Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewaanika wabunge 15, waliobainika kuchukua posho za safari bila kusafiri huku wengine wakikatisha safari zao.
Akizungumza katika mahojiano maalumu jana na mwandishi wa gazeti hili, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashililah, alisema tayari fedha hizo zimesharejeshwa kwa kukatwa kwenye mishahara yao.
Dk Kashililah alisema baadhi ya wabunge waliomba wasikatwe fedha hizo kwenye mishahara yao, badala yake wazirejeshe wao wenyewe.
Hata hivyo, Katibu huyo wa Bunge alisema wabunge hao walishindwa kusafiri kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuwa na ugeni wa viongozi wa chama na matatizo ya kifamilia.
"Kwa mfano Komba (Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba) alishindwa kwenda kwa sababu ya kutembelewa na ziara ya Katibu wake wa Chama (Abdulrahman Kinana) muda wa safari ukamalizika hivyo akashindwa kusafiri na taarifa zilikuwepo ofisini," alisema Dk Kashililah na kuongeza.
Akizungumzia safari ya Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani, Freeman Mbowe nchini Uingereza, Dk Kashililah alisema Bunge halina uwezo wa kumzuia mbunge yeyote kufanya shughuli zake safarini baada ya kumaliza jukumu lililompeleka.
Dk Kashililah alisema Mbowe alikamilisha ziara yake ya Bunge na kwamba baada ya hapo aliendelea na shughuli za chama chake nchini humo.
"Suala hili lilikuwa limebeba hisia za kisiasa, baada ya kusikika tu bungeni basi vyombo vya habari vikaanza kuwahukumu wabunge ni mafisadi bila hata kutafuta ufafanuzi kutoka wetu. Sisi taarifa hizo tulikuwa nazo kabla ya hata ya kuibuka bungeni, lakini lilivyotafsiriwa sikupenda," alisema Dk Kashililah.
Dk Kashililahb alisema, "Bunge lilikuwa limeratibu jumla ya safari mbalimbali zilizokuwa zimependekezwa na Kamati 16, lakini hazikufanikiwa kwenda zote kwa pamoja.
Alisema ziara zote za kamati huandaliwa kwa mujibu wa kanuni ya 117 ambayo inazipatia mamlaka Kamati hizo kuandaa ziara inazooana zina manufaa kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
Source: Gazeti la Mwananchi tar.29/12/2013
More info:

OFISI ya Bunge imeanza kuwakata mishahara wabunge 10 waliobainika kulipwa posho za ziara za kikazi za kibunge ambazo hawakusafiri na baadhi yao kukatisha safari zao njiani. Hatua hiyo imetangazwa jana na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashallilah, katika mahojiano maalumu aliyoyafanya na baadhi ya vyombo vya habari, Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.
Alisema huo ni utaratibu wa kawaida unaotumiwa na ofisi yake kurejesha fedha za Bunge ambazo hazikutumika kama ilivyokusudiwa, isipokuwa kwa wabunge ambao hukubali kwa hiari yao kuzirejesha.
Dk. Kashilillah aliwataja wabunge ambao mishahara yao imeanza kukatwa kuwa ni Mbunge wa Mbinga, John Komba (CCM), Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage (CCM) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).
Wengine ni Mbunge wa Hai ambaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (Chadema), Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Kawawa (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Matiko (Chadema), Mbunge wa Viti Maalumu, Joyce Mukya (Chadema) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM).
Alipoulizwa kama uamuzi huo ni hatua za kuwaadhibu wabunge hao kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kibunge, alisema hakuna mbunge anayeadhibiwa, bali ni utaratibu wa kawaida ambao umekuwa ukitumika kwa muda mrefu.
"Hakuna mbunge anayeadhibiwa hapa, huu ni utaratibu wa kawaida kabisa, kwa sababu Ofisi ya Bunge inazo taarifa zote za wabunge, hivyo hata wale ambao tuliwalipa lakini hakuwasafiri au walikatisha ziara, taarifa tulikuwa nazo mapema kabla hawajaanza kuumbuana bungeni.
"Hayo waliyoyasema bungeni ni mambo yao ya kisiasa, lakini ofisi yangu ina taarifa zote za wabunge 15 ambao hawakusafiri au walikatisha safari zao. Wapo waliokwisharejesha na ambao hawajarejesha, hawa ofisi ya uhasibu imekwishaanza kukata mishahara yao," alisema Dk. Kashilillah.
Chanzo:Mtanzania