Waandishi kuweni Makini na Lugha ... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandishi kuweni Makini na Lugha ...

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by PascalFlx, May 13, 2009.

 1. P

  PascalFlx Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vyombo vya habari ni njia moja nzuri sana ya kuboresha lugha na njia mojawapo hatari sana ya kuharibu lugha tena kwa kasi sana..., Leo katika pitia pitia magazeti ya nyumbani katika mojawapo ya gazeti linalonivutia kwa habari zake 'mwananchi' wakati nasoma habari yenye kichwa cha habari "Polisi aliyepigwa na majambazi atolewa hospitali na risasi mwilini" ya tarehe 12/05/2009 tovuti "http://mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=11906" kusema kweli sikuridhika na uandishi ufuatao

  "Katika mapambano hayo, majambazi wawili walipoteza maisha, na wengine wawili, akiwemo askari huyo na raia mmoja, walijeruhiwa."

  Sijui kama ntakuwa nimekosea mimi au vipi ila kwa sentensi hiyo unaposema majambazi wawili ....., na wengine wawili ...., kwa ueleo wangu wa kiswahili nadhani hapo bado tunaongelea majambazi hivyo nadhani hapa neno wengine sio mahala pake kwa fikra zangu sentensi hii ilibidi iandikwe vingine ili kutofautisha vitu vitatu mosi waliofariki, pili waliojeruhiwa na tatu majambazi,raia na askari.Kwani ikibaki hivyo ilivyo inaonekana kana-kwamba huyo askari alikuwa ni mmojawapo wa majambazi hayo.

  wakadau kama kuna mchango wowote toeni ili turekebishane lugha yetu bado inakuwa kurekebishana ni muhimu (maana labda mimi nimesoma vibaya).
   
 2. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kuna wakati waandishi wengi hukosea sana katika utumizi wa lugha na upatanisho wa kisarufi na hali hii imekuwa ikijitokeza siku hadi siku mpaka unaweza kujiuliza je? Wahariri waliopo katika vyombo hivyo hufanya kazi ipi? Au nao wanaathirika na misemo jamii, japo ni lazima sote kwa pamoja tuhamasishane katika uandishi wenye mashiko ya lugha yetu ya kiswahili sanifu na sio kuandika kwa mitazamo yetu binafsi, hii itasaidia kuipa hadhi lugha
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Koma nne?
  "Katika mapambano hayo, majambazi wawili walipoteza maisha, na watu wengine wawili akiwemo askari na raia mmoja kujeruhiwa."
  Nimeamua kufanya zoezi maana koma zinanipiga chenga washkaji. Bado inahitaji marekebisho? :)


  pascalflx,
  "Waandishi kuweni Makini na Lugha ..."
  Ni sahihi?

  Jinsi tunavyosikia au kusoma kwa wengine, ndivyo nasi tutakavyozoea kuandika. Waandishi wanatakiwa kuonesha mfano.
   
Loading...