Wabambwa wakitengeneza noti 'gesti'

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
JESHI la Polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa wakiwa wanatengeneza noti bandia kwenye nyumba ya kulala wageni ya Kisale iliyopo
mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Bw. Michael Kamuhanda amesema kuwa tukio hilo limetokea jana saa tano usiku huko katika nyumba ya kulala wageni Kisale iliyopo mtaa wa Matomondo eneo la misufini mjini hapa.

Kamuhanda aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Daniel Lukinja (66) Mkazi wa Namtumbo, Emmanuel Eruka (29) Mkazi wa Manispaa ya Morogoro na Fransis Soko (54) Mkazi wa Bombambili Songea Mjini.

Amesema kuwa siku iyo ya tukio Askari Polisi wakiwa kwenye doria waliwakamata watuhumia hao wakiwa na makaratasi yanayodaiwa kutumika kutengenezea noti bandia

Alieleza kuwa makaratasi hayo yaliyokamatwa ambayo yalikuwa yameifadhiwa kwenye box yalikuwa yatumike kutengenezea noti bandia ambazo idadi yake haikuweza
kufahamika mara moja kwa ajili ya kutaka kumuibia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi.

Watuhumiwa hao walikutwa kwenye chumba kimoja ambamo ndio walikuwa wakifanya shughuli hizo kwa muda mrefu hadi taarifa zikawafikia raia wema ambao waliiarifu polisi hadi kukamatwa kwao.

Alisema kuwa polisi inaendelea kufanya uchunguzi wa kina
ili kubaini ukweli wa jambo hilo na kwamba watuhumia hao watafikishwa mahakamani mara tu upelelezi utakapo kamilika.
 
Watuhumiwa hao walikutwa kwenye chumba kimoja ambamo ndio walikuwa wakifanya shughuli hizo kwa muda mrefu hadi taarifa zikawafikia raia wema ambao waliiarifu polisi hadi kukamatwa kwao.

Sidhani kama ni noti mpya it takes time hadi watu waanze kutengeneza noti mpya kwanza inabidi wasistudy unless wanacapitalise advantage kwamba watu bado hawajazizoea noti mpya na itakuwa rahisi kuwachanganyia
 
mkuu fake zipo tayari kwenye mzunguko...
pia ni rahisi kuwachanganya watumiaji hasa wa mikoani hasa wakulima na wafugaji kwa sababu hawajazijua vizuri...
pia kuna watu hawajazipata wapo tayari kununua elfu kumi kwa 11,000 au buku kwa 1,200 hao ndio watz halisi
 
myself i have seen the fake bill this weekend in the street..take my word bro kuna watu ndo kazi yao hiyo
 
mkuu fake zipo tayari kwenye mzunguko...
pia ni rahisi kuwachanganya watumiaji hasa wa mikoani hasa wakulima na wafugaji kwa sababu hawajazijua vizuri...
pia kuna watu hawajazipata wapo tayari kununua elfu kumi kwa 11,000 au buku kwa 1,200 hao ndio watz halisi
bongo tambarare kila kitu kinawezekana
 
nchi kwishen hv mchina anafanya hv kwa nchi zote duniani?

tatizo sio mchina kaka....tatizo ni wafanyabiashara...hivi unafikiri mfanya biashara ukiletewa the same nokia original lets say ni 50 dollars na fake ambayo ni karibia ifanane na original kwa 10 dollars atachukua ipi? hasa hawa wafanyabiashara wa hizi nchi zetu
 
am agreed with you na kudhibiti haiwezekani maana tbs ni watoto wa vigogo
 
Wachina wanatengeneza hadi spare za scania, bus linawekwa weak brake pipe ya kichina,driver akifunga brake kitonga pipe inaburst kinachofuata ni majonzi
 
Mchina sio wa kulaumiwa,wakulaumiwa ni Serikali-all fake and counterfeits zinapita TRA(serikali) why wanapokea Tax? Uwezi pitisha conteina kwa njia za panya iweje matani na matani ya fake products and movies kwa mfano yanaingizwa kila kukicha apa Tanzania na TRA awafanyi kitu?
Zipo mpaka fake dolars,so Serikali yetu inatakiwa kuwa na kitengo cha kuchunguza haya.Na ata uko China awawezi print note chache lazima ziwe nying so sio kitu cha mtu mmoja ni makundi ya watu!
Pia wanaweza ata kuwa awa awa wawekezaji toka China tena uwenda wakawa wanazichapisha apa apa Bongo,kwani aiji akilini mchina auaza maua ya plastik,ana endesha vogue na anaishi Masaki kodi dola 5000 kwa mwezi kwa biashara ya maua ya plastic!
Tanzania ni shamba la bibi na litaendelea kuwa Shamba la bibi.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.....
 
njia za panya kama zipo nyingi inawezekana
 
Back
Top Bottom