Wabongo Michigan (TAMI) waenda Cedar Point Park (Picha)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
wadau Michigan wafurahia Summer huko Cedar Point



baadhi ya wanajumuiya wa Michigan katika matembezi hayo




Ankal,

Jumamosi Jumuiya ya Watanzania michigan TAMI iliandaa siku ya kujumuika pamoja katika kutemebelea viwanja vya maonesho ya bembea za aina mbalimbali na burudani huko Cedar Point kwenye Jimbo la Ohio.







Wanachama na familia zao pamoja na Watanzania wengine ambao walipenda kushirikiana nasi tukiwa na marafiki zetu wengine kutoka England, na Congo tuliweza kujumuika katika kufurahia majira haya ya joto kwenye viwanja hivi maarufu ambapo wenye kuthubutu waliweza kupanda bembea ziendazo kasi na kushuhudia burudani nyingine mbalimbali. Mjumuiko huu ni wa kwanza kwa mwaka ambapo TAMI imelipa gharama nusu ya tiketi na kukodisha usafiri wa kwenda huko.



TAMI imeandaa shughuli nyingine za kutuunganisha Watanzania pamoja katika furaha, umoja, upendano na udugu ambao msingi wake ni kuheshimiana, kushirikiana na kuwa pamoja katika shida na raha. Wiki ijayo TAMI inashirikiana na jumuiya za Wana Afrika Mashariki wenzetu katika kuandaa sherehe ya Siku Kuu ya Uhuru wa Marekani, Julai 4. Mwishoni mwa mwezi wa saba TAMI imeandaa vile vile burudani ya muziki wa "kukata na shoka" katika tarehe, muda na mahali ambapo tutathibitisha baadaye.



Zifuatazo ni baadhi tu ya picha za baadhi ya wanachama wakiburudika Cedar Point. Unaweza kuona picha zaidi kwenye tovuti yetu ya:
http://www.tamiusa.org
Asante
Wadau Michigan!!

 
Kuna mdada anam dangle mtoto hapo utafikiri kafundishwa kubeba mtoto na Michael Jackson.

michael-jackson-dangling-baby-son.jpg
 
Mimi nilikuwa nachokoza makusudi wenyewe waliomo katika picha wajitokeze kama joka la mdimu, mwambie dada yetu child protective agencies wakiziona hizi picha ana kesi.

Y'all had a good time man, I was chillin with my peeps somewher on some beach sound overlooking som.e islands eating fish and chips, looking at the ducks.

But you're not gonna see me posting pics up in here, too many crazies posting crazy remarks about sisters dangling babies.

No sir, not me.Plus I ain't even sure the Feds aren't on my trail already.
 
Kutoheshimu faragha za wengine, unatawanya taswira za wenzako kwenye tandao la wazi huku wewe mwenyewe haumo, unyonyaji wa kuaminiwa.
 
Kutoheshimu faragha za wengine, unatawanya taswira za wenzako kwenye tandao la wazi huku wewe mwenyewe haumo, unyonyaji wa kuaminiwa.

umejuaje kama simo? na unajua sijaheshimu faradha za watu? Unafikiri naweza kuweka picha za watu bila wenyewe kuridhia? Ukienda kwenye tovuti yetu unaweza kubahatisha kuniona.. LOL
 
Ukienda kwenye tovuti yetu unaweza kubahatisha kuniona.. LOL

"Kubahatisha" kukuona, maana unachomoa kuoneka ovyo, za wenzako unawabandika kwenye tandao la wazi. Eti umepata idhini yao, wewe si unatangaza jumuia na kutapakanya taswira, we mbona haumo?

Mkubwa, sio poa hiyo.
 
Back
Top Bottom