Wa kwanza kwenda mahakamani awe nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wa kwanza kwenda mahakamani awe nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ubungoubungo, May 17, 2009.

 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wajamenieee, naomba kueleweshwa hapa. JK, na mawaziri wengi tu, nikiwaunganisha na wale mafisadi papa woote, na wananchi wanaopasapoti mafisadi, pamoja na original comedy watoto wa manji na RA.

  Kumekuwa na kauli kuwa "msiwasingizie watu, mwenye jambo alipeleke mahakamani", kauli hiii si ngeni hapa tz. yaani, wanataka watz tusitoe tuhuma za ufisadi kwa watu, tuziache tu mioyoni mwetu, na kama tunataka kuzitoa, tukazitoe mahakamani. wanataka kwamfano mimi nikiwa na tuhuma ninazozifahamu kuhusu RA au manji, nisitoe hadharani. swali langu ni, hivi wa kwanza kwenda mahakamani ni nani? ni mtoa tuhuma au mtuhumiwa? mpaka mtu akatoa tuhuma kama livyofanya Mengi hivi, ina maana anao uhakika, na hivyo ana i alart selikali. kama mtuhumiwa anaona ameonewa ndo awe wakwanza kwenda mahakamani for defamation. kwanini wanataka kutunyamazisha?

  kwanini hata JK anasema tusiseme,kama tuna dukuduku tuziachie mahakama? sawa, tukienda polisi, jeshi letu lenyewe la polisi tunalijua, wanavyofanya mambo kwa rushwa na kutawaliwa na mafisadi. hivi watz tutumie njia gani kuwafichua mafisadi? kwa njia ya polisi haiwezekani, ukienda pale useme RA anatakiwa kuchunguzwa watamchunguza miaka kumi wakati yeye akiendelea kujiimarisha na kupoteza ushahidi. cha maana ni kumuibukia kwenye tz, mikutano au popote pale na kumlipua, kama wao wanaona wameonewa waanze kwenda mahakamani. langu ndo hilo. mnasemaje jamani, nani aanze kwenda mahakamani, waliotuhumiwa au tunaotuhumu, na kwa mazingira yapi, na je itawezekana kupata suluhisho? njia gani watz tutumie kupiga vita dhidi ya ufisadi?
   
Loading...