ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,065
- 61,398
Mjini hapa maisha ya ajabu sana.watu wametengeneza system ilimradi wapige TU hela.mtu umepanga chumba unaambiwa kila mwezi utoe hela ya kuzolewa takataka shilingi 5000 hio kampuni yenyewe ukiangalia Ni wazembe gari lenyewe badala ya kupita kila week Kama inavyotakiwa linapitaka kwa mwezi Mara moja au wakati mwingine halipiti kabisa.bado tena Kuna hela ya sijui Ni ulinzi shirikishi hatujui Kama hata Ni kweli wanalinda eti kila mpangaji atoe 5000.kwanini hii hela asitoe mwenye nyumba.bado hela ya maji,umeme hata Kama hutumii umeme Sana unatakiwa utoe 10000.kwa hiyo Mambo yote haya ukifikiria Ni kuumizana tu Ni mirija watu wanajiwekea kupiga hela.