Waasi wa CAR wakataa pendekezo la rais Bozize

Waasi wa CAR wakataa pendekezo la rais Bozize

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
[h=1]Waasi wa CAR wakataa pendekezo la rais Bozize[/h]
31 Disemba 2012 12:06
121228044815_sp_protests_in_central_african_republic_144x81_reuters_nocredit.jpg

Waasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wamekaribia mji mkuu wa nchini Bangui na wamepuuzilia mbali, tangazo la rais wa nchini hiyo Francois Bozize, siku ya Jumapili, kuanzisha mazungumzo ya amani na viongozi wao.
Msemaji wa waasi wa Eric Massi, ameiambia BBC kuwa, ni vigumu sana kwao kumuamini rais Bozize, kwa sababu wanajeshi wake wanaendelea na harakati za kuwashambulia wapiganaji wao mjini Bangui.
Amesema, ikiwa jeshi la kutunza amani la Muungano wa Afrika , halitatumwa mjini Bangui, waasi hao wataingia na kutoa ulinzi wa wafuasi wao.
Lakini serikali ya nchi hiyo imekanusha madai hayo, ya kuwafanya mashambulio dhidi ya wafuasi wa waasi hao.
Siku ya Jumapili, rais Bozizi alitangaza kuwa yuko tayari kuunda serikali ya muungano wa kitaifa na waasi hao na kuwa hatawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2016.


source: BBC swahili
 
Serikali ya Marekani, imesema imewaondoa raia wake katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kuingia mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema haijavunja uhusiano wake wa kibalozi na serikali ya nchi hiyo, ila imechukua tahadhari kuhusu usalama wa raia wake.
Marekani pia imeonya raia wake dhidi ya kwenda nchini CAR wakati wa machafuko hayo.
Hali ya wasi wasi imetanda katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Afrika ya kati, Bangui, huku waasi wanaopinga serikali wakikaribia kufika mji huo.
Mjumbe mmoja wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kuwa ameshuhudia raia wa mji huo wakiwa na wasi wasi mkubwa kutokana na na tishio la shambulio.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa umewahamisha wafanyakazi wake wote nchini humo, nayo serikali ya Marekani imetoa wito kwa raia wao kuondoka nchini humo.
Serikali ya Ufaransa kwa upande wake imeagiza usalama kuimarisha katika ubalozi wake mjini Bangui, baada ya kushambuliwa na waandamanaji.
Waandamanaji hao walirusha mare ya kuchoma bendera ya Ufaransa.
Raia hao wanataka serikali ya Ufaransa kusiadia kuzima uasi Kaskazini mwa nchi hiyo.
Wanadai serikali ya Ufaransa imewatekeleza.
Ufaransa ina takriban wanajeshi mia mbili mjini Banguia na utawala wa nchi hiyo umetoa wito kwa Ufaransa kuingilia kati na kusaidia kukabiliana na wanajeshi wa waasi ambao wameuteka maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo.
Lakini rais wa Ufaransa Francois Hollande amekataa wito huo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ameliambia shirika la Habari la Reuters kuwa mzozo huo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.


source: bbc
 
Muungano mpya wa waasi katika jamhuri ya Afrika ya kati ulianzisha mashambulizi yake upande wa kaskazini mwa nchini Desemba 10.
Kundi hilo la waasi lijulikanalo kama Seleka liliteka mji wa Kaga- Bandoro Jumanne. Waasi hao sasa wako kilometa 300 kutoka mji mkuu Bangui, ulio karibu na kusini mwa mpaka na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Seleka inaunganisha makundi manne ya waasi kutoka kaskazini. Wapiganaji wengi walihusishwa katika mzozo wa miaka minne ambao ulimalizika rasmi kwa mkataba wa amani wa mwaka 2007, licha ya kwamba mapigano yamekuwa yakirudia mara kwa mara upande wa kaskazini tangu mwaka 2009.
Kasi na urahisi ambao jeshi hilo la muungano wa waasi limeweza kuchukua miji muhimu kaskazini inaleta wasiwasi. Wachambuzi wanasema majeshi ya serikali yanatoa upinzani mdogo.
Chad, mshirika wa karibu wa rais Francoise Bozize wamepeleka majeshi kumlinda.
Mkurugenzi wa Afrika ya kati wa shirika la kimataifa la mizozo Thierry Vircoulon amesema jeshi la Chad ndio ngao ya serikali na si rahisi kwa waasi kupambana nao.
Anasema jeshi la Chad limepelekwa kimkakati kwenye maeneo ya mji mkuu ili kuulinda . Anasema waasi wanadhibiti kiasi cha robo tatu ya mji, hata hivyo lengo si kuchukua Bangui na kuiangusha serikali. Amesema waasi wamechukua miji muhimu ili kuonyesha nguvu zao na kujiweka kwenye nafasi nzuri katika meza ya mazungumzo.
Kutekwa kwa Kanga Bandoro Jumanne kumekuja siku moja tu baada ya waasi kukubali kusitisha kusonga mbele na kuanza mazungumzo. Serikali imesema haitafanya mazungumzo mpaka waasi hao waondoke kwenye miji waliyoiteka.
Viongozi wa kikanda sita walijiunga chini ya jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya kati wamesema lazima waasi waondoke na wametoa wito wa kufanya mazungumzo ya amani katika mji mkuu wa Gabon Libreville.
Seleka anasema serikali haikuheshimu mikataba ya amani ya mwaka 2007 na 2011 ikiwa ni pamoja na kipengele cha kuwalipa wapiganaji waasi na kuwaingiza kwenye jeshi la serikali.
Maelfu ya waasi wameripotiwa kukimbia mapigano ya hivi karibuni kaskazini ambapo usalama mdogo umekuwa tatizo linalokuwepo na kuondoka.
Msemaji wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu wa Jamhuri ya Afrika ya kati Vincent Pouget ameiambia VOA kwamba mapigano yamekata mawasiliano ya simu za mkononi kwenye eneo hilo.
Anasema ni ngumu kujua ni kiasi gani hasa raia waliokimbia na wapi walipo, jambo linalopelekea juhudi za uokozi kuwa ngumu zaidi . Amesema baadhi wanakimbia kwenye makazi ya muda mfupi karibu na viwanja hivyo, wakati wengine wanakimbilia maporini, vijiji vya karibu au kwenye maeneo yanayokubalika kama kwenye mishen za kanisa katoliki. Amesema kuwapatia maji safi ya kunywa na vyoo ni jambo muhimu kuzuia ugonjwa.
Doctors Without Borders wanasema wamepata ripoti za ghasia dhidi ya raia ikiwa ni pamoja na uporaji. MSF inasema wengi wa waliokimbia bado wanaogopa kurudi nyumbani
 
Back
Top Bottom