Waamuzi Singida wampinga Ndolanga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waamuzi Singida wampinga Ndolanga

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Jan 4, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CHAMA cha waamuzi (FRAT) Mkoa wa Singida kimesema hakikubaliani na maamuzi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya FRAT Taifa, Muhidini Ndolanga, kufuta matokeo ya chaguzi zote zilizofanyika nchini kwa madai kwamba marekebisho ya katiba hayajafanyika.
  Kauli hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti wa FRAT Mkoa wa Singida, Josephat Magazi, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika mjini Singida, na kusema haridhishwi na tamko la Ndolanga.

  Alisema Magazi kuwa tamko hilo linapingana kabisa na maamuzi ya kikao kilichopitisha katiba ya chama hicho, kilichofanyika mkoani Dodoma na kukubaliana kwamba mikoa iendelee kuzifanyia marekebisho ya katiba zao.

  Hata hivyo Magazi hakusita kuhoji kifungu kilichotumika kufuta chaguzi hizo ambacho kwa namna moja au nyingine kitakuwa kimepingana na maamuzi hayo ya mkoani Dodoma.

  “Tulipokuwa kwenye mkutano mjini Dodoma tulikubaliana kwamba chaguzi ziendelee na marekebisho yafanyike taratibu kwa kila Mkoa,” alisisitiza Magazi.

  ‘Sasa ni kifungu kipi kilichotengua maamuzi hayo mazito tuliyokubaliana kwenye mkutano huo wa Dodoma?” alihoji Magazi kwa masikitiko makubwa.

  Hata hivyo Magazi hakusita kuweka wazi kuwa hawakutegemea kupokea taarifa kama hiyo kupitia kwa Ndolanga na badala yake kauli hiyo ilitarajiwa kupokelewa kutoka TFF.

  Aidha mwenyekiti huyo wa waamuzi alitanabaisha kuwa mpaka sasa anachoamini binafsi ni kwamba uchaguzi waliofanya Mkoa wa Singida ni halali na kwamba iwapo utakuwa umefutwa wanasubiri taarifa kamili kuhusu kufutwa kwa matokeo hayo.

  Katika mkutano huo wa uchaguzi, Josephat Magazi alichaguliwa tena kuendelea kuwa mwenyekiti na Haruna Kabombwe ni katibu mkuu wa chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

  Katika uchaguzi huo uliosimamiwa na mwalimu mstaafu Mtua akishirikiana na James Kitila aliyechaguliwa kushika nafasi ya mweka hazina wa chama hicho ni Issa Saidi huku mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa, Anorld Bugado.

  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Mkoa ni Richard Nganya na kuongeza kwamba kuna nafasi nne ambazo hazikujazwa kutokana na kutokuwa na wagombea.

  Nafazi hizo ni pamoja na Makamu mwenyekiti, Katibu msaidizi, mjumbe mmoja wa Kamati ya Utendaji mkoa na mjumbe mmoja wa waamuzi wanawake.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,599
  Trophy Points: 280
  Kwani hakuna wanamichezo wengine????lazima Ndolanga tuuu....miaka yoote!!
   
Loading...