Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Wakati huu ambapo vyuo vyetu vya elimu ya juu vimegubikwa na matatizo makubwa ya uongozi na sera mbovu za uchangiaji na ukopeshwaji kiasi wanafunzi hawapati nafasi ya kusoma kwa utulivu, MBUNGE wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), amelalamikia kuwepo kwa mavazi yasiyo ya heshima kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na kuitaka serikali kuzuia hali hiyo.
Mheshimiwa Spika, mavazi haya ya wanavyuo yanalishushia hadhi taifa letu hivyo ni vema serikali iweke sheria ya mavazi yanayotakiwa kutumiwa na Watanzania ili kuliongezea hadhi taifa, alisema. Mh. Zambi haoni mambo lukuki muhimu yanayoishushia hadhi taifa letu bali nguo wanazovaa wanafunzi - na hili ameamua kulivalia njuga.
Mh. Zambi haoni habari ya FFU kuyazingira maeneo ya hivyo vyuo kama vile tuko kwenye uwanja wa mapambano kama inatudhalilisha mbele ya dunia - utafikiri tuko Gaza ?. Mh. Zambi, mbunge wa CCM, haoni kama tendo la watoto wetu kudahiliwa mbele ya mtutu wa bunduki linatudhalilisha mno kama taifa.
Mh. Zambi haoni sera duni za elimu ya juu zinavyofanya vyuo hivi kufungwa holela kwa visingizio visivyo na vichwa wala miguu kama vinatudhalilisha kama wazazi. Mh. Zambi haoni watoto wetu wanavyonyimwa fursa ya kupata elimu kwa sababu tu wazazi wao hawana uwezo kwenye karne hii ya 21 kama kitendo cha kulaaniwa ?
Hivi vyote Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), havioni ila katumwa na wapiga kura wake kulalamikia nguo wanazovaa wanavyuo wetu. Hivi hao wapiga kura wake wameona wapi nguo zinazovaliwa kwenye vyuo vingine duniani ikilinganishwa na za wanetu. Je, hili linawaumiza kuliko hoja za maendeleo jimboni Mbozi ?
Kwa hakika namshangaa Mh. Zambi - kwa mtindo huu hatufiki.