John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 112
- 217
Waandishi wa kitabu cha zaburi
Zaburi ni nini katika Biblia
Zaburi maana yake ni nyimbo takatifu. Hivyo kitabu cha Zaburi katika biblia, ni kitabu cha nyimbo takatifu. Zimeitwa nyimbo takatifu kwa sababu zimetungwa kwa lengo la kumrudisha mtu kwa muumba wake, kwa njia hiyo ya kusifu na kumwimbia. Pia, pamoja na kwamba zilikuwa ni nyimbo, lakini ndani yake pia zilikuwa zimejaa unabii wa mambo yanayokuja.
Katika agano la kale nyimbo hizo ziliimbwa na Wayahudi (Waisraeli) wakati wa kuabudu katika masinagogi yao. Hata leo, wakristo wanatumia baadhi ya mashairi hayo kutengeneza nyimbo nzuri za kumwimbia Mungu, kumshukuru na kumsifu.
Kitabu cha Zaburi katika biblia kwa sehemu kubwa (50%) kimeandikwa na Mfalme Daudi. Biblia inasema kuwa Daudi alianza kumwimbia Mungu tangu akiwa mdogo (1Samweli 16:16)
Kwa kifupi, kitabu cha Zaburi ni mkusanyiko wa maombi, mashairi na nyimbo ambazo zinalenga mawazo ya yule anayemuabudu Mungu, katika sifa na kuabudu. Sehemu za kitabu hiki zilitumika kama nyimbo katika ibada ya Israeli ya kale. Urithi wa kimuziki wa zaburi umeoneshwa na mada yake inatokana na neno la Kigiriki ambalo linamaanisha “wimbo unaoimbwa na vyombo vya kimuziki”.
Zaburi nyingi za kibinafsi zinahusisha sifa ya Mungu kwa ajili ya uwezo wake na wema wake, kwa ajili ya uumbaji wake wa ulimwengu, na kwa ajili ya matendo yake ya awali ya ukombozi kwa ajili ya Israeli. Wanawazia ulimwengu ambamo kila mtu na kila kitu kitamsifu Mungu, na Mungu naye atasikia maombi yao na kujibu.
Kitabu cha Zaburi kimegawanywa katika vitabu vitano.
Zaburi ya 1-2 ni za utangulizi
Zaburi imepangwa kama ifuatavyo:
Kitabu cha 1: 3-41
Kitabu cha 2: 42-72
Kitabu cha 3: 73-89
Kitabu cha 4: 90-106
Kitabu cha 5: 107-150
Tangu nyakati za kale, yasemekana kuwa kuhani Ezra ndiye aliyepanga kitabu cha Zaburi jinsi kilivyo leo.
Kitabu cha Zaburi kina jumla ya zaburi 150.
Kitabu hicho kimeandikwa na zaidi ya watu 7.
Waandishi wa kitabu cha Zaburi wameoneshwa hapo chini:
1. Mfalme Daudi: aliandika jumla ya zaburi 75 (50% ya zaburi zote 150)
Zaburi alizoandika Daudi ni zifuatazo:
2-9, 11-32, 34-41, 51-65, 68-70, 86, 95, 101, 103, 108-110, 122, 124, 131, 133, 138-145
2. Mfalme Sulemani: zaburi 2 (72 na127)
3. Nabii Musa: zaburi 1 (90)
4. Asafu: kiongozi wa sifa, muimbaji, muonaji, anayesimama mbele ya sanduku la Mungu daima kumsifu Mungu: zaburi 12 (50, 73-83)
5. Wana wa Kora: zaburi 11 (42, 44-49, 84-85, 87)
6. Hemani: mtu wa hekima: zaburi 1 (88)
7. Ethani: mtu wa hekima: zaburi 1 (89)
8. Wasiotambulika: jumla ya zaburi 48
Zaburi 48 ambazo waandishi wake hawajulikani ni kama ifuatavyo:
1, 10, 33, 43, 66-67, 71, 87, 91-94, 96-99, 100, 102, 104-107,
111-121, 123, 125-126, 128-130, 132, 134-137, 146-150
Utaona kuwa kuna zaburi 48 ambazo waandishi wake hawajulikani. Aidha, haijulikani wana wa Kora walioandika zaburi 11, walikuwa wangapi. Kama ingejulikana, kungekuwa na zaidi ya waandishi 7.
Ukiacha Sulemani na Musa, waandishi wengine wote walikuwa makuhani au Walawi ambao walihusika na kutoa muziki kwenye ibada madhabahuni wakati wa utawala wa Daudi.
Daudi aliyeandika zaburi 75 (50%) kati ya zaburi 150 ni nani
Daudi alikuwa ni Mfalme na mwanamuziki wa kipekee kwa kuwa alikuwa mwimbaji na pia mtungaji wa mashairi. Alipokuwa mvulana, alikuwa mchungaji na akili yake yenye utambuzi na ufahamu wa hali ya juu ilihifadhi habari nyingi kuhusu maeneo ya malisho ya Bethlehemu.
Alikuwa amefurahia kusikia sauti ya vibubujiko vya maji na sauti ya wana-kondoo wanapojibu anapowaita. Akivutiwa na umaridadi wa sauti hizo zilizomzunguka, alichukua filimbi na kinubi na kuanza kumsifu Mungu. Bila shaka ilipendeza kusikia muziki wa Daudi alipoimba Zaburi ya 23.
Kwa sababu ya utu wake mchangamfu, Daudi alipenda nyimbo zenye furaha zinazochangamsha na miziki yenye midundo yenye kupendeza.
Kwa ujumla, Daudi alikuwa msanii mwenye kipawa, kwa kuwa alikuwa mtengenezaji wa ala za muziki, mshairi, mtungaji, na mtumbuizaji. Daudi alifanya mambo makubwa hata zaidi.
Daudi hukumbukwa kwa kuwa yeye ndiye aliyepanga uimbaji na muziki katika nyumba ya Yehova. Alikuwa na waimbaji na wanamuziki 4,000, waliosimamiwa na Asafu, Hemani na Ethani.
Daudi aliwaweka chini ya wataalam mbalimbali 288 ambao waliwafunza na kuwaongoza. Wanamuziki na waimbaji hao 4,000 walikuwepo wakati wa sherehe tatu kubwa zilizofanywa kila mwaka. Hebu piga picha, kwaya hiyo kubwa yenye kuvutia (1Mambo ya Nyakati 23:5; 25:1, 6-7). Muziki wa Daudi ulioongozwa na roho takatifu, ulikuwa bora katika njia.
Jambo tunaloweza kujifunza ni kwamba Zaburi hizi zilizoandikwa na Daudi, zimewezwa kutukuzwa na Mungu mwenyewe mpaka leo, kwa sababu zimejaa maneno ya sifa kwa Mungu na ya kumtukuza sana.
Zaburi kwa ujumla
1. Zaburi ni aina ya sala iliyotungwa kama shairi au wimbo. Zaburi zinafundisha jinsi binadamu awezavyo kuzungumza na Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo kitabu cha Zaburi kinatumiwa na Wakristo kama kitabu cha sala (maombi).
2. Masomo kwenye zaburi hasa, ni sifa za Mungu, shukrani, maombolezo, huzuni na toba, furaha na imani, elimu ya kidini, na ombi la ushindi dhidi ya maadui wasiomcha Mungu.
3. Zaburi imeandikwa na watu 7. Hata hivyo, kuna zaburi 48 ambazo waandishi wake
hawajulikani. Hivyo, kama wangejulikana, kungekuwa na zaidi ya waandishi 7.