Waandishi wa habari (magazeti) mbadilike

Ntambaswala

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
255
78
Hivi sasa nchini kuna zaidi ya magazeti kumi yanatoka kila siku. Lakini ukinunua moja tu utakuwa umesoma magazeti yote kwa habari ya front page. Ni jambo la kushangaza sana inakuwaje magazeti kufanana habari wakati fulani hadi picha. Kuna sababu mbili tu huo upuuzi:
  1. Magazeti kuwa na chanzo kimoja cha habari.....hamujiongezi mnasubiri press release, semina, matukio, matamko ya viongozi, mahakamani etc
  2. Nimeshuhudia matukio mengi sana hasa ambayo lugha ya mawasiliano huwa ni lugha ya kiingereza, waandishi huwa wengi sana lakini huwa hawafanyi coverage kabisa wanakuwa bize na simu. Baada ya tukio humfuata mtu ''mswahili'' miongoni wa wale waendesha tukio wanamhoji basi habari imekamilika. Au kati ya hao waandishi anakuwepo ambaye lugha hupanda baada ya tukio kukamilika humzunguma yeye ndo anawapa kila kitu baadaye kila mwandishi huenda kujiongeza kidogo na kuandika habari yake
Kutokana na mabadiliko ya uendeshaji mambo wa serikali hii nashauri waandishi pia wabadilike. Viongozi wengine hutafuta kiki kwa matamko ambayo hayana utekelezaji zaidi ya kutaka kuonekana kwenye media.

Kuanzia sasa waandishi wasiripoti habari yoyote ambayo kiongozi anasema ''NITA'' tunataka habari ambayo kiongozi anasema 'NIME"...hiyo NITA ibaki kwa Mhe. Rais maana yeye akisema NITA hufanya kweli.
 
Back
Top Bottom