Wabeza kauli ya Waziri Mkuu Pinda

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
WASOMI na wanasiasa wamesema kitendo cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuirejea kauli yake ya kukemea mashangingi kinaonyesha jinsi mtendaji huyo mkuu wa serikali asivyojua wajibu wake na kutokuwepo kwa uwajibikaji.

Juzi akiwa mjini Dodoma, Waziri Pinda alisema kumekuwa na mashindano ya mawaziri kununua magari ya kifahari, badala ya kupunguza matumizi na kuwasaidia Watanzania masikini.

Waziri Pinda, ambaye alikuwa nje ya nchi kwa ziara ya kikazi, alionyesha kushangazwa na jinsi viongozi wa serikali ya India wanavyotumia magari ambayo si ya kifahari na kueleza kuwa viongozi wa wilaya hawana budi kuanza kununuliwa magari ya thamani ya chini ya Sh100 milioni.

Waziri Mkuu aliwahi kutangaza kuwa serikali imeamua kutonunua tena magari hayo, lakini alitoa kauli hiyo wakati shehena nyingine ya magari ya kifahari ikiwa njiani kuja nchini.

Akizungumza na Mwananchi jana, mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Mwesiga Baregu alisema: "Mimi nilivyosikia waziri mkuu kasema hivyo, nilicheka na kujiuliza maswali mengi sana.

Kauli hii inaonyesha udhaifu wa serikali na pia inaonyesha waziri mkuu haelewi majukumu yake. Yeye ana uwezo wa kumshauri rais na kupanga mambo ya msingi ya serikali.

"Kulalamikia magari ya kifahari serikalini ni kilikuwa kilio cha wananchi kwa serikali, sasa wananchi wanategemea majibu na siyo serikali kulalamika tena kwa wananchi. Kauli yake inaonyesha kuwa anawashitaki mawaziri na makatibu wakuu kwa wananchi."

Alisema serikali inapaswa kueleza aina ya magari ambayo inataka yatumike serikalini na siyo kuwalalamikia wananchi.

Profesa Baregu alisema bado wananchi wanahitaji majibu mengi ambayo serikali imekuwa ikiyakalia kimya kwa muda mrefu.

Alisema majibu ya masuala ya ubadhirifu wa fedha serikalini na mikataba tata bado wananchi wanahitaji majibu yake na si malalamiko.

Naye katibu mkuu wa NCCR Mageuzi, Samuel Ruhuza alisema kauli za Waziri Pinda zina lengo la kuwaridhisha Watanzania na hazina ukweli wowote.

Alisema pia kuwa lengo la kauli hizo lengo ni kujijengea mazingira mazuri ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

"Kusema kweli waziri mkuu katushangaza sana kwa kuwa kwa sasa anataka kuonyesha kuwa serikali inajali matatizo ya wananchi kwa kuwa itapunguza matumizi kwa kununua magari ya bei nafuu.

Tunajua kuwa yeye alikuwa mtu wa usalama na hivyo anajua kitu watu wanachotaka kusikia, hivyo anatumia fani yake hiyo kuwalaghai Watanzania," alisema.
 
Anayejua anayeitawala dunia na Tanzania hahangaiki sana na kushangazwa na matukio ya ajabu yanayoikumba Tanzania na dunia kwa ujumla.Hawa si viongozi,ni puppets wa powerful agents in Washington and London.They are controlled by remote control!

Kwa hiyo hawana maamuzi yao, wanatekeleza maamuzi ya watu wengine.Linalolo nishangaza hata hivyo ni kwa nini wamekubali kuingia mikataba ya kipuuzi kabisa na watu hao huku wakijui kwamba nia yao ni ku-enslave watanzania na mankind kwa ujumla.
 
Waziri Mkuu pinda kamshangaza kila binadamu lakini si vibaya kama atachukua hatua badala ya kuendelea kulalama.
 
Labda inaweza kusaidia kidogo katika kuwafanya watumishi kufanya mamabo ya kweli katika maendeleo ya taifa letu
 
Maana yeye ndiye mwenye mamlaka yote na hizi zote ni Kampeni kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, Labda aje yeye na mfano wa kununua gari la aina yake ndio watu wengine wafuate
 
Maana yeye ndiye mwenye mamlaka yote na hizi zote ni Kampeni kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, Labda aje yeye na mfano wa kununua gari la aina yake ndio watu wengine wafuate

mie nadhani labda anunue kile kigari sijui huwa kinaitwa nini kwa Kingereza kiswahili Mwendo wa kobe -na wengine wafate tujaribu ku cut -cost
 
Yeye mwenyewe moja wapo alipomaliza tu mkutano amepanda VX lake na kuondoka zake, Pinda labda anunue kikobe na sisi ndio tutamfuata
 
Hawa ndio viongzo wetu, mchana wanaongea usku wanafanya yale yale mambo wanayokataa mchana
 
Waziri Mkuu pinda kamshangaza kila binadamu lakini si vibaya kama atachukua hatua badala ya kuendelea kulalama.


Mnashangaa ya Pinda kutoelewa taratibu za serikali anayoiongoza inavyonunua mashangingi? Mbona mkulu wa kaya nae alishasema kuwa haelewi sababu kwanini nchi anayoiongoza ni masikini!! Na inaelekea mambo bado, kwani hata FISADI PAPA Lowassa nae kaibukia makanisani anahubili juu ya ufisadi!!Inaelekea tutashangaa ya Mussa lakini ya firauni bado yanakuja!!
 
Namshauri Pinda aende Rwanda halafu Kagame atamwambia cha kufanya. Akishindwa basi apeleke 24 hours resignation notice kwa Kikwete ili tuanze upya.
 
la kushangaa ni sisi wapiga kelele hivi akija mwenye akili anaweza kuuliza kati ya anaepiga kelele na anaepigiwa kelele nani ziko fiti (sina jibu)
 
Mnashangaa ya Pinda kutoelewa taratibu za serikali anayoiongoza inavyonunua mashangingi? Mbona mkulu wa kaya nae alishasema kuwa haelewi sababu kwanini nchi anayoiongoza ni masikini!! Na inaelekea mambo bado, kwani hata FISADI PAPA Lowassa nae kaibukia makanisani anahubili juu ya ufisadi!!Inaelekea tutashangaa ya Mussa lakini ya firauni bado yanakuja!!

Hii kali nashindwa kucheka ,
 
Back
Top Bottom