Waandishi wa habari mna"bore" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi wa habari mna"bore"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lole Gwakisa, Apr 21, 2011.

 1. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kuna waandishi wazuri lakini walio wengi wanaboa sana.Hebu soma taarifa ya wizi wa fedha za TRA zinazomhusu mfanyabiashara mmoja jijini Dar.

  Gazeti la Majira:Kortini kwa wizi wa bil.3.8/- za TRA,
  Gazeti la Daily News:Businessman arraigned for 2bn/- money laundering,
  Guardian: Dar businessman in court over 3bn/- theft,
  Nipashe:Kizimbani kwa tuhuma ya kuiibia TRA Sh. bilioni 3.,

  Mtuhumiwa katika sakata hili wengine wamemuandika kama Erick Talemwa, wengine Erick Lugeleka!
  Kwa hakika kama hawa waandishi waote walikuwepo kwenye kesi hii basi waandishi wetu wanamatatizo makubwa.
  Rais mstaafu Mkapa(alikuwa mwandishi aliyebobea) yupo kwenye rekodi kwa kukataa kuongea na waaandishi wa kiTanzania na hii inaweza kuwa sababu tosha kabisa.
   
 2. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi nami naona nishapata ulemavu!!

  kila nikisoma habari, siwezi kuichukulia kama yote ni ukweli, najua lazima imechakachuliwa tu!!!

  sijajua wanafanya hivyo kuuza magazeti, au elimu ya yao, hata sielewi!!!!!!!!!!
   
 3. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  hata mm cwez kuridhika kusoma gazet moja kwan ninajua kutakuwa na matatzo kama hayo hvyo nimezoea kusoma magazet matatu au manne ndo angalau unajua nn kinachoongelewa mana hawa cjui wakat wanaandika wanakuwa wanawaza familia zao au wanasinzia
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kosa hapo sio la waandishi bali kosa la la WAHARIRI hawafanyi homework zao vizuri.

  Wengi ni wavivu sana wanaachia vishoka wawape habari na wao wanaziweka gazetini bila kuzifanyia uhakiki na kuzichunguza.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Lole Gwakisa, nimefarijika ulipoanza na uwepo wa waandishi wazuri, ni kweli fani ya habari imevamiwa na waganga njaa na wachumia tumbo kibao, lakini pia kuna wacheche wazuri, na inapotokea sababu , pia tuwa tunawatambua wachache hawa wazuri, ili watumike kama chachu ya kuwatengenezi wengine wengi kuwa wazuri.

  Hili la Mkapa na waandishi wa nyumbani kulikuwa na tatizo hapo. Mkapa ni mtu ambeye alikuwa na hasira sana, he couldn't stand criticisim za aina yoyote no matter matter how genuine ndio maana hata vipindi kama 'Kiti Moto' enzi zile, ilibidi kiuliwe kise Mzee hapendi!.

  Pia media team ya rais Mkapa pia was an insult on topo ofv injury kwa kuwa waoga kupindukia. Nikiwa mwandishi wa kujitegemea, mara kadhaa niliomba kufanya interview na rais Mkapa, mara zote nilikataliwa.

  Nikatokea kuwa nje ya nchi, nikakutana na Rais Mkapa nchi tatu tofauti, mara zote akizungumza na waandishi wa nje freely. Wakati mmoja alikwenda kuhudhuria UN GA pale New York, tukakuta UN imewapangia schedule marais wote kufanya press conferences, na kutoa nafasi kwa waandishi wowote, kufanya booking ya kufanya interviews na marais wowote. Press Sec wa wakati huo akaniambia, "haya sasa wewe si kila siku ulikuwa unaomba nafasi ya kufanya interview na rais, haya sasa nafasi ndio hii, itumie"!. Kusema kweli nilikataa, nikamwamia lengo la interview yangu ni kufanyia nyumbani, yaani mimi mwandishi Mtanzania kufanya interview na rais wangu ndio nije niifanyie New York? . Nikamwambia kama kweli uko genuine, naomba tuandalie fursa kama hizi sisi waandishi wa nyumba na mahojiano yaje yafanyikie nyumbani., a thing that never happened!.

  Kwa dharau zake za waandishi wa nyumbani na kutukuza wale wa nje, Tim Sebastian aliwahi kumuumbua Mkapa kwenye BBC-Hard Talk, nilipokiona kipindi kile, nikajifikiria ndio mimi ningempata kwenye Kiti Moto, bara baada ya mahojiano, ningeishia Segerea.

  Kuna waandishi wengi tuu Tanzania ambao wamejikuta they had to make a choice kati ya kutumikia fani ya habari, au kujenga familia. Ulifika wakati unaangalia umuhimu nambari moja upeleke wapi kwenye setting priorities, kama ni utaifa kwanza, unatumia kalamu yako kwa kuweka maslahi ya taifa mbele no matter what happens to you, na matokeo ndio kuwapata watu kama kina Stan Katabalo ambapo no body knows familia yake ina hali gani baada ya kujitoa mhanga. Sisi wengine, tulijiwekea familia kwanza na kujikalia pembeni.

  JK alipoanza, alianza vizuri kwa kuwaita waandishi Ikulu na kuruhusu maswali freely, baadaye wakaanza censoring ya kuchagua waandishi na maswali yatakayo uliza, hatimaye zile hotuba za rais za kila mwisho wa mwezi, sasa zimegeuka vile vile kama za Mkapa, ni mahubiri tuu, yaani rais ana preach kila mwisho wa mwezi. Papa Don't Preach!.

  Siku hizi ukiona maswali ya papo kwa papo na rais, basi ujue ni kwenye mkutano wa kimataifa, ama kuna ugeni wa kitaifa, tena maswali yenyewe, lazima yahusu mada husika!.
   
 6. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kabisa mkuu, hata magaeti yenye heshima kama Daily News na Guardian wanafanya makosa ya ajabu kabisa.
  Kwa hili la kesi hii sijui nani ndio ana habari za kweli kati ya haya magezeti mengi yaliyo andika habari ileile.
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nakufagilia mkuu Pasco, uandishi sasa hivi kwa kuendekeza tumbo unakosa standards kabisa.
  Wakuu wa nchi najua wana wakwepa sana waandishi wa habari ili wasipate maswali ya pao kwa papo, lakini Waziri Mkuu Pinda amewakosha watu wengi kwa kujibu maswali ya pao kwa papo Bungeni na vile vile hukutana na wahariri wa vyombo vya habari kwa mara kadhaa sasa.
  Mimi hatahivyo kinachonikera ni hasa habari andishi za magazeti ambazo hazina viwango wala uelewa unaokidhi soko.
  Sijui kosa ni wahariri au vyuo wanakopata mafunzo hawa waandishi wenyewe.
  Ukisoma gazeti la Esat African na ukilinganisha nahata Guardian na Daily News, uandishi wake ni tofauti kati ya mbingu na nchi.
  Shame!
   
Loading...