Waajiri na Makampuni Binafsi, toeni Maoni yenu vyuo vipi vinapika wataalam vizuri

Wewe ni HR tu,huwezi jua mambo ya kwenye field ya kozi nyingine,ndiyo maana kwenye interview,Mara nyingi Head of Department au Manager ndiyo hua wanauliza maswali ya field yao,technical questions, na ndiyo mwenye uamuzi wakupendekeza nani achukuliwe! HR unajua IAS number 1 hadi 40 huko zinasemaje?? HR ni intro na kwenye benefit tu!!
Tusipende kua wajuaji wa kila jambo!!
Utakuwa wa CBE wewe. Ingia www.vabusiness.co.tz ndiyo mimi
 
Garbage in, garbage out.. Nilikuwa na debate na jamaa mmoja anasema, shule za Goba zinafaulisha sana.. Nikamwabia, asilimia kubwa ya wakazi wa Goba ni graduates.. So most likely watoto wao wakawa na uwezo mkubwa genetically uki compare na watoto waliozaliwa na wazazi wa Buza.. So even though shule za Buza zinafundisha vizuri ila kwa kuwa wanafunzi hawako genetically brilliant, huzifanya shule kuonekana kuwa hazifundishi vizuri, which may not be true!
 
Ni muda muafaka kwa Waajiri na Makampuni binafsi kutoa mrejesho kwa Wanafunzi wa Vyuo gani Wanafanya Vizuri katika Maeneo yao ya kazi. Pia tunaomba watoe mrejesho ni maeneo gani ambayo yana upungufu mkubwa wa Wataalam wa Fani husika.

Nikimaanisha kuna Position inabidi Human Resource Officers kutumia muda mwingi kurudia kutangaza Ajira ya nafasi husika kwa kukosa Watu wenye sifa sahihi (Job employment Re-advertisement)

Nchi za wenzetu feedback kama hizi huvisaidia Vyuo ku-restructure baadhi ya Course zao ili kuendana na matakwa ya Soko la ajira.
Toa Maoni yako chuo bora kwa Kupika Wanatahiniwa katika Fani zifuatazo:

1. Usafirishaji (Anga na nchi Kavu)
2. Biashara
3. Fedha, Benki na Bima
4. Uhandisi (Civil, Chemical, Electrical, Machenical. etc)
5. Afya (Udaktari, Uuguzi, Maabara)
6. Utawala (Public Admistration, Human Resources)
7. Mawasiliano (ICT & Telecom)
8. Kilimo na Mifugo ( Veterinary Medicine, Animal Health, Food science, Agriculture)
8. Madini (Geology)
9. Utawala katika Afya (Public Health)
10. Mipango
11. Usafiri (Maji)
12. Uandishi wa Habari na Mahusiano
13. Ualimu (Sanaa)
14. Sayansi ya Siasa
15. Ualimu (Sayansi)
16. Sheria
17. Social Work
18. Uchumi
Hakuna hata kimoja vyote hovyo
 
Sijui kama nakosea, ila nadhani UDSM bado ni chaguo namba 1 namba moja la wahitimu wengi wa kidato cha sita kwa fani zote. Hivyo watu wengi waliofanya vizuri mitihani ya kidato cha sita wanaenda udsm. Hii ndo kusema udsm ina chukua cream. Na graduate wengi wa udsm wanafanya vizuri sana wakiingia kazini. Inawezekana siyo kwa sababu udsm wanafundisha vizuri ila ni kwa sababu wanafunzi wenyewe ni wazuri.

Pili, iko hivi. Shuleni au chuoni tunaenda kupata general knowledge kuhusiana na fani fulani. Utakacho kuja kufanyia kazi ni sehemu ndogo sana, ya vile ulivyojifunza. So nategemea graduate anapopata kazi..ajifunze/afundishwe kazi.

Tatizo kubwa ni mentality ya watu wetu. Hawapendi kusoma, hawapendi kujifunza. Wanadhani wakimaliza shule ndo wamemaliza kusoma. Kumbe kusoma hakuna mwisho. Unapoanza kazi ndo inabidi usome sana ili kuboresha kazi yako.

So mimi napenda kuajiri watu ambao wanapenda kusoma. Ndo maana si ajiri direct. Intern miezi 6 ndo ajira inafuata kama utakuwa vizuri.
Unamaanisha wanaofanya vibaya ndo wanaenda vyuo vingine, acha kuongea mamb Bila utafiti,
 
Mwalimu wa chuo kikuu hajawahi kufanya kazi ana claim notisi kama wewe miaka Nenda miaka rudi

Nenda vyuo vingi vya ulaya mambo makubwa na mawazo ya technolojia huanza kwa wanafunzi vyuoni pamoja na walimu wao

Tanzania walimu wengi wa vyuo hawajafanya practical ya kazi zao

Mfano:Bashiru wa ccm wa sasa akirudi chuo atakuwa mwalimu mzuri wa Political science alishajua mfumo wa siasa, Kabla alikuwa anawafundisha wanafunzi alichofundishwa na sio uhalisia

Mfano:Benno Ndulu Governor mstaafu BOT akirudi kufundisha economics chuo hasa mambo ya Inflation,Monetary economics au Public finance atafundisha uhalisia zaidi kwani ameyaishi maisha ya uchumi wa nchi kwa zaidi ya miaka nane anafahamu pressure ya kazi,Pressure ya forex ikipungua kwenye reserve

Elimu ya Tanzania haijawa direct link na kinachofanyika makazini

Walimu wengi wa Finance au Banking vyuoni hawajawahi fanya kazi kwenye taasisi yeyote ya fedha hapa nchini ,Sasa huyo mtu anakufundisha habari za mikopo au credit management wakati yeye mwenyewe hajui kinachoendelea kwenye soko la mikopo,Mwalimu anatumia vitabu vya india kuelezea Banking sector ya Tanzania

Mfano, Graduate wa umeme ukimpeleka Tanesco anaona malue lue, Darasani wanafundishwa umeme wa miaka ya 1970
Basi waalimu wa vyuo wangepewa nafasi katika taasisi mbalimbali kuwa washauri (consultants) ili waweze kuoanisha mazingira ya darasani na uhalisia, hiyo ingepelekea anahakikisha mtaani wanafuata sheria na taratibu na pia darasani wanafunzi watapata mwanga wa nini hasa kinatokea mtaani.
 
Mawasiliano (ICT & Telecom)- UDOM(CIVE)
Asee hawa watu wapo smart sana kwenye sekta iyo kama wakati ungekuwa unarudi nyuma Ningesoma Cive Degree yangu ya mambo ayo
 
PRIVATE U
Ni muda muafaka kwa Waajiri na Makampuni binafsi kutoa mrejesho kwa Wanafunzi wa Vyuo gani Wanafanya Vizuri katika Maeneo yao ya kazi. Pia tunaomba watoe mrejesho ni maeneo gani ambayo yana upungufu mkubwa wa Wataalam wa Fani husika.

Nikimaanisha kuna Position inabidi Human Resource Officers kutumia muda mwingi kurudia kutangaza Ajira ya nafasi husika kwa kukosa Watu wenye sifa sahihi (Job employment Re-advertisement)

Nchi za wenzetu feedback kama hizi huvisaidia Vyuo ku-restructure baadhi ya Course zao ili kuendana na matakwa ya Soko la ajira.
Toa Maoni yako chuo bora kwa Kupika Wanatahiniwa katika Fani zifuatazo:

1. Usafirishaji (Anga na nchi Kavu)
2. Biashara
3. Fedha, Benki na Bima
4. Uhandisi (Civil, Chemical, Electrical, Machenical. etc)
5. Afya (Udaktari, Uuguzi, Maabara)
6. Utawala (Public Admistration, Human Resources)
7. Mawasiliano (ICT & Telecom)
8. Kilimo na Mifugo ( Veterinary Medicine, Animal Health, Food science, Agriculture)
8. Madini (Geology)
9. Utawala katika Afya (Public Health)
10. Mipango
11. Usafiri (Maji)
12. Uandishi wa Habari na Mahusiano
13. Ualimu (Sanaa)
14. Sayansi ya Siasa
15. Ualimu (Sayansi)
16. Sheria
17. Social Work
18. Uchumi
PRIVATE
UNIVERSITIES
 
Kwa mfano Elimu gani ambayo mtu anaweza kujifunza mwenyewe bila Mwalimu?
Zipo nyingi ila nakutajia chache ambazo mimi nimejifunza mwenyewe
1.uchoraji(Artist).
2.programming from scratch mwenyewe languages 8.
3.lugha za kigeni nimejifunza mwenyewe nipo fluent kwenye romance languages zote .
 
Zipo nyingi ila nakutajia chache ambazo mimi nimejifunza mwenyewe
1.uchoraji(Artist).
2.programming from scratch mwenyewe languages 8.
3.lugha za kigeni nimejifunza mwenyewe nipo fluent kwenye romance languages zote .
Hakuna kitu kama hicho. Kwa mfano, programming hata kama ahukukaa darasani lakini kupitia YouTube tutorials tayari ulikutana na walimu huko.
Jua elimu/Mwalimu siyo lazima iwe formal schooling hata informal schooling, tayari ulipata mwanga pa kuanzia kupitia hiyo informal schooling.
 
Back
Top Bottom