Waandamanaji wakaa tayari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waandamanaji wakaa tayari

Discussion in 'International Forum' started by kilimasera, Feb 27, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Waandamanaji wakaa tayari

  Watu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli wanajiandaa kwa mapambano zaidi, baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi kusema atafungua maghala ya silaha kwa ajili ya wanaomuunga mkono.


  Kanali Gaddafi

  Uondoaji wa maelfu ya wafanyakazi wa kigeni unaendelea kwa njia ya anga, bahari na barabara, lakini wengine bado wamekwama.

  Marekani imezuia matumizi yoyote ya fedha na amana za Kanali Gaddafi na baadhi ya watu wake wa karibu.

  Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa katika mzozo wa kisiasa wa siku 10.

  Siku ya Ijumaa, waandamanaji wanaopinga serikali mjini Tripoli wameshambuliwa kwa nguvu na bunduki.

  Shirika la habari la AP limesema, limeelezwa kuwa serikali ya Kanali Gaddafi inawapa silaha raia wanaoiunga mkono ili kuweka vizuizi mjini Tripoli na kuwabana waandamanaji.

  Wakazi ambao wamezungumza na AP kwa njia ya simu siku ya Jumamosi, wameripoti kuwa magari ya raia wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi yanafanya doria mitaani.

  BBC Swahili - Habari - Waandamanaji wakaa tayari
   
 2. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  It looks like this is going to be the bloodiest uprising ever... :hatari:
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hata Mubaraka alikuwa na mkwara mkubwa sana tu lakini siku zilifika na akaondoka vizuri tu
  kwa sasa atakachokuwa anakifanya jamaa ni booking of asylum somewhere in Zimbabwe
   
Loading...