The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Duniani kuna dini zaidi ya 99 na madhehebu ya dini mengi yasiyo na idadi. Wakristo wana madhehebu zaidi ya 43,000.
Takwimu zzinaonyesha angalau nusu 54% ya wakazi wa Dunia hii wanaamini kwenye miungu ya mashariki ya kati, yaani miungo ya waarabu na wayahudi, sehemu nyingine wanaamini miungo wao na idadi kubwa ya watu inaongezeka ya kutokuamini muungu wowote. Wachambuzi wanakadiria labda kufikia mwaka 2100 dini inaweza kua ina waamini wachache sana kuliko ilivyo sasa.
Hoja yangu ni kwamba,Afrika tumekua na miungu wetu ama ambao wamekua wakiabudiwa na vizazi vilivyotutangulia miaka na miaka na kwa bahati mbaya ujio wa hizi dini za mashariki ya kati na miungu wao kukawa na kampeni kubwa na mbaya dhidi ya miungu wetu na kudharau miungu wetu.
Ukiangalia uhalisia, hii miungu yote inafanana, hii ya kiafrika na hata ya mashariki ya kati, haina tofauti yoyote, hizi zaka, sadaka, sijui rituals gani zote zinafanana. Kazi yake ni kutoa faraja kwa maisha ya Duniani lakini haina msaada wowote zaidi ya hapo.
Kitu pekee kimesababisha dini hizi za mashariki ya kati kuchukua nafasi zaidi huku kwetu ni documentation, waarabu na wayahudi walijanjaruka mapema, wakaweka hizo ibada zao kwenye maandishi. Ukiangalia hizi dini hazikupata nafasi kubwa sana kwenye jamii ambayo tayari ilikua na documentation ya dini zao kama India, Japan, China na mashariki ya Asia yote.
Je waafrika tumeshindwa nini kuweka kwenye maandishi dini zetu za asili na kubaki kung'ang'ania hizi dini wa jamii nyingine. Good thing kuhusu dini zetu hazikua na chuki kama hizi dini za watu wa mashariki ya kati, hazitaki kulazimisha mtu aamini miungu wake na ukikataa uuwawe. Wataalam wa dini hebu wekeni dini zetu za kiafrika kwenye maandishi mrisishe vizazi.