Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Kufuatia kifo cha kinyama cha aliyekuwa mwandishi wa habari wa channel ten mkoani Iringa hivi karibuni, waandishi wa habari kupitia Taasisi/vyama vyao kama Press Clubs, MCT na Jukwaa la wahariri walitoa matamko na misimamo mbalimbali.
Mojawapo ya mambo waliyofanya ni pamoja na Wanahabari wa Iringa kutangaza kususia kuandika/kutangaza habari za polisi kwa kipindi chote hadi siku arobaini za matanga ya marehemu Mwangosi.
Jambo la ajabu sana ni kwamba hata kabla ya siku kumi vyombo vya habari vimewasaliti wanahabari wenzao wa Iringa kwa kiasi cha kutisha. Vyombo vya habari vya Startv/RFA na ITV/Radio One vikaamua kupeleka waandishi wao Iringa wakaripoti kikamilifu habari za maadhimisho ya siku ya usalama barabarani kwakuwa wawakilishi wao walioko huko wasingeweza kufanya kinyume na msimamo wa IPC.
Kwa usaliti kama huu wanaofanyiana wanahabari wasitarajie kuheshimika ama kuaminika na jamii kama wao wenyewe hawajithamini na hawana umoja na mshikamano miongoni mwao. Walianza kusalitiana siku ya maandamano yao kwa kumwalika nchimbi pamoja na vituo vya Startv/RFA na ITV/Radio One kuongoza kwa kutangaza habari za kipolisi.