Waandishi wa habari walioambiwa na mch. Lusekelo watakufa mwezi March, je wameshakufa?

Testar

JF-Expert Member
May 30, 2015
7,613
12,895
Wakuu wa jukwaa amani kwenu!
Kama mtakumbuka siku za nyuma lilitokea tukio la kuripotiwa habari ya ulevi wa mch. Anthony Lusekelo. Iliripotiwa kuwa mchungaji Lusekelo alipata kileo kikali kabla ya kwenda kumpromoshea maneno makali jirani yake.
Aidha, wadukuzi walifika mbali zaidi na kuripoti kuwa mchungaji alipiga pombe aina ya Konyagi, jambo lililosababisha mchungaji abadilishane jina na pombe kwani siku hizi konyagi bapa inaitwa Lusekelo.
Tukio hilo lilimkasirisha sana Mch. Lusekelo kwani aliapiza kuwa waandishi waliomwandika vibaya watakufa 'kabla' ya mwezi march mwaka huu.
Sasa nauliza je wale waandishi walishafariki?

Kati yenu kuna aliyehudhuria maziko ya mwandishi wa habari ndani ya miezi miwili iliyopita?

Kama hawajafa, je ina maana mch. Lusekelo hana maono na hawezi kuona mambo yanayokuja?

Hii ina ashiria nini kwenye uhalali wa uchungaji wa Lusekelo?
 
Anajivika uungu sio, apeleke huko ujenzi huru wake!! Yaani amfanyie maombi afe!! Ile ...... ya mfalme Suleiman haipo Ku kichwa chake. Labda alikuwa anatabiri kifo cha viroba sokoni.
 
atakuwa mchungaji wa kondoo wa kufugwa,, yaani ukifuatilia waumini wake wanaotoa ushuhuda wa mali walizopata kupitia mzee wa upako... utavunjika mbavu. dah, eti mtu kajenga gorofa, anamiliki bus 5, nyumba, na mali kedekede baada ya kuingia kwenye kanisa la mzee wa upako, na hapo hana hata mwaka>>>> sasa unajiuliza huyu anafanya upako wa Mungu au Miujiza gani kama siyo usanii. Utakuata waumini wamejaaaaa teleeee, wanashangilia ushuhuda
 
Back
Top Bottom