahidi miaka nenda rudi bila utekelezaji. Huyu anaonekana wazi yupo kwa ajili ya kuwajali wapiga kura wake kwa jumla kuliko mbunge anayetaka pesa za kuwazawadia mtu mmoja mmoja anayemfuata Dodoma kumwomba msaada jambo ambalo ni nje ya utaratibu wa kazi za mbunge.
   
 14. mzalendo mtanganyika

  mzalendo mtanganyika JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 301
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  kuna kila haja ya kuanza kujenga sera endelevu ili kuendelea kuikaba koo ccm. cdm ina kazi moja tu........kuwaleta ccm kwenye right sight za kuwafanyia surprise attack huku waki-buy time kufanya full scale assault na kubeba nchi 2015.hoja nzito , uvumilivu wa kisisasa na ku-attack at the right time are the only strong weapons to win this battle.................
   
 15. andate

  andate JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2,655
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  kulikimbia tatizo sio kutatua tatizo. hao wabunge walitakiwa wawepo bungeni kuipinga hiyo bajeti, na pengine wangepata wafuasi wengi wa kuipinga bajeti hiyo. hao ni kama askari anaegharamiwa na kodi ya wananchi halafu anakwepa kuwalinda wananchi. Wamewasaliti waliowapigia kura. Je pengine wamepewa kidogodogo ili wasitie timu, tutajuaje? kwa jinsi walivyokuwa wabishi halafu siku muhimu ya kupitisha bajeti ndio hawapo bungeni??????? hao ni wasaliti tu.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yeeeeeesssssssss, we can. Lets join together to fight it. Ninachofurahi vijana na wasomi wengi wanafunguka akili na kuelewa kile ambacho tunapambana nacho. Ukiona hadi vijijini moto unawaka ujue kuuzima ipo kazi, na watakaposhtukia nyumba imeteketea.

  Tunatakiwa kuwa kitu kimoja, kujenga uvumilivu, kuelimisha umma bila kuchoka, papo kujitahidi kukosoa pale ambapo wapambanaji wanapoteleza, vinginevyo tutaendekeza yale yale. Huu ndio ukomavu, maana makamanda wakikosea step katika mapambano, wanarudi kujipanga upya na mbinu mpya baada ya kusoma mkao wa adui.
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kuna mbinu nyingi katika mapambano, na kina mbinu ina advantage na disadvantage. Chadema baada ya uchaguzi walianza na kulikimbia bunge na kikwete, mbinu hiyo ilizaa matunda kwa serikali kunyong'onyea na kuanza harakati za Katiba kitu kinachoendelea hadi sasa. Mbinu nyingine waliyotumia ni mikutano ambayo ilisaidia kuelimisha umma, kama wangekubali na vitisho vya kusitisha hayo haya yanayotokea leo yasingetokea, ingebaki kama ilivyokuwa NCCR Mageuzi kilipokuwa chama cha msimu na kuibuka wakati wa uchaguzi tu.

  Hawa wabunge waliotoka nje ya kikao wakati wa kupiga kura ya kupitisha bajeti, dhamiri zao ziliwasuta kutokukubaliana, na hivyo kutoka nje ya kikao ni mojawapo ya option itumikayo katika mabunge mengi duniani. Wanacho cha kuwaelewa wapiga kura wao kivitendo kwamba waligomea bajeti hiyo na kutoka isijeonekana wamshiriki kupitisha.
   
 18. B

  Bob G JF Bronze Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wasaliti ni wale waliounga mkono bajeti Dhaifu na wasaliti wengine ni wale waliokimbia bunge kuogopa kupinga bajeti hadharani
   
 19. v

  vedastus albogast Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 23, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hiyo ni passive resistance
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Chadema wangetoka nje ya ukumbi wasingekuwa wasaliti wa bajeti ya serikali, sasa kwa kuwa waliotoka nje ya ukumbi walikuwa wa kutoka chama cha Magamba basi wanavishwa ngozi ya usaliti? How can I get your point?
   
Loading...