Waafrika mziki wetu umekua?

Waafrika mziki wetu umekua?

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,505
Reaction score
5,096
Hitimisho la muziki kwa miaka ya nyuma lilikuwa ni kutoka huko Marekani na ULAYA maana tuliona wasanii wengi wakipishana kuja Afrika kufanya shoo na kuondoka na vitita vya fedha tofauti na miaka hii.

Nina mwaka wa tatu sasa au zaidi sikuwahi kuona msanii yeyote kutoka America au huko ULAYA kuja huku Afrika hasa Tanzania.

Maswali yangu ni haya:-

1_Mziki wa Afrika umekua?

2_Tumeamua kuachana na wao na kupenda vya kwetu?

3_Suala la Uchumi umechangia kuachana na wasanii wa Marekani na ULAYA kwakuwa walikuwa wanataka fedha nyingi?

Maana hata ule ushabiki wa redioni kupiga nyimbo zao siku hizi siusikii na kuona kabisa wasanii wa huko mbele kuanza kupotea barani Afrika.
 
Yote yanaweza kuwa majibu ila inshort kwa kiasi fulani muziki umekuwa kutokana na kukua kwa teknolojia
 
Mziki umekuwa sana tena sana, yale mambo ambayo tulikuwa tunapata huko kwao pekee, sasa yanapatikana hapa kwetu Afrika kuanzia ubora wa video na sauti pia.
 
Sikiliza muziki wa Marijani Rajabu, Mbaraka Mwinshehe, Salum Abdallah halafu uje uone mapinduzi ya muziki wa kisasa mnaouita ni mziki wa Tanzania uliokuwa kuanzia yalipoanza yale mashairi Kuku kapanda baiskeli, Bata kavaa laizoni . Uje hadi zama za mashairi ya katoto kandi kako ndindindi, nakadhalika. Kusema kweli utashindwa kuelewa kama tasnia ya muziki wa Tanzania inaenda mbele au inarudi nyuma.

Huo muziki wa wasanii watatu wa kwanza niliowataja ndiyo ulikuwa muziki wa asili wa Tanzania. Huo tunaosema umekuwa ni muziki ambao tunautoa kwa wenzetu na kuueleta kwetu tukidhani tunatoa bidhaa yetu kupeleka nje kumbe tunafanya kinyume chake.! Muziki kukua ni zaidi ya show. Ingependeza kama muziki asili wa Tanzania kama zile nyimbo za Saida Karoli, Taarabu ya pwani - Achana na hii wanayoita modani taarabu -, na Singeli ndizo zingekuwa zinachezwa kwenye vituo vya nje na kuwapa wasanii wetu ugali.

Vinginevyo, kwa mtazamo wangu kutoka chini ya sakafu ya moyo wangu, bila chuki, upendeleo na hiyana yeyote kwa mtu au kitu chochote huku nikiwa nimeweka mapenzi binafsi ya mtu A au mtu B pembeni, naomba niseme kuwa sina cha kusema kuhusu mwelekeo wa muziki wa Tanzania. Ahsante!
 
Shukrani[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Back
Top Bottom