Waaminio katika ushirikina ni tatizo kuliko ushirikina wenyewe

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Oct 31, 2017
7,621
16,373
Imani kuhusu uwepo ushirikina/uchawi imekuwepo kwa kipindi kirefu mno japo hakuna uthibitisho usio na shaka juu ya uwepo wake isipokuwa hadithi za hapa na pale zinazojaribu kueleza kuwa ushirikina upo. Binafsi siwezi kuthibitisha kuwa ushirikina upo japo kuna mazingira niliyoyaona ambayo yanahusishwa na ushirikina au uchawi. Kiufupi ushirikina unabaki kama imani zingine tu kuwa iko hivi iko vile.

Ushirikina uwepo au usiwepo si kitu, ila imani za watu juu ya ushirikina ni tatizo kubwa kuliko ushirikina wenyewe (kama kweli upo). Hii imani inaendekezwa sana kukweli, inafanya mambo yaonekane mabaya kuliko hata uhalisia. Imani hii inasababisha watu wakose uwezo wa kufikiria namna nora ya kushughulika na matatizo yao na kuwaza kuwa kuna njia ya mkato kupitia ushirikina.

Mtu akipata changamoto ya kiuchumi anafikiri kuwa amerogwa, anaenda kwa mganga. Hivi ni lini maisha yameshawahi kuwa marahisi na yasiyo na changamoto? Unadhani mganga atakwambia katumie panado ili duka lako liuzel?!! Lazima utaambiwa fulani ni mbaya wako; kafanya hivi kafanye vile, kamfanye hivi kamfanye vile. Baada ya hapo unazalisha chuki, unaanza kuwazia watu mabaya pasi na sababu za msingi. Kama mtu huyu asingeupa kipaumbele ushirikina asingeenda huko na hayo yote yasingetokea.

Watu wanaomini ushirikina kupita kiasi ndo hao hao ambao hata likitokea jambo la kawaida ambalo linaweza kutokea mahala popote pale utaona wanakuja mbio kutaka kutuaminisha kuwa linatokana na ushirikina. Ni ujinga tu. Hii ni dunia, na lolote linaweza kutokea mahala popote kwa kuwa kila kitu hakiko tuli. Hakika nasema uchawi au ushirikina hauna ,matokeo yoyote halisia, bali ni vile tu watu wameshafungwa huko.

Waaminio ushirikina wamekuwa mtaji mkubwa wa waganga uchwara ambao wamekuwa wakila pesa zao na zaidi kusababisha chuki na mambo mengine ya hovyo kwenye jamii.

Waaminio ushirikina wamekuwa mtaji mkubwa wa manabii uchwara ambao wamekuwa wakiwatumia kwa maslahi yao binafsi.

Ni kweli kuna wakati tunapitia wakati mgumu kiasi unawaza kama hili jambo limetokea kwa hali ya kawaida au kuna kitu cha ziada, lakini tusikimbilie kwenye ushirikina. Hakuna suluhisho la kudumu huko zaidi ya kujiongezea matatizo wewe mwenyewe na wengine wanaokuzunguka.

Hatuna shida na imani ya mtu, ila imani inapoleta mgawanyiko na machafuko katika jamii hakuna namna inapaswa kuvulika. Watu wanatekwa na maluweluwe, mtu timamu kabisa anashadadia maluweluwe na kuipotosha na kuiharibu jamii yake mwenyewe, ujinga.
 
witchcraft: means all negative thought coming inside of your mind.(shetani wa mtu ni mtu mwenyewe) na
huo ndiyo uchawi wenyewe .
 
Kwa hiyo mkuu unamaanisha sisi tuliozaliwa miaka ya 2000 hatupaswi kabisa kuzungumxia haya mambo?

Ndiyo sbb dunia hujaimaliza, ngoja nikupe mfano Kuna mtu alikuwa hakimu alipoenda open court kuhukum Ile anamaliza kesi kusimama kakukata suruali yoote imeliwa na mchwa.
Kule masasi walimu waliochapa watoto walijikuta nje kwenye uwanja wa shule asbh
 
Uchawi upo ila hupaswi kuuamini kuliko kiasi. Demu wangu kapima mara nne huko nyuma kaambiwa anangoma harafu kapima tena mara nne mfurulizo kwa mwaka huu tu kaambiwa yuko negative. Ananambia eti kuna mchawi anamchezea akili mi namchora tu. Nimemwambia labda ajiunge jf akutane na nadharia za deception.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi upo ila hupaswi kuuamini kuliko kiasi. Demu wangu kapima mara nne huko nyuma kaambiwa anangoma harafu kapima tena mara nne mfurulizo kwa mwaka huu tu kaambiwa yuko negative. Ananambia eti kuna mchawi anamchezea akili mi namchora tu. Nimemwambia labda ajiunge jf akutane na nadharia za deception.

Sent using Jamii Forums mobile app

Demu ndio nini?
 
Shida sio KUAMINI shida ni uelewa kwenye huko KUAMINI
Bila kuwa well informed IMANI hugeuka kuwa mzigo mzito kwenye lolote kuanzia mahusiano mpaka kwenye mambo ya kiroho

Jr
mambo vipi Mshana jr? out of topic, naomba unipe elimu juu ya subliminal messages kama una ufahamu nazo pls.
 
Back
Top Bottom