Waafrika ni Watu wa ajabu

fuu xkuz

Senior Member
Feb 5, 2016
147
195
IMG_0083.jpg
Watu (45,000) wanafariki kila mwezi katika ardhi ya DR Congo kwa sababu ya vita. Watu 2,000 na ushee israeli na Palestina imekuwa wimbo wa Dunia na Waafrika wanaimbishwa pray for this and that!

Utafiti wa International Rescue Committee unaonyesha watu milioni 5.6 katika miaka 9 pekee (kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2007) walifariki kutokana na vita DR Congo.

Huo ni wastani wa vifo 1,500 kwa siku, lakini sio habari kubwa kwa Waafrika. Kwa maana nyingine ni kwamba, kuanzia mwaka 1998 hadi 2007, kila siku DRC kuna vifo vya idadi ya watu karibu sawa hao waliofariki huko Israeli na Palestina.

Raia wengi wa DR Congo wanafariki kutokana na kukosa huduma za kijamii kama hospitali, magonjwa mengi ya milipuko na kuambukiza, njaa kutokana na kukosa makazi na utulivu, hawazalishi.

Vita, ukoloni, utumwa, ufisadi yamebadilisha taifa hili ambalo licha ya kuwa miongoni mwa mataifa tajiri zaidi Duniani, sasa limekuwa masikini zaidi. DR Congo imebarikiwa kila aina ya madini.

DR Congo ni nchi tajiri zaidi duniani kwa maliasili. Madini mengi ghafi hayajatumika yenye thamani ya hadi takriban $24 trilioni. Huu ni uchumi wa USA na Ulaya kwa pamoja.

Kuna aina zaidi ya 1,100 za madini katika ardhi ya nchi ya DR Congo. Amana hizi ni pamoja na akiba kubwa zaidi ya madini ya coltan na kiasi kikubwa cha madini ya kobalti.

80% ya ardhi ya DR Congo inafaa kwa kilimo. DR Congo ina eneo sawa na Ulaya Magharibi. Ulaya Magharibi ni England, France, Germany, Italy, Netherlands, Spain, Portugal, Belgium, Austria, etc.

DR Congo ina hazina ya 10% ya hifadhi ya Shaba Duniani. 30% ya Cobalt ya Dunia. DR Congo inazalisha 80% ya madini ya Coltan yanayotumika kutengeneza simu, iPods, sumaku na jet engine.

DR Congo inazalisha madini ya Uranium. Vita ya pili ya Dunia, Marekani alipiga miji miwili ya Japan (Hiroshima na Nagasaki) kwa mabomu ya atomic. Mabomu yalitengenezwa na madini ya Uranium.

DR Congo inamiliki ardhi ambayo inatoa madini ya almasi, dhahabu, bauxite, graphite, fedha, zinki. Pia wanayo madini ya lead ambayo yanatumika kutengeneza risasi na mabomu.

DR Congo ina ardhi yenye mafuta. Kuna misitu mikubwa yenye miti mikubwa, wanyama, vivutio vya watalii katika milima ya Virunga na Ituri. Mito na mabonde yenye unyevu na rutuba. Maziwa na bahari.

Mto Congo ni mto wa pili kwa ukubwa Duniani. Kuna maporomoko (Inga Water Falls) ambayo yanaweza kuzalisha umeme wa kusambazwa Afrika na Ulaya kwa wakati mmoja.

Makundi yenye silaha ya M23, ADF, FDLR, CODECO, RED-Tabara na wengine yamesababisha majanga ya kibinadamu na ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia.

Tangu kuibuka upya kwa kundi la M23 mwezi Novemba 2021, zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kukimbia makazi yao. Hili ni kundi linalofadhiliwa na serikali ya Rwanda chini ya Rais Paul Kagame.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo limelaaniwa kabisa na utajiri wake wa madini hayo. DR Congo ni ulimwengu usio na matumaini kwa raia wake. Ni jehanamu kwa wananchi wake.

DR Congo yenye raia 75 milioni, asilimia 80 ya raia wake, sawa na 60 milioni wanaishi chini ya kipato cha Dola moja (Tsh. 2,500). Umoja wa Mataifa wanaeleza, zaidi ya watu milioni 5.7 wanakabiliwa na uhaba wa chakula DRC.

Wageni kutoka nje ya DR Congo wamevamia ardhi na kuifanya uwanja wa mapigano na mavuno ya rasilimali za watu wa Congo. Watu wa DR Congo wamebaki kuwa maskini wa kutupwa.

Wageni wamesababisha machafuko, wamevuruga utaratibu wote wa uchumi, wameiba mali nyingi za nchi ya DR Congo. Wananchi wa DR Congo wamekimbia makazi yao sasa ni wakimbizi.

Machafuko yanaifanya DR Congo kuwa nchi tajiri kwa rasilimali Duniani lakini taifa maskini zaidi Afrika wakati mataifa ya Magharibi yakiendelea kunufaika na vita ndani ya DR Congo.

Wanaosababisha vita DR Congo ni mabeberu wanaoleta silaha za kivita na misaada ya kijeshi wao wanachimba madini na kupeleka kwao. Tuwaambie acheni kupora mali ya DRC! Ondoeni mikono yenu DRC!

Hupati Waafrika au Watanzania wanafunga na kuomba kwa ajili ya nchi kubwa Afrika ya DR Congo. Utawasikia wakichakarika na 'Pray for Ukraine, Pray for Israeli, Pray for Palestina'. DR Congo haikumbukwi!
IMG_0084.jpg
 
kuna migogoro ya kisiasa na sera za kiuchumi ambavyo ni ngumu kwetu kuelewa, vinasababisha naya machafuko....

nchi ya uchumi mdogo yenye maliasili nyingi lazima itaporwa na nchi zenye uwezo

lakini pia kwasababu ya haya yote, nadiriki kusema hakuna mungu
 
kuna migogoro ya kisiasa na sera za kiuchumi ambavyo ni ngumu kwetu kuelewa, vinasababisha naya machafuko....

nchi ya uchumi mdogo yenye maliasili nyingi lazima itaporwa na nchi zenye uwezo

lakini pia kwasababu ya haya yote, nadiriki kusema hakuna mungu

Umeibukia mbali sana mkuu,tujadili kuhusu haya yanayoendelea kwa sasa na sio uwepo/kutkuwepo kwa Mungu
 
Back
Top Bottom