Vyuo vikuu kuandamana kote nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyuo vikuu kuandamana kote nchini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 21, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,206
  Trophy Points: 280
  Date::1/21/2009
  Vyuo vikuu kuandamana kote nchini

  *Wanapinga udahili mpya

  Hussein Issa na Kuruthum Ahmed
  Mwananchi​

  WAKATI zoezi la kudahili wanafunzi likiwa linaendelea katika vyuo vya umma nchini, hali imebadilika baada ya mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) kutangaza maandamano nchi nzima yanayolenga kupinga udahili huo na yaliyopangwa kufanyika Jumamosi.

  Mwenyekiti wa TSNP, Mulokozi Elgius aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa maandamano hayo, ambayo yamepangwa kuanzia mkoani Dar es Salaam, yatashirikisha wadau wa elimu nchini wakiwemo wazazi wa wanafunzi hao pamoja na wanafunzi wa wote wa elimu ya juu na wale wa shule za sekondari.

  Elgius alisema maandamano hayo yataanzia Ubungo Mataa saa 3:00 asubuhi na kuishia viwanja vya Jangwani.

  Alisema wamelitaarifu Jeshi la Polisi ili wapatiwe ulinzi na si kwamba wameomba kibali cha maandamano, hivyo akasema wana imani wanafunzi wote wataunga mkono maandamano hayo.

  "Hapa tumeshatoa taarifa kwa Jeshi la polisi ili lituipe ulinzi... sasa ni jukumu lao. Likikataa, tunaendelea na maandamano ili waje watuue kama wanavyotaka," alisema.

  Munishi Deogratius, mbunge wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Daruso) ambayo imetangazwa kuvunjwa na uongozi wa chuo, alisema maandamano hayo yana lengo la kupinga sera ya uchangiaji wa elimu ya juu, kuhitaji wanafunzi wote warudishwe vyuoni bila masharti yoyote.

  "Lengo ni kulinda na kutetea maslahi ya wanafunzi hivyo hatuna nia ya ugomvi na serikali au polisi tunajua watakufa wengi lakini haki itendeke tu," alisema.

  Serikali ilifunga vyuo vikuu saba vya umma baada ya wanafunzi kugomea masomo wakipinga sera ya uchangiaji elimu ya juu kwa madai kuwa mfumo unaotumiwa kujua uwezo wa mwanafunzi kiuchumi (means testing) ili apate mkopo unabagua na hivyo kutaka sera ifutwe, au wanafunzi wote wapate mkopo kwa asilimia 100.

  Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kuwa wameipata barua kutoka kwa wanafunzi hao, lakini akasema jeshi lake litatoa jibu lake kabla ya Januari 24.

  "Hatuwezi kujibu leo kwani tunakaa nayo kwa masaa ishirini na nne ndio sheria ya jeshi la polisi linapoletewa maombi kama hayo, hivyo tutawajibu tu hamna tabu,"alisema Kova


  Makamu mkuu wa UDSM, Profesa Lweikaza Mukandala alikataa kusungumzia suala hilo na badala yake akaelezea kuwa zoezi la udahili linaendelea vizuri na kwamba ulinzi ni mzuri.

  Mukandala alikanusha habari kwamba chuo kinaongozwa kisiasa, akisema kuwa huo ni uzushi mtupu na kwamba chuo hakina dini wala chama.

  Wakati huo huo Patricia Kimelemeta na Ellen Manyangu wanaripoti kuwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeeleza kusikitishwa na kitendo cha serikali kuwafutia udahili wanafunzi 2,000 wa UDSM na kuwakamata wanafunzi wanne kwa madai ya kuandamana kupinga kufutiwa kwa udahili wenzao.

  LHRC imeitaka serikali kuangalia upya mfumo mzima wa uchangiaji elimu nchini na hasa kuipitia sera ya uchangiaji ili kupata mwongozo wa kutatua migogoro hiyo.

  Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Francis Kiwango aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa iwapo itapitia upya sera hiyo, serikali itaweza kupata njia mbadala ambayo itasaidia kupunguza migogoro vyuoni.


  Alisema migogoro iliyopo sasa inatokana na sera mbovu ya uchangiaji elimu ambayo ndio inayotoa mwongozo kuhusu ulipaji wa ada kwa wanafunzi. Alisema ili kutatua matatizo kama hayo, wajibu wa serikali ni kuhakikisha kuwa inawasaidia wanafunzi wote bila ya kuangalia tofauti na matabaka yao.

  Alisema serikali imeshindwa kutafuta njia mbadala ambayo itasaidia kutatua tatizo hilo ndio maana inatumia nguvu za dola kuwatisha wanafunzi badala ya kuzingatia haki zao.


  Udahili kwenye lango la Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce) ulitawaliwa na malalamiko ya wanafunzi, wengi wakiwa wamesimama nje ya geti la chuoni hapo na kudai utaratibu wa kuvaa kitambulisho ili uweze kuingia ndani ni swa na ‘Kipande Yystem'.

  Waliiambia Mwananchi kwa nyakati tofauti kuwa masharti yaliyowekwa ili kuweza kurejea chuoni, likiwemo la kumaliza kwanza kulipa ada, ni magumu.

  "Mimi ninadaiwa Sh50,000 yamatibabu na jina halijatoka na mimi sijui kama watanifukuza shule kwa ajili ya kiasi hicho cha pesa kwani mfukoni nimesaliwa na Sh20,000 ndiyo zinazoniwezesha kuishi mjini hapa," alisema mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa tatu ambaye akutaka jina lake liandikwe na ambaye anatokea Kigoma.

  Pia baadhi ya wanafuzi walisema michango iliyoongezwa kama ya kulipia kitambulisho kipya Sh5,000 haina msingi na inawaongezea mzigo.

  "kuna michango ambayo wameiongeza ambayo mimi naiona kama vile wanajaribu kutoa adhabu kwani mchango wa wa matibabu mwanzo ulikuwa umechanganjwa kwenye ada lakini sasa unajitegemea lakini pia hii Sh5,000 tunayolipa ya kitambulisho niwizi mtupu kwani kitambulisho akijabadilika kitu ukilinganisha na kile cha awali zaidi ya rangi, lakini namba ni ileile, hadi picha" alisema mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina moja la Bonge.


  vitu vingine ambavyo vimelalamikiwa na wanafunzi hao ni kulipia vyumba kwa awamu ya pili wakati walishalipia awali kabla ya mgomo.

  "Uongozi wa chuo unasema kiendacho kwa mganga hakirudi, kwa maana hiyo hawazitambui Sh60,000 tulizo lipa kwa ajili ya muhula ambao hatukusoma, sasa kama si wizi wa machomacho, ni nini," alihoji mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliyekataa kutaja jina.
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Ni wazo zuri, tutawaunga mkono. Ili mradi tu wajitahidi kukwepa vurugu ili wasije waka-undermine arguments zao.

  Mahatma Gandhi aliwahi kusema yafuatayo:

  "I cannot teach you violence, as I do not myself believe in it. I can only teach you not to bow your heads before any one even at the cost of your life. I object to violence because when it appears to do good, the good is only temporary; the evil it does is permanent."

  Wawe makini pia kwani kwa hali ilivyo 'wapinzani' wao wanaweza kupandikiza watu walete fujo ili ionekane ni maandamano ya vurugu na si kudai haki.
   
 3. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wazo siyo zuri la kuandamana maana mambo mengine wanachangia wao. Unajua unaweza kuwa una haki kwenye suala fulani ila the way utakavyoliwakilisha ukaonekana ni mkorofi.

  Wawe makini maana virungu ni vya bure wanaweza wapitisha na haki wasiipate.
   
 4. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,196
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Du!!! Ebwana Eeeeeh

  I dont think kama hao 'washika Mpini' watawakubalia

  cha muhimu ni kuwashawishi waTz wote tuandamane pamoja nao. Ni jukumu letu sote
  kuwatetea hawa wanazuni kwa maslahi ya taifa.
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kauli ya Kova itakuwa hii ikifika ijumaa
  Hii itakuwa kauli ya kupoteza muda udahili ukamilike. Na wakipeleka maombi mapya jumatatu jibu ni Ijumaa- Udahili umeisha anayetaka kuingia darasani aingie asiyetaka arudi nyumbani.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Jan 21, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hivi serikali inaamini kuwa inaweza kuwazuia wanafunzi??

  bila suluhisho la kudumu , hili swala halitaisha kibabe, wapende wasipende, LITAKUWA KAMA MWIBA KILA MWAKA KILA SIKU.
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni muhimu kwa Watanzania wote kuunga mkono maandamano hayo kwani Elimu ya Tanzania sasa ipo gizani kwa kuwa wasio na uwezo kifedha watakosa elimu.
   
 8. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nyie madogo acheni kudanganyana tulieni someni mmalize shule msipoangalia mtamaliza 20015 huko maana mnachokidai wakuu wenu wa nchi walishasema tena kwa msisitizo mkubwa kuwa sera ya uchangiaji elimu haiwezi kubadilika kama mnavyofikiria nyie, sasa hebu angalie ni viongozi wangapi wa DARUSO ambao wamekwisha kamatwa kutokana na maandamano mliyotaka kuyafanya pale getini siku ya jumatatu?? Basi kama viongozi wenu wapo selo sasa hivi hapo mjue wanawatetea lakini kama wapo nje wanakula kuku na wale wengine ndo wameshikiliwa na kupelekwa mahakamani mh hapo kuweni makini sana na hao viongozi wenu maana kama wao ni wapigania haki ya wanafunzi wote basi walistahili kuwepo huko mahakamani kuonyesha kuwa kweli wanauchungu na nyinyi, hebu pevukeni akili kidogo hao jamaa wanajua kuw awazi ngoma imekula kwao waligoma kujaza forms za kudahiliwa upya na sasa mambo yamewaendea vigumu wanaamua kushinikiza migomo isiyokuwa na mpango, ankeni mtapotezewa muda wenu bure.
   
 9. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Kama mwanafunzi anapinga kuchangia elimu akae nyumbani aache vurugu wengine wataka kusoma.
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kama wanafunzi wanaamini wanaonewa ni kwa nini hawaendi kumshitaki anayewaonea mahakamani??? Kwa nini wanapendelea political methods za kudeal na mambo na kusahau kabisa legal methods? Au wanajua kuwa hawawezi kushinda kesi? Hayo maandamano ni ya kipuuzi na kama tunataka kuwasaidia hawa vijana wanaotakiwa kuconcentrate kwenye kutafuta elimu tuwaambie in their face kuwa they are not who they think. Wajaze form walizopewa, na waendelee na masomo. Asiyejaza form hataki shule. Aliyeshindwa kutimiza masharti lakini akajaza form atafanyiwa reassessment ili aweze kuruhusiwa kuendelea na masomo kama ilivyoelezwa na wizara. Sasa upuuzi wa maandamano wa nini???mnataka kuwatetea watu wasiojaza form za kuomba kurudi shule!!! Hawataki kusoma hao, wangetaka kusoma wangejaza hizo form. Wasiokuwa na ada wasihofu, hao wote watapewa fursa ya kusoma ila wanahitajika kuwa na subira.
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Vijana wanahitaji mwongozo. Wanatangazia wenzao nchi nzima maandamano kabla ya kupata idhini ya polisi. Wanasema wametaarifu polisi kwa hiyo wasipotaka kuleta ulinzi basi waje wawaue. Kwa hiyo unaemshuku kuwa anaweza kukuua ndio huyo huyo unamwomba aje akulinde halafu kibali chake cha kuundamana hutaki! Uongozi wao una dosari.

  Kuna kiongozi wao mmoja juzi juzi alikuwa naive akaenda kuhojiwa na polisi bila wakili, anasema alikuwa comfortable na polisi wa Kibongo. Maafande wa Kova hawajui cha Miranda rights wakamuuliza maswali mia nne usiku kucha bila time out, alipata kipande uso kibaya sana kidogo arudishe namba!
  [​IMG]
   
 12. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wanafunzi UDSM kizimbani
  Nora Damian

  WANAFUNZI watano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shitaka la kufanya mkusanyiko usio halali.

  Wanafunzi hao ni Anthony Machibya, Owawa Juma, Sabinian Pius, Titus Ndula na Paul Issa.

  Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Kenyela mbele ya hakimu mkazi, Victoria Nongwa kuwa wanafunzi hao walitenda kosa hilo Januari 19 mwaka huu saa 3:45 asubuhi katika maeneo ya chuo hicho.

  Ilidaiwa wanafunzi hao walibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali ambao ulikuwa umejielekeza kuleta hasira na kujenga chuki kwa watu wengine.

  Baadhi ya ujumbe uliokuwemo katika mabango hayo ni, "Nyerere angefufuka leo angelia machozi ya damu", "Kweli Kikwete umesahahu umaskini wa Watanzania wako", "Hivi Pinda wewe ni mtoto wa mkulima", "Wazazi wetu tuoneeni huruma tunateseka jamani" na "Vyuo vya uma vimeuzwa kwa matajiri".

  Hata hivyo, wanafunzi hao walikana shitaka hilo na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika. Kenyela aliwasilisha maombi kupinga dhamana kwa washitakiwa.

  Maombi hayo yaliungwa mkono na hati ya kiapo, ambapo Kaimu Mkuu wa Upelelezi wa mkoa wa Kinondoni, Koka Moita alidai kuwa washitakiwa wakiachiwa watavuruga zoezi la udahili linaloendelea chuo kikuu.

  Moita alidai pia kuwa ana taarifa za kuaminika kwamba mshitakiwa wa pili ameandaa maandamano nchi nzima yanayotarajiwa kufanyika Januari 24, mwaka huu wakati hajatoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika na masuala ya ulinzi.

  Wakili wa upande wa utetezi, Flugency Massawe alipinga hoja hizo kwa madai kuwa makosa yote wanashitakiwa nayo washitakiwa yanastahili dhamana na kwamba, hakuna kiapo kinachoendana na kosa la washitakiwa.

  "Mahakama haifanyi kazi kwa hisia chuo kimefungwa kwa muda mrefu na hakuna chochote kilichofanywa na washitakiwa wakati huo," alisema Massawe.

  Baada ya kusikiliza hoja zote hakimu Nongwa alitupilia mbali hoja za upande wa mashitaka kwa kuwa washitakiwa bado ni watuhumiwa, hadi mahakama itakapothibitisha kosa lao.

  Hakimu Nongwa alitoa masharti ya dhamana kwa washitakiwa akiwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa serikali atakayesaini dhamana ya Sh 500,000.

  Nongwa alisema washitakiwa pia hawaruhusiwi kwenda kwenye maeneo ya chuo kikuu bila ruhusa ya mahakama na hawaruhusiwi kufanya mikutano bila ruhusa kutoka mamlaka husika na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi Oysterbay kila Ijumaa asubuhi.

  Washitakiwa hao walirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 5 mwaka huu itakapotajwa tena.

  Huku hayo yakiendelea Tumsifu Sanga anaripoti kuwa Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova alisema hatatoa kibali cha kuandamana kwa wanafuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam mpaka atakapopata uhakika wa hali ya usalama barabarani kwa siku hiyo.

  Kamanda Kova alisema Jeshi lake limepokea barua ya wanafunzi hao ikilitaka jeshi la polisi kutoa ulinzi siku ya Jumamosi katika maandamano ya wanafunzi hao kupinga sera ya uchangiaji wa elimu ya juu ombi lao litafanyiwa kazi kwa muda wa masaa 48 na uwezekano wa kukataliwa ama kukubaliwa upo na si kuhusiana na maandamano kwa kuwa hawakuomba kibali cha kuandamana.

  "Jeshi la polisi lina taratibu zake wao waliomba kupewa ulinzi hawakuomba kibali cha kufanya maandamano, hivyo tunatarajia kujadili barua yao ya kuomba ulizni na si maandamano kwa kuwa barua yao tumeipata na tunaifanyia kazi ndani ya masaa 48 na tutawapa jibu la barua yao kulingana na hali ya usalama itakavyokuwa siku hiyo," alisema Kamanda Kova.

  Wakati huo huo, Hussein Issa na Patricia Kimelemeta wanaripoti kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kimekiri kuwa sera ya uchangiaji wa elimu kwa vyuo vikuu nchini ina upungufu ambao yanahitaji kufanyiwa marekebisho.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Makamu wa Chuo anayeshughulikia utawala, Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa wanachosubiri wao ni kuona kuwa Waziri Maghembe anaiwasilisha bungeni ili ijadiliwa na kupitishwa.

  "Kweli tumeona mapungufu yapo, tumeunda tume ambayo iko chini ya Profesa kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) kwa ajili ya kukusanya maoni na kuikabidhi kwa waziri ili aweze kuifikisha bungeni kufanyiwa marekebisho,"alisema Profesa Mgaya.

  Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, wanafunzi walipaswa kuwa na uvumilivu ili wajue uamuzi wa bungeni ambalo ndile lenye mamlaka ya kubadili sera.

  Alisema kubainika kwa tatizo hilo kulitokana na fomu mbili za wanafunzi mapacha ambao wanalipiwa na mzazi mmoja huku kila mwanafunzi akiwa na daraja lake la malipo. Mmoja alikuwa analipiwa daraja A na mwingine C, hivyo kusababisha mkanganyiko baina ya wanafunzi hao.

  Alisema hata hivyo katika fomu zilizojazwa na wanafunzi wengine kumekuwa na mikanganyiko mingine baada ya watoto wa vigogo kuwekwa katika daraja la kwanza na wanaotoka katika familia ya kawaida

  daraja tatu.

  Profesa Mgaya alifahamisha kuwa kutokana na hali hiyo, waliona bora sera hiyo ipitiwe upya.

  Hata hivyo, udahili chuoni hapo unaendelea chini ya ulinzi mkali wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na mafisa wa usalama wa taifa waliotanda kila eneo.

  Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini(Uvejuta), Silinde David alisema maandamano yao yatabaki pale pale hata kama viongozi wao wamekamatwa.

  "Sisi tutafanya maandamano hata kama wenzetu wamekamatwa," alisisitiza.
   
 13. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sina uhakika na hii imekaaje kisheria.

  Lakini dhana hii ya kutoa taarifa tu inatumika na wengi tu, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa na vya kirai.

  Mantiki niliyoisikia ni kwamba sheria ya kuomba kibali inapingana na sheria nyingine au katiba ya nchi (au kitu kama hicho, sikumbuki sawa sawa).

  Kwa hiyo argument yao mara nyingi ni kwamba, kisheria si lazima kuomba kibali, bali unatakiwa utoe taarifa tu kwa polisi ili watoe ulinzi wakati wa maandamano hayo.
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Ukisikiliza lugha za hawa wanaoandaa maandamano utaona kuwa wanahitaji msaada mkubwa kimawazo.

  Kuandamana ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania. Utaratibu uliopo ni kwamba ukitaka kuandamana unatoa taarifa polisi ili watoe ulinzi. Polisi kama chombo kinachosimamia ulinzi na usalama kinatathmini hali ya usalama wakati wa maandamano hayo na uwezo wake wa kutoa ulinzi. Polisi wakiridhika kuwa hali ya usalama itakuwa shwari na wanaweza kutoa ulinzi then wanakuja kutoa ulinzi bila tatizo, lakini iwapo tathmini ya polisi itawaonyesha kuna hatari ya kutokea machafuko na hali ya kukosekana usalama wakati wa maandamano basi ni JUKUMU lao kuzuia maandamano hayo. Iwapo wanaoandaa maandamano watahisi kuwa polisi haijawatendea haki kuzuia maandamano kwa ''kisingizio'' cha hali ya ulinzi na usalama, wanapaswa kwenda mahakamani kuishitaki polisi kwa kuwazuia kutumia haki yao ya kikatiba - kwa kuwafanyia uonevu. Polisi watawajibika kuionyesha mahakama vielelezo vyote vilivyowafanya waamini kuwa halia ya ulinzi na usalama wakati wa maandamano hayo haitakuwa shwari.Mahakama itatoa maamuzi. Ambaye hataridhika na maamuzi yatakayotolewa atakata rufaa katika ngazi husika za mahakama. Maamuzi ya mahakama ndio ya mwisho, na hii tabia ya vikundi vya watu kuamua kuwa watafanya wanalotaka wao bila kujali taratibu zilizopo inaashiria aidha kupenda vurugu, kuwa na uelewa mdogo au tabia ya kitoto.

  Nitatoa mfano kidogo hapa: Kila mtanzania ana haki ya kwenda mahali anapotaka ndani na nje ya nchi - freedom of movement, lakini iwapo kutakuwa na epidemic ya cholera katika kata fulani, basi watu watazuiwa kuingia na kutoka kwenye kata hiyo mpaka ugonjwa huo utakapodhibitiwa. Sasa kwa mantiki kama za hawa wanafunzi wa UDSM, wao wangesema wataingia tu kwenye kata yenye cholera kwa sababu ni haki yao ya kikatiba kwenda mahali wanapotaka! Hii siyo busara. Wapeni wanafunzi wa UDSM ushauri.
   
 15. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Very discouraging coward type of words. Lakini ukisoma hiyo signature yako unaweza kujjiua wewe ni mtu wa aina gani. Logic ya darasa la sita.
   
 16. L

  Labibah Member

  #16
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Please please help them,give them a good technics to make things moving dude.
   
 17. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yeye pia anataka kusoma; kwa nini akatazwe kwenda na amefaulu vema ktk mazingira magumu kuliko hao wenye hela na vyeti vya kufoji? Tafakari vema sio kuongea tu au wewe ndio wale ambao hawajui adha ya wananchi wengi wa Tz?
   
 18. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Coward??
  What i think is that the whole issue is being politicised! DARUSO...now TSNP all these organisations lack reasoning. They are taken for a ride by the political leaders who are just trying to play their cards under the table.

  I was once a student at UDSM and we used to have that thing called SOLIDARITY and within our faculty we had that thing called FoE spirit all these were to make each person reason with one another and come up with the best ways to go through and get what you want in a more convenient way. However finally we still had a lesson that whenever the University was closed due to strikes/demonstrations we lost more than we gained > most guys had to Disco some had to do carry overs/ repeat years etc!!

  Lets be frank here guys as much as these students want to pursue their education they still need to have better ways to reason and fight to get what they want. Vijana jiungeni na muifanye sauti yenu isikike lakini mkimobilize such things like maandamano & violence you wont get anything. There are alot of ways why not look for the best one..why rely on the traditional DARUSO ways???
   
Loading...