...sikuelewi hapo,tuwe wakweli kidogo,hiyo JKT,Ruvu sec na kilosa whatever it s zimesaidia nini kilimo?hata hayo magereza ni sifuri kwenye kilimo...chakula kingi bado tunaagiza nje kuliko tunachozalisha,dawa ni watu binafsi wanaoelewa namna ya kupata mikopo na utaalam ndio watasaidia kilimo lakini hizi siasa za Kilimo kwa wote or sijui kwanza ni mipango failure tuu
naelezea kuhusu kujifunza uzalishaji kama wewe ulipita jkt enzi hizo utaona tulikuwa tuna zalisha , hata ukiachana na mazao makuu kama mahindi na mpunga, kulikuwa na bustani za mboga na ufugaji, tatizo ilikuwa mkuu wa kambi lazima ampeleke mkinsi mazao, na yeye mwenyewe achukue, maaaskari wa chini wachukue, kwa hiyo uzalishaji bora kwa mantiki hiyo ulikuwepo, tatizo tulikuwa na mapungufu katika nidhamu ya utunzaji, ruvu sekondaty na shule za kiliso na vyuo vya kilomo vilikuwa vinaongezea hiyo elimu ya kilimo, na kuonyesha kwa matendo uzalishaji bora wa mazao mimi nilipita tengeru niliona , ukiriguru, uyole kote huko elimu hiyo ilikuwepo sasa hili la mkorea labda useme kwenye usimamizi ndio tujifunze toka kwao.
kwa sasa hilo la ruvu sec, jkt, kilosaetc huwezi kuona kwani investment zote zimeenda chini, yaani tume kata tamaa kwamba hatuwezi au hakuna mwenye kuona kwamba hivi ni vituo vya kujifunzia na ni vya uzalishaji pia.
Kwa mfano kuna rafiki yangu alikfanya research akawa anataka kuuza nje mboga mboga, za JKT akakuta kuna ********* ndio kashikilia, basi ujue uongozi ndio ulipokuwa una pata kidogo dogo chao.
Ikiwa Kenya wanaweza ku-export maua, iweje sisi tushindwe kuzalisha chakula kingi chenye obora na kuuza nje? Hivi sasa waelewa rukwa walikuwa wa supply mahindi WFP kwa ajili ya wakimbizi kigoma, je wajua kwamba kuna watu kwa wakati mbali mbali walipewa vibali vya ku-export mahindi nje? lakini akiwa mkulima mwenyewe ana nyimwa hicho kibali kisa nchi ina njaaa.
Je huyu mkulima yeye hataki faida? mkorea tuna mruhusu sisi wenyewe kwa wenyewe tunawekeana hiana. kutakuwa na motisha hapo.