Waafrika ni Watu wa ajabu

Waafrika ni Watu wa ajabu

Mimi nimeandika hoja zangu kwa kuzingatia misimamo mbalimbali inayoendelea huko duniani,most based on africa. Kuwepo/kutokuwepo kwa Mungu haikuwa core concept yangu. Though naheshimu sana mtizamo wako katika hili na ningependa tuendelee kuelimishana katika hili
ni rahisi tu,

Kama Mungu ni muweza wa yote, na ana upendo kama tunavyosema kila siku, hana sababu ya kuangalia watu wasio na hatia wakiuawa kila siku kwenye hizi vita bila kuingilia kati.....

Labda kama sababu mimi siijui, ila ndo ninaona hivyo
 
Mtoa mada umeongea kitu Cha ukweli. Sana. Nchi zetu za kiafrika utajiri wa rasilimali tulizojaliwa umegeuka kuwa laana. Badala ya neema. Mfano hai ni hapa kwetu Tanzania.

Nchi ya Congo vurugu zote zile zinasababishwa na mabeberu. Juzi nilikuwa naongea na jamaa yangu analinda amani huko anasema vita Ile haiwezi kuisha Leo Wala kesho. Walifanyiwa ambush mbaya mno Kwa kwelekezwa njia waliko jificha waasi. Waliokolewa majeshi ya Kongo yaliyokuwa karibu. Huku helcopta ziko juu.

Unafiki wetu wa Viongozi hasa ndo shida.
 
Hii ndo afrika
IMG-20231018-WA0006.jpg
 
View attachment 2786455
Watu (45,000) wanafariki kila mwezi katika ardhi ya DR Congo kwa sababu ya vita…. Watu 2,000 na ushee israeli na Palestina imekuwa wimbo wa Dunia na waafrika wanaimbishwa pray for this and that..

Utafiti wa International Rescue Committee (@RESCUEorg) unaonyesha watu milioni 5.6 katika miaka 9 pekee (kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2007) walifariki kutokana na vita DR Congo.

Huo ni wastani wa vifo 1,500 kwa siku, lakini sio habari kubwa kwa waafrika. Kwa maana nyingine ni kwamba, kuanzia mwaka 1998 hadi 2007, kila siku DRC kuna vifo vya idadi ya watu karibu sawa hao waliofariki huko Israeli na Palestina

Raia wengi wa DR Congo wanafariki kutokana na kukosa huduma za kijamii kama hospitali, magonjwa mengi ya milipuko na kuambukiza, njaa kutokana na kukosa makazi na utulivu, hawazalishi.

Vita, ukoloni, utumwa, ufisadi yamebadilisha taifa hili ambalo licha ya kuwa miongoni mwa mataifa tajiri zaidi duniani, sasa limekuwa masikini zaidi. DR Congo imebarikiwa kila aina ya madini.

DR Congo nchi tajiri zaidi duniani kwa maliasili. Madini mengi ghafi hayajatumika yenye thamani ya hadi takriban $24 trilioni. Huu ni uchumi wa USA na Ulaya kwa pamoja.

Kuna aina zaidi ya 1,100 za madini katika ardhi ya nchi ya DR Congo. Amana hizi ni pamoja na akiba kubwa zaidi ya madini ya coltan na kiasi kikubwa cha madini ya kobalti.

80% ya ardhi ya DR Congo inafaa kwa kilimo. DR Congo ina eneo sawa na Ulaya Magharibi. Ulaya Magharibi ni England, France, Germany, Italy, Netherlands, Spain, Portugal, Belgium, Austria.. etc.

DR Congo ina hazina ya 10% ya hifadhi ya shaba Duniani. 30% ya cobalt ya Dunia. DR Congo inazalisha 80% ya madini ya coltan yanayotumika kutengeneza simu, ipods, sumaku, Jet engine.

DR Congo inazalisha madini ya Uranium. Vita ya pili ya Dunia, Marekani alipiga miji miwili ya Japan (Hiroshima na Nagasaki) kwa mabomu ya atomic. Mabomu yalitengenezwa na madini ya Uranium.

DR Congo inamiliki ardhi ambayo inatoa madini ya almasi, dhahabu, bauxite, graphite, fedha, zinki. Pia wanayo madini ya lead ambayo yanatumika kutengeneza risasi na mabomu.

DR Congo ina ardhi yenye mafuta. Kuna misitu mikubwa yenye miti mikubwa. Wanyama, vivutio vya watalii katika milima ya Virunga na Ituri. Mito na mabonde yenye unyevu na rutuba. Maziwa na bahari.

Mto Congo ni mto wa pili kwa ukubwa Duniani. Kuna maporomoko (Inga Water Falls) ambayo yanaweza kuzalisha umeme wa kusambazwa Afrika na Ulaya kwa wakati mmoja.

Makundi yenye silaha ya M23, ADF, FDLR, CODECO, RED-Tabara na wengine yamesababisha majanga ya kibinadamu na ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia.

Tangu kuibuka upya kwa kundi la M23 mwezi Novemba 2021, ‘Zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kukimbia makazi yao. Hili ni kundi linalofadhiliwa na serikali ya Rwanda chini ya Rais Paul Kagame.

Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Kongo limelaaniwa kabisa na utajiri wake wa madini hayo. DR Congo ni ulimwengu usio na matumaini kwa raia wake. Ni jehanamu kwa wananchi wake.

DR Congo yenye raia 75 milioni, asilimia 80 ya raia wake, sawa na 60 milioni wanaishi chini ya kipato cha dola moja (Sh2,500). Umoja wa Mataifa wanaeleza, zaidi ya watu milioni 5.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula DRC

Wageni kutoka nje ya DR Congo wamevamia ardhi na kuifanya uwanja wa mapigano na mavuno ya rasilimali za watu wa Congo. Watu wa DR Congo wamebaki kuwa maskini wa kutupwa.

Wageni wamesababisha machafuko, wamevuruga utaratibu wote wa uchumi, wameiba mali nyingi za nchi ya DR Congo. Wananchi wa DR Congo wamekimbia makazi yao sasa ni wakimbizi.

Machafuko yanaifanya DR Congo kuwa nchi tajiri kwa rasilimali Duniani lakini taifa maskini zaidi Afrika wakati mataifa ya magharibi yakiendelea kunufaika na vita ndani ya DR Congo.

Wanaosababisha vita DR Congo ni mabeberu wanaoleta silaha za kivita na misaada ya kijeshi wao wanachimba madini na kupeleka kwao. Tuwaambie Acheni kupora mali ya DRC! Ondoeni mikono yenu DRC!

Hupati waafrika au watanzania wanafunga na kuomba kwa ajili ya nchi kubwa Afrika ya DR Congo. Utawasikia wakichakarika na Pray for Ukraine, Pray for Israeli, Pray for Palestina. DR Congo haikumbukwi.View attachment 2786456
Sisi ni nani kama DRC wenyew wanasema pray for Israel kama wanawaombea washenzi wanaoua watu hospitali nani anawakumbuka.
 
Hupati waafrika au watanzania wanafunga na kuomba kwa ajili ya nchi kubwa Afrika ya DR Congo. Utawasikia wakichakarika na Pray for Ukraine, Pray for Israeli, Pray for Palestina. DR Congo haikumbukwi.

MMM, Martin Maranja Masese
Screenshot_20231019_185811_X.jpg
 
Mwafrika sio mpuuzi na hawezi kuwa mpuuzi. Asilimia kubwa ya Waafrika ni wajinga tu ambao hawataki kujifunza au kusaka maarifa. Ila pale ambapo Mwafrika atasaka maarifa, itakuwa mwisho wa the West dominance duniani.

Soon ujinga utawatoka.
 
Kusema Mwafrika mpuuzi ni kuwaita wazazi wako na mababu zako kuwa wapuuzi.

Wangekuwa wapuuzi usingekuwepo, wangekuwa washakuua, wasingekulea na kukupa stahiki zote, na pia wasingekufunza mambo ya msingi ya maisha.

Tatizo mnadanganyika kuwa wazungu wameleta teknolojia, ni wazungu wachache ndo walijitoa kuleta mapinduzi ya teknolojia, asilimia kubwa ni wajinga tena wengine ni wehu kuliko sisi. Hata sisi ili mapinduzi ya teknolojia yafanyike inabidi watu wachache wajitoe , tatizo la Africa ni kwamba Serikali zenyewe zinaua vipaji Kwa kutokutoa motisha na kuwekeza kwenye utafiti.

Ukisema Waafrika ni wapenda ngono, hakuna binadamu asiyependa ngono, wazungu wanapenda ngono kama sisi, sema wachache ndo hawauendekezi, kama Waafrika wachache wasiouendekeza ngono wakitokea, mabadiliko yataonekana.

Hakuna Mwafrika mpuuzi ila kuna Waafrika wajinga na wapumbavu pia.
 
Umezunguka sana mkuu, sisi Waafrika hivyo vyote vinatuhusu kama ni asilimia kwetu zimezid
 
Utalalamika sana lakini matatizo yote ya duniani yanatokea kwa kupangwa na watu walionyuma ya pazia I mean wakubwa wa dunia(usiniulize ni wakina nani just go and find it for your self) hawa ndio wanamiliki media zote kubwa duniani napia ni watu wenye nguvu sana ambao wanapanga machafuko mengi duniani Kama hizi vita na wanaamua kipi kipewe kipaumbele kufatiliwa dunia kwa maslahi yao wanayoyajua wao wenyewe.

Hivyo sio tu waafrika hata mabara mengine wameingizwa kwenye huu mkumbo wa kupikwa hivyo ucjali ikifika mda wa Kongo pia nayo itaangaliwa Kama palestina na Israeli napia Kama urusi na Ukraine. So stop blaming the African only because there is a lot of people who are already brainwashed due to this conflicts between fake Jewish and Palestine.
 
Back
Top Bottom