Mwana, kwanini kunitendea hivi? Umeupasua moyo wangu mara ya pili. Jamani muwe na huruma

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Messages
1,758
Points
2,000

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2014
1,758 2,000
Juzi asubuhi saa tatu simu yangu ilikuwa ikiita kwa muda mrefu; iliita ikakata, ikaita tena ikakata, baadaye nikatoka ofisini kwa M.D wangu kuelekea kwangu nikapokea namba ngeni.

Ilisikika sauti ya mwanamke ya upole ikiuliza, "Wewe ni xxxx?" nikauliza, "unamtaka nani?", akasema "Okay, unaongea na Mwanahamisi. Habari za siku?"

Niliuliza Mwanahamisi wa wapi akanijibu, "Aaargh na wewe nawe, Mwanahamisi wa xxxx"

Huyu dada mwaka juzi nilimuona sehemu nikampenda tukawa marafiki, mwishowe nikamwomba uhusiano wa kimapenzi. Aliniambia yeye yupo tayari ila anataka tuzae.

Nlimwambia hapana, tusubiri kwanza, kuzaa kunataka maandalizi nami kwa muda huo sikuwa tayari. Ndani ya week tatu nilijikuta nampenda sana huyu dada, hatukuwahi ku-sex but nilikuwa natoka naye nanunua vitu napeleka kwake.

Siku moja akanambia haoni haja ya kuwa na mimi; yeye anataka mwanaume wa kuzaa naye na mwenye malengo naye. Nlivumilia siku moja, ya pili nikasema nimfuate kwake.

Nilikuta kwake nje kuna gari ime-park, nikaingia ndani getini kwenda gonga kwenye nyumba anayokaa yeye. Alitoka amejifunga khanga tu kifuani, akaniuliza nasemaje. Nilimwambia nimekuja tuongee, aliniambia hapana ana mgeni nisimsumbue.

Niliumia sana, sana. Ndani ya masaa 24 nimeachwa na mwanamke ana mwanaume mwingine?

Leo Mwanahamisi amenipigia anasema tuonane, namuuliza tuonane wapi kwa ajili ya nini, akasema tu ana mengi ya kuongea nami. Sikuwa tayari ndiyo akafunguka alipewa mimba na yule mwanaume then mwanaume akaikataa. Hivi sasa anahangaika kulea mtoto hana la kufanya, duka lake la nguo lilishafilisika akafunga na alipokuwa anaishi alihama na kurudi kwa wazazi wake.

Anaomba tuonane tuongee yaishe, ameshajifunza. Nimeumia sana sababu nilimwambia mapema Mwana, "Tatizo si kukupa tu mimba, mtoto anataka maandalizi na malezi. Subiri ufike wakati muafaka tuamue", akaona mimi sina mipango.

Leo ananiambia anateseka na mtoto, jamaa alishakata mawasiliano na kumbe ni mume wa mtu. Mimi nilisha-move on. Nampenda huyu dada but kovu lake lipo moyoni kila napofikiria siku ile ya mwisho kuonana naye, napata maumivu.

Kinachoniuma ni vile sikutaka aje akumbwe na janga kama hili. Niimwambia Mwana, "Mimi nakupenda ndiyo maana nataka tupate muda kwanza then tuamue, ila kuna wanaume hawatajali hilo, watakupa tu mimba kama utakavyo" Alinijibu yeye anaweza lea hata watoto wawili, mmoja siyo issue kwake.

Leo hii Mwana ametelekezwa nami nashindwa kumrudia, siwezi. Aliniacha kipindi namuhitaji, sina kazi ya kueleweka, yeye ndiyo nilimwona angekuwa faraja kwangu. Nimempigia simu rafiki yake ananambia Mwana amechoka, amechakaa huwezi mtambua.

Hili linaniuma zaidi. Alikuwa mzuri wa sura na umbo, alikuwa anavutia sana Mwana. Leo anarudi kwangu akiwa amechoka kachakaa anataka turudiane. Moyo wangu unakataa ulishaumia sana, kovu lake limeshindwa kufutika. Nilishamsamehe lakini nimeshindwa kusahau alilonitendea huyu dada.

Dada zangu, muwe na huruma. Haya maisha kuna leo na kesho. Some times munatuumiza sana sisi ambao huamini katika mapenzi. Athari zake sometimes huja kuwapata wanawake wengine innocent pia.

Naandika kwa uchungu sana. Naumia kila ninapomfikiria Mwana. I wish asingenipigia. Nsingefahamu yupo katika hali hiyo. Mtu ambaye nilimthamini mwingine kaenda kumharibu na kumtupa! Almost mwezi mzima sikuwahi hata ku-sex naye, jamaa in a short time he did it. Leo mimi nitamfanya nini tena Mwana huyu?
 

Ligaba

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Messages
342
Points
1,000

Ligaba

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2018
342 1,000
Wewe ni kama mwana na mwanaume ni kama wewe.

Hivi unapata wapi muda wa kumfikiria mtu aliyekutaa? Kwangu mwanamke akinikataate na kwa dharau, ni kheri na huwa nikimove on sina haja ya kumfikiria hata afie mbele yangu.
 

Coffee

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2017
Messages
1,085
Points
2,000

Coffee

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2017
1,085 2,000
Dah! Huyo hata usimsikilize ni shetani mkubwa yaani kwa alivyokutenda anapata wapi huo ujasiri wa kukutafuta? Anaamini unampenda so ukimpa nafasi tu umeingia cha kike man.
 

Forum statistics

Threads 1,364,450
Members 520,742
Posts 33,316,805
Top