Vyuo vikuu tumieni mfumo wa division hizi GPA zinatuchanganya wazazi

Habari wanajamvi?
Wazazi siku hizi tumekuwa na hamasa kubwa ya kusomesha watoto wetu hadi elimu ya juu, tatizo kubwa wazazi wengi aidha tumeishia la saba au hatukusoma kabisa.
Sasa matokeo ya watoto wetu yakitoka unakuta tu cheti cha matoto kimeandikwa "pass with honours" sasa mimi kama mzazi nashindwa kujua mwanangu amepasua sana au amepata ufaulu wa chini.
Hivyo naomba chonde chonde tumieni mfumo wa division kwani mwanangu akipata division four najua tu hapa hamna kitu. Naomba kuwasilisha
Kwa kifupi huyo ni kilaza.
 
Jukumu lako kama mzazi ni kusomesha tu, hayo matokeo ni jukumu la mwanafunzi.
 
Sasa huku kijijini ananitafsilia nani wengi wameishia kidato cha nne na mfumo wa division ndio wanauelewa. Hivyo zikiwekwa division ni rahisi zaidi
Sasa huko kijijini hamuwezi hata kugoogle bandugu,halafu si unaweza kusoma hata open kama kuna elimu uliikosa
 
Sasa huko kijijini hamuwezi hata kugoogle bandugu,halafu si unaweza kusoma hata open kama kuna elimu uliikosa
Kwanini mnaogopa division? Mnaficha nini? Au hamjiamini na matokeo yenu yanayoletwa kwetu wazazi?
 
Mkuu sifuatlie hayo mambo mtafutie Kaz tu Mana dunia hii bila connection Kaz hakuna hata waseme wana ajili kwa mfumo gani
 
Mkuu sifuatlie hayo mambo mtafutie Kaz tu Mana dunia hii bila connection Kaz hakuna hata waseme wana ajili kwa mfumo gani
Sawa kwa huyu haiana jinsi ila naomba mfumo uwe wa division ili wanaofuata nisapate tabu kung'amua matokeo yao
 
GPA ni international standard ya elimu ya juu... hayo mambo ya division ni local.... ww una force waweke division kwenye elimu ya kimataifa una force 2... kiufupi wakiweka gpa inakuwa inajulikana popote wana deal na m2 wa level gani... ss hawawezi kubadili mfumo kwa faida ya wa2 wachache... kma huelewi pambana na hali yako..... by the way gpa mbwe mbwe 2.. mtt anaweza akawa na lower second... ila akawa vzr 2 kazini zaidi ya mwenye first class
 
Back
Top Bottom