Waajiri na Makampuni Binafsi, toeni Maoni yenu vyuo vipi vinapika wataalam vizuri

Carica_papaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
758
1,232
Ni muda muafaka kwa Waajiri na Makampuni binafsi kutoa mrejesho kwa Wanafunzi wa Vyuo gani Wanafanya Vizuri katika Maeneo yao ya kazi. Pia tunaomba watoe mrejesho ni maeneo gani ambayo yana upungufu mkubwa wa Wataalam wa Fani husika.

Nikimaanisha kuna Position inabidi Human Resource Officers kutumia muda mwingi kurudia kutangaza Ajira ya nafasi husika kwa kukosa Watu wenye sifa sahihi (Job employment Re-advertisement)

Nchi za wenzetu feedback kama hizi huvisaidia Vyuo ku-restructure baadhi ya Course zao ili kuendana na matakwa ya Soko la ajira.
Toa Maoni yako chuo bora kwa Kupika Wanatahiniwa katika Fani zifuatazo:

1. Usafirishaji (Anga na nchi Kavu)
2. Biashara
3. Fedha, Benki na Bima
4. Uhandisi (Civil, Chemical, Electrical, Machenical. etc)
5. Afya (Udaktari, Uuguzi, Maabara)
6. Utawala (Public Admistration, Human Resources)
7. Mawasiliano (ICT & Telecom)
8. Kilimo na Mifugo ( Veterinary Medicine, Animal Health, Food science, Agriculture)
8. Madini (Geology)
9. Utawala katika Afya (Public Health)
10. Mipango
11. Usafiri (Maji)
12. Uandishi wa Habari na Mahusiano
13. Ualimu (Sanaa)
14. Sayansi ya Siasa
15. Ualimu (Sayansi)
16. Sheria
17. Social Work
18. Uchumi
 
Mwalimu wa chuo kikuu hajawahi kufanya kazi ana claim notisi kama wewe miaka Nenda miaka rudi

Nenda vyuo vingi vya ulaya mambo makubwa na mawazo ya technolojia huanza kwa wanafunzi vyuoni pamoja na walimu wao

Tanzania walimu wengi wa vyuo hawajafanya practical ya kazi zao

Mfano:Bashiru wa ccm wa sasa akirudi chuo atakuwa mwalimu mzuri wa Political science alishajua mfumo wa siasa, Kabla alikuwa anawafundisha wanafunzi alichofundishwa na sio uhalisia

Mfano:Benno Ndulu Governor mstaafu BOT akirudi kufundisha economics chuo hasa mambo ya Inflation,Monetary economics au Public finance atafundisha uhalisia zaidi kwani ameyaishi maisha ya uchumi wa nchi kwa zaidi ya miaka nane anafahamu pressure ya kazi,Pressure ya forex ikipungua kwenye reserve

Elimu ya Tanzania haijawa direct link na kinachofanyika makazini

Walimu wengi wa Finance au Banking vyuoni hawajawahi fanya kazi kwenye taasisi yeyote ya fedha hapa nchini ,Sasa huyo mtu anakufundisha habari za mikopo au credit management wakati yeye mwenyewe hajui kinachoendelea kwenye soko la mikopo,Mwalimu anatumia vitabu vya india kuelezea Banking sector ya Tanzania

Mfano, Graduate wa umeme ukimpeleka Tanesco anaona malue lue, Darasani wanafundishwa umeme wa miaka ya 1970
 
Sijui kama nakosea, ila nadhani UDSM bado ni chaguo namba 1 namba moja la wahitimu wengi wa kidato cha sita kwa fani zote. Hivyo watu wengi waliofanya vizuri mitihani ya kidato cha sita wanaenda udsm. Hii ndo kusema udsm ina chukua cream. Na graduate wengi wa udsm wanafanya vizuri sana wakiingia kazini. Inawezekana siyo kwa sababu udsm wanafundisha vizuri ila ni kwa sababu wanafunzi wenyewe ni wazuri.

Pili, iko hivi. Shuleni au chuoni tunaenda kupata general knowledge kuhusiana na fani fulani. Utakacho kuja kufanyia kazi ni sehemu ndogo sana, ya vile ulivyojifunza. So nategemea graduate anapopata kazi..ajifunze/afundishwe kazi.

Tatizo kubwa ni mentality ya watu wetu. Hawapendi kusoma, hawapendi kujifunza. Wanadhani wakimaliza shule ndo wamemaliza kusoma. Kumbe kusoma hakuna mwisho. Unapoanza kazi ndo inabidi usome sana ili kuboresha kazi yako.

So mimi napenda kuajiri watu ambao wanapenda kusoma. Ndo maana si ajiri direct. Intern miezi 6 ndo ajira inafuata kama utakuwa vizuri.
 
Na graduate wengi wa udsm wanafanya vizuri sana wakiingia kazini. Inawezekana siyo kwa sababu udsm wanafundisha vizuri ila ni kwa sababu wanafunzi wenyewe ni wazuri.
Udsm si ndo nasikia wanaongoza kwa uozo (rushwa, umimi, uzembe, wizi, ubabaishaji, low productivity, nk) huko makazini? Au labda mi nasikia vibaya!
 
Sijui kama nakosea, ila nadhani UDSM bado ni chaguo namba 1 namba moja la wahitimu wengi wa kidato cha sita kwa fani zote. Hivyo watu wengi waliofanya vizuri mitihani ya kidato cha sita wanaenda udsm. Hii ndo kusema udsm ina chukua cream. Na graduate wengi wa udsm wanafanya vizuri sana wakiingia kazini. Inawezekana siyo kwa sababu udsm wanafundisha vizuri ila ni kwa sababu wanafunzi wenyewe ni wazuri...
Mtu kama wewe ndio hao "chaguo la kwanza"!! Mleta mada kataja fani mbalimbali! Kwahiyo unachotaka kusema, mtu mwenye ranch yake akitaka kuajiri mtu wa Animal Science, Veterinary Medicine, na Agricultural Economist, basi sehemu bora itakayotoa hao watu ni UDSM?!

Au kama mtu anamiliki Dental Clinic, basi sehemu ya kupata Dentists Bora ni UDSM?! Yaani wakati una-encourage kuseoma, nina wasiwasi ikiwa wewe umesoma na kuielewa thread fupi tu ya mleta mada!
 
Sijui kama nakosea, ila nadhani UDSM bado ni chaguo namba 1 namba moja la wahitimu wengi wa kidato cha sita kwa fani zote. Hivyo watu wengi waliofanya vizuri mitihani ya kidato cha sita wanaenda udsm. Hii ndo kusema udsm ina chukua cream. Na graduate wengi wa udsm wanafanya vizuri sana wakiingia kazini. Inawezekana siyo kwa sababu udsm wanafundisha vizuri ila ni kwa sababu wanafunzi wenyewe ni wazuri...
Umeongea point ya muhimu sana, hakuna chuo kikuu duniani kinachofundisha watu kufanya kazi.

Mwajiriwa mpya anahitaji 'onjob training', hapo sasa ndio utajua mwajiriwa yupi ni bora na yupi sio, kutokana na wepesi wake wa kutumia maarifa aliyotokanayo chuo kujifunza kazi.
 
First thing first ni graduate mwenyewe... Watu wengi wanaomaliza chuo hapa nchini wanashida kwenye hands on skill...

Waajili wengi wa makampuni binafsi na walio serious pamoja makampuni ya kimataifa yana zingatia professional skills kuliko Academic certificates
 
Ni muda muafaka kwa Waajiri na Makampuni binafsi kutoa mrejesho kwa Wanafunzi wa Vyuo gani Wanafanya Vizuri katika Maeneo yao ya kazi. Pia tunaomba watoe mrejesho ni maeneo gani ambayo yana upungufu mkubwa wa Wataalam wa Fani husika.

Nikimaanisha kuna Position inabidi Human Resource Officers kutumia muda mwingi kurudia kutangaza Ajira ya nafasi husika kwa kukosa Watu wenye sifa sahihi (Job employment Re-advertisement)

Nchi za wenzetu feedback kama hizi huvisaidia Vyuo ku-restructure baadhi ya Course zao ili kuendana na matakwa ya Soko la ajira.
Toa Maoni yako chuo bora kwa Kupika Wanatahiniwa katika Fani zifuatazo:

1. Usafirishaji (Anga na nchi Kavu)
2. Biashara
3. Fedha, Benki na Bima
4. Uhandisi (Civil, Chemical, Electrical, Machenical. etc)
5. Afya (Udaktari, Uuguzi, Maabara)
6. Utawala (Public Admistration, Human Resources)
7. Mawasiliano (ICT & Telecom)
8. Kilimo na Mifugo ( Veterinary Medicine, Animal Health, Food science, Agriculture)
8. Madini (Geology)
9. Utawala katika Afya (Public Health)
10. Mipango
11. Usafiri (Maji)
12. Uandishi wa Habari na Mahusiano
13. Ualimu (Sanaa)
14. Sayansi ya Siasa
15. Ualimu (Sayansi)
16. Sheria
17. Social Work
18. Uchumi
Uhasibu kwa degree ya kwanza nne bora zangu ni kama ifuatavyo
1. Mzumbe University
2. UDSM
3. Institute of Accountacy Arusha
4. Tanzania Institute of Accountacy.

Mimi ni mwajiri na vile vile kazi yangu inanikutanisha na wahasibu wa taasisi mbalimbali
 
Hivyo vyuo vitatu naamini vinafundisha uhasibu vizuri kuliko UDSM. Point inakuja pale the best performers wanapoenda UDSM na kwingine wakaenda wengineo kina sisi. Hivyo vyuo wanapokea Div II za mwisho na III za mwanzo na kuzifanya zisimame kwenye soko wakati UD inachukua I na II za mwanzo na kutumia nguvu kidogo tu.
 
Back
Top Bottom