Waajiriwa wa Serikali nijuzeni hapa kuhusu vigezo vya kupata maternity leave

NOKIALUMIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
396
277
Hivi ni kweli kupata maternity leave ni lazima mtu awe kamaliza miaka mitatu kazini?

Sheria zinasemaje?

Maaana wife ameenda kuomba ruhusa kanyimwa na ana two years kwenye utumishi wa umma, kambiwa hastaili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni kweli kupata maternity leave ni lazima mtu awe kamaliza miaka mitatu kazini???

Sheria zinasemaje ..

Maaana wife ameenda kuomba ruhusa kanyimwa na ana two years kwenye utumishi wa umma , kaaambiwa hastaili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Katika Mzunguko wa Likizo (kipindi cha miezi 36) utastahiki siku 84 za Likizo unayolipwa ya Uzazi ikiwa utajifungua mtoto mmoja au siku 100 za Likizo unayolipwa ya Uzazi ikiwa utajifungua zaidi ya mtoto mmoja.

Siku hizi zinajumuisha siku za mapumziko na Sikukuu za Umma. Hata hivyo kwa sababu ya matatizo yoyote yale ya kujifungua/kuzaa uwe unahitaji siku za ziada unaweza kujadiliana na mwajiri kuhusu uwezekano wa kutumia siku za Likizo ya Ugonjwa, au siku kadhaa kutoka kwa Likizo yako ya Kila Mwaka, au upate siku za ziada za likizo usiyolipwa.
 
Kafanyiwa umafia tu. Hata akiwa na miezi 4 huweza kupewa hii likizo. HR au boss wake wana bifu au nguvu kazi hakuna kazini kwao
 
Ata kama hajatmza mengne ni busara
Huyo tena ametumikia miaka 2 so nazn kuna shida tuu hapo
Jarbu kuwasiklza na kuwaomba hyo lkzo
NB:- jarb kujua mahusiano ya mkeo na ofisi pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni kweli kupata maternity leave ni lazima mtu awe kamaliza miaka mitatu kazini?

Sheria zinasemaje?

Maaana wife ameenda kuomba ruhusa kanyimwa na ana two years kwenye utumishi wa umma, kambiwa hastaili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtumishi anapoajiriwa kwa Mara ya kwanza,,,anaruhusiwa kupata ujauzito baada ya kufikisha mwaka mmoja kazini,,,,yaani kuthibitishwa,,,rejea kanuni za kudumu h.12 (6) za mwaka 2019.

Hivyo hapo mke wako hakutendewa haki,,,anatakiwa angeruhusiwa kupata likizo ya uzazi,,,na baada ya hapo anatakiwa kuzaa kila baada ya miaka 3.

Standing order inamarekebisho ya 2019?

Mi najua ni kweli hana haki mpaka afanye kazi miaka 3. Huwa busara tu inatumika.

HR wake ana roho mbaya tu.
 
Standing order inamarekebisho ya 2019?

Mi najua ni kweli hana haki mpaka afanye kazi miaka 3. Huwa busara tu inatumika.

HR wake ana roho mbaya tu.
Ungetaja ni Kanuni ipi inayoelezea haya unayoyasema katika hiyo standing orders.

Miaka 3 inayozungumzwa kwenye standing orders ni baina ya mimba moja hadi nyingine.

Mfano, mtumishi kaajiriwa mwaka 2019, then mwaka 2020 akapata mimba, anastahili maternity leave. Baada ya hapo hastahili tena likizo hii mpaka ipite miaka 3.

Yaani kutoka likizo moja ya uzazi hadi nyingine, ni lazima mtumishi akae miaka 3. Nadhani walikua wanahimiza watumishi wazae kwa mpango. Watoto wapishane walau miaka 3.
 
Hivi ni kweli kupata maternity leave ni lazima mtu awe kamaliza miaka mitatu kazini?

Sheria zinasemaje?

Maaana wife ameenda kuomba ruhusa kanyimwa na ana two years kwenye utumishi wa umma, kambiwa hastaili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipi walimpa hiyo likizo au ndo amenyimwa??

Huyo afisa utumishi wake ni kilaza na hazijui Sheria na Kanuni za utumishi wa Umma.

Mkeo anayo haki ya kupewa likizo ya uzazi as long as ameshafanya kazi zaidi ya miezi 12 na tayari ameshathibitishwa kazini.

Miaka 3 inayozungumzwa kwenye Kanuni ni muda wa kukaa baina ya likizo moja ya uzazi hadi nyingine. Ukishapewa likizo ya uzazi, huwezi pewa tena mpaka ipite miaka 3.

Muhusika akamwambie HR wake asome Kanuni ya 98(1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 aisome kwa pamoja na Kanuni H.12(2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma toleo la Mwaka 2009.

Kuna baadhi ya HR Officers wanadhulumu haki za watumishi kwa kushindwa kutafsiri sheria na kanuni.
 
Back
Top Bottom