JONASON
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 461
- 706
Habari ndugu zangu .Kwanza nianze kwa mikasa iliyonikumba mimi ni kijana ambae nimemaliza chuo miaka mitatu nyuma na katika kusaka ajira mara nyingi nimehudhuria usaili sehemu mbali mbali kinachoniuma ni kwamba mimi natoka mkoan na mjini sikua na ndugu huwa nafikia katika nyumba za wagen sasa unakuta umefanya usaili wa kuandika (written interview) mnaambiwa tutawatumia ujumbe sasa unakaa kusubir oral hupat muongozo wowote .Ni bora wawe wanatoa matokeo ya jumla hata katika mtandao ili ujue kama haujafika viwango vyao urudi.Wiki hii nimekuja dsm katka usail wa kampun moja sasa nimefikia gest nimefanya written tukaambiwa tuandike namba za simu mpaka sasa kimya na kila aliefanya hana taarifa yoyote hivyo nashukuru jana baada ya kuishiwa fedha nilitimuliwa gesti nikatoka nikawa natembea tembea mitaani nikakutana na dogo mmoja tulisoma nae shule ya msingi ila nilimuacha madarasa akanipokea mpaka geto kwake akasema nitalala tu ila msosi nijitegemee ..Dahh!! Najuta laki moja yangu niliyoipata kwa kuuza mihogo imeisha kwa safar isiyoeleweka...Basi tunaomba waajir tukija katka usaili ni vema zoezi lisichukue muda mrefu na pia mtu atambue kwamba anaendelea na hatua nyingine ya usaili au arudi kufanya mambo mengine maana tunatumia muda na fedha pia tuwe na huruma jamani tuweke ubinadamu mbele jamani ..Naongea nikiwa muhanga wa hilo suala.