Wabaya wa CHADEMA wavurugana!

Wabaya wa CHADEMA wavurugana!

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,170
Reaction score
162,607
SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu kufichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare, baadhi ya wahusika wameanza kuvurugana.

Kwa mujibu wa Lissu, njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA.

Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare.

Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.

Jana gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.

Vile vile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu' huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana kuhusu kuvuja kwa siri zao.

Saumu akiwa katika grosari maarufu kwa jina la Kwa Kimaro jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.

"Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda," alitamba.

Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling'aka: "Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?"

Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake' aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA.

"Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?" alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.

Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.

Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana.

Katika madai yake, Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.

"Awali walipewa 400,000, wakapewa tena 300,000, pia wakapewa 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa," alisema Lissu.

Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.

Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kama anahusika nazo kwa namna yoyote.

CHANZO:TANZANIA DAIMA

MY TAKE:
HUU NI MWANZO TU WA KUUMBUKA!
 
SIKU moja baada ya Mkurugenzi wa Mambo ya Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu kufichua njama zinazofanywa ili kutengeneza ushahidi wa uongo kwa ajili ya kuutumia katika kesi ya ugaidi inayomkabili Wilfred Lwakatare, baadhi ya wahusika wameanza kuvurugana.
Kwa mujibu wa Lissu, njama hizo zinafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama na ujasusi ili kutumia ushahidi huo mahakamani dhidi ya Lwakatare ambaye ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA.
Alisema kuna baadhi ya vijana wa CHADEMA wa Idara ya Ulinzi na Usalama wanaopewa fedha na kuahidiwa kufundishwa namna ya kuzungumza katika kesi hiyo ya Lwakatare.
Lissu alisema kuna baadhi ya vijana wakiongozwa na Saumu Mulugu ambaye alifukuzwa kazi CHADEMA mwanzoni mwa mwaka jana, wamepokea fedha kutoka kwa kigogo mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa) ili kufanikisha mpango huo.
Jana gazeti hili lilimnasa Saumu akiwa anawasiliana na wenzake, huku akiwatuhumu baadhi yao kuwa ndio waliovujisha siri kwa Lissu.
Vile vile alionekana akiwasiliana na kigogo mmoja wa CCM ambaye alikuwa akimwita ‘mkuu’ huku akimsomea baadhi ya taarifa zilizoandikwa magazetini jana kuhusu kuvuja kwa siri zao.
Saumu akiwa katika grosari maarufu kwa jina la Kwa Kimaro jirani na eneo la Benki Kuu ya Damu Salama Mchikichini jijini Dar es Salaam, alisikika akiwalalamikia wenzake kwa kumsaliti na kuvujisha mkakati wao kwa Lissu.
“Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda,” alitamba.
Saumu ambaye alikuwa akizungumza kwa sauti kubwa ya ghadhabu kupitia simu, aling’aka: “Nyie kwanini mmeniuza kwenye ishu ambayo tumeipanga wote?”
Baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ‘mkuu wake’ aliendelea kupiga simu akimlalamikia mtu ambaye hakumtaja, kuwa alikuwa amezima simu yake makusudi kwa kuwa ndiye alivujisha siri zao kwa CHADEMA.
“Mimi sitakubali na nimehakikishiwa na bosi wetu kuwa huyo aliyetusaliti tutatumia wale askari kumwekea hata unga. Haiwezekani fedha tumepokea za kwanza, za pili na tatu kwanini tuuzane dakika za mwisho?” alidai Saumu huku akiendelea kugida bia yake.
Huku akihaha huku na kule, Saumu alikuwa akiwapigia simu baadhi ya madereva wa CHADEMA makao makuu na kuwaomba simu za baadhi ya watu, na hata wakati mwingine kuwafokea akidai ndio waliofichua siri hiyo.
Hata hivyo, baada ya kutilia shaka nyendo za chanzo chetu kudaka siri zake, ghafla alitokomea na kuzima simu zake mara moja kwani hata alipotafutwa baadaye hakupatikana.
Katika madai yake, Lissu alisema hadi sasa vijana hao wameshapewa sh 400,000 ili wakubali kwenda kufundishwa jinsi ya kuzungumza mahakamani kuwa CHADEMA ni chama cha kigaidi, kwamba Lwakatare alipanga mikakati ya kigaidi.
“Awali walipewa 400,000, wakapewa tena 300,000, pia wakapewa 35,000 mara mbili. Na fedha zote hizi walikuwa wanapewa kwa njia ya M-Pesa,” alisema Lissu.
Alidai kuwa Saumu ndiye anayeratibu mpango wote kati ya Jeshi la Polisi na vijana hao wa CHADEMA kwa kuwarubuni kwa fedha.
Alisema vikao baina ya vijana hao wa CHADEMA na Saumu vimewahi kufanyika mara kadhaa katika moja ya hoteli maarufu nchini juu ya mambo ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari au mahakamani kwenye kesi ya Lwakatare.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizo kama anahusika nazo kwa namna yoyote.

CHANZO:TANZANIA DAIMA

MY TAKE:
HUU NI MWANZO TU WA KUUMBUKA!
Wabaya wa chadema wako wengi tu mfano,Lema,Zitto, Mbowe na hata Kitila
 
Watatajana hadi mshangae na mkuu wa kaya anavyoelekeza.Kwa uhakika nilio nao,hakuna sehemu ya ajira hapa nchini ambako CHADEMA haina mtu!Huko wanakopitisha ma M-PESA,AIRTEL M,TIGO,Walimu,Jeshi,Polisi,Usalama wa CCM wamejaa tele...Hebu jaribu kufanya urafiki na wajeshi wachache halafu uwadodose uone kwamba km si waakati tu umebakia magamba yasepe!KILA MAHALI na wako tayari kuacha kazi..Chezea CDM wewe!
 
Mungu ni mkubwa kuliko pesa. Haya sasa wanaanza kujichanganya na Mungu anawachekelea taratibu. Jamani wao wana pesa sisi tuna Mungu.
 
Kuna siku hata shetani nae atachoka kushirikiana na Mwigulu kuikandamiza cdm,wish kwa cheo alichonacho angejitahidi kutangaza sera za chama na kukisuka upya chama chao ili kibadilike na kurudi kwenye misingi yake aliyoiacha Mwalimu na hata BWM kuliko ilivyo sasa
 
Wabaya wa chadema wako wengi tu mfano,Lema,Zitto, Mbowe na hata Kitila

Umekunywa chai....?? kama bado karibu hapa Brajec Grill napata supu....nitakununulia....maana njaa inakomenti zake
 
Chanzo Tanzania Daima ha ha ha yaani ukiisoma hiyo habari ni sawa wameandikiwa wale machizi wa Mirembe ha ha ha Chadema kama ndio style zenu za kupambana na ukweli ki-dizaini hii basi RIP
 
Hicho chanzo cha hiyo habari sina imani nacho. Hiyo ni habati ya kusadikika tu inaonesha ni jinsigani CDM inavyo tapatapa
 
Umekunywa chai....?? kama bado karibu hapa Brajec Grill napata supu....nitakununulia....maana njaa inakomenti zake

mimi sijanywa chai lakini siwezi kuwa kama makupa ahahahaaaaaa sio mbaya ila inakuwa mbaya pale unapoiendekeza,,njaa tuzitumie kama changamoto kuhustle kuondokana nayo kihalali lakini wenzetu wanona bora wapakatwe na kulambalmab miguu ya magamba ndio wale,ahahahaa nitakufa njaa yangu bhana
 
Chanzo Tanzania Daima ha ha ha yaani ukiisoma hiyo habari ni sawa wameandikiwa wale machizi wa Mirembe ha ha ha Chadema kama ndio style zenu za kupambana na ukweli ki-dizaini hii basi RIP

Mbona muhusika ametajwa?
 
Mi nilishasema siku nyingi, huu utitiri wa vijana wanaojifanya wanauchungu na hii nchi ni janga la kitaifa....Wengi wapo kwenye siasa kwa maslai binafsi hivyo wanatumika ovyo katika mambo ya kijinga kabisa! What is TZS 400,000/=.....nA HAWA HAPO CDM WAMEJAA TELE NJAA TUUU INAWAWEKA KUWA KARIBU NA CHAMA. NAOMBA SASA HIVI VIJANA WOTE WALIOPO HAPO MAKAO MAKUU LAZIMA IJULIKANE WANAFANYA KAZI GANI ZA KUAJIRIWA NA SIO KUSHINDA HAPO
 
Jaman naomba mnielezee maana ya cdm

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
kuwa wapuuzi ambao bado wanasoma tanzania daima gazeti la mbowe lilijaa wachaga wa hai
 
"Kwanini mmelikisha siri zetu kwa Lissu hadi amejua tulikutana katika hoteli ya kifahari na Mwigu? Sasa nitawaonesha, maana laki tano zenu ninazo mimi. Siwapi bali nitazitumia kujilinda," alitamba.
Laki tano tu, toba! kweli Yuda alimuza Yesu Kristu kwa pesa ya kumununua mtumwa mgonjwa. Vijana tujifunze kufanya kazi, mbona ukilima tuta zako mbili za mchicha utapata zaidi ya hiyo laki tano kwa mwezi. Sasa mnategenezeana bifu, na huenda mkatoana roho kwa ajili ya laki tano tu.
 
Back
Top Bottom