Tuelimishanee
Member
- May 23, 2018
- 20
- 18
Na Mwandishi wetu, Dar
Kampuni inayozalisha taulo za kike ya Human Cherish (HQ), Desemba 8, 2021 ilifanya Mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutangaza uboreshaji wa huduma za kampuni hiyo,Sambamba na kugawa bidhaa hizo kwa waandishi waliokuepo katika Mkutano huo.
Katika hali ya kushangaza taulo hizo ziligundulikana kuwa zimeshakwisha muda wake wa matumizi(exp).
Baada ya kutokea kwa Sintofaham hiyo baadhi ya waandishi walifanya jitihada za kutafuta Uongozi wa Kampuni hiyo ili kuweza kuzungumza nao juu ya tukio hilo lakini hawakufanikiwa kuwapata.
Chanzo cha taarifa hizi kilielezea kuwa, walishangazwa na tukio hilo huku wakigubikwa na maswali mengi kichwani yaliokosa majibu .
"Ilinza kama masihara Mwandishi mmoja alituma picha kwenye group akielezea kuwa taulo alizopata yeye zimekwisha muda wa matumizi, na kututaka tukague na za kwetu Ili kuangalia usalama wa bidhaa hizo lakini majibu yalikuja sawa kuwa zote zimemaliza muda"kilielezea chanzo hicho.
Kiliendelea kusema kuwa, ni jambo la aibu mno kufanya tukio hilo kwa waandishi wa habari, huku akihoji ni box ngapi zimepelekwa mashuleni kwa ajili ya wanafunzi, na je zipo salama kweli....wangapi wametumia na nini kitatokea kwa watu ambao wameshatumia.
"Tunaziomba mamlaka husika kufatilia kampuni hii juu ya bidhaa zinazozalishwa kwani hatuna tena Imani nazo, sijui wamekusudia nini, au watasema walikua hawajui kua zimekwisha muda wa matumizi"kilihoji chanzo hizo.