Waandishi 600 wafa kwa Covid-19

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,792
Geneva, Switzerland (AFP). Zaidi ya waandishi wa habari 600 wamekufa kwa ugonjwa wa corona tangu Machi 1, mwaka jana, taasisi ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari imesema ikitoa wito kwa kada hiyo kupewa kipaumbele katika chanjo.

Taasisi hiyo, Press Emblem Campaign (PEC), ambayo hufuatilia vifo vya wanahabari duniani, imesema kati ya waandishi 602 waliokufa kwa corona, zaidi ya nusu ni kutoka America Kusini, ambako wamekufa 303.

Vifo 145 vya waandishi vimetokea Bara la asia, 94 Ulaya, 32 Amerika Kaskazini na 28 Afrika.

PEC imesema haikuwa rahisi kuwatambua waandishi walioambukizwa wakiwa kazini, na kuwa orodha hiyo inahusisha pia waandishi waliostaafu.

Taasisi hiyo yenye makao yake makuu Geneva, Uswisi, imesema kundi la waandishi linapaswa kupewa kipaumbele katika chanjo.

“Kwa sababu ya taaluma yao, waandishi wanaokwenda maeneo ya kazi wanathibitisha kuthibitisha kuwa ni kundi lililoko hatarini. Baadhi yao, hasa wale wa kujitegemea na wapigapicha, hawawezi kufanyia kazi nyumbani,” amesema Katibu mkuu wa PEC, Blaise Lempen katika taarifa.

Orodha ya PEC imejumuisha taarifa zilizopatikana katika vyombo vya habari katika mataifa husika, taarifa za taasisi za wanahabari na maofisa wake walioko katika kanda mbalimbali.

Alisema orodha kamili inaweza kuwa kubwa zaidi ya 602 kwa kuwa sababu za vifo vya wanahabari wakati mwingine hazitajwi, vifo vyao havitangazwi au hakuna taarifa za kuaminika kutoka katika maeneo yao.

Peru inakabiliwa na vifo vingi zaidi ikiwa na wanahabari 93 waliokufa kwa corona, ikifuatiwa na Brazil (55), India (53), Mexico (45), Ecuador (42), Bangladesh (41), Italia (37) na Marekani (31)

PEC, taasisi iliyoanzishwa mwaka 2004, hutoa msaada wa kifedha kwa familia za wanahabari ambao wamekufa kwa Covid-19.
 
Nawakumbuka Marin Hassan Marin, Elisha Elia na Godfrey Dilunga, Mungu awarehemu.
 
Back
Top Bottom