Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vya elimu ya kati na elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi Serikali itakaposema vinginevyo
Pia, amesema Rais Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi zilizokuwa zifanyike Aprili 26, pamoja na Sikukuu za Wafanyakazi za Mei Mosi ili kuepuka msongamano na kuzuia kusambaa kwa #COVID19
Aidha, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia leo jumla ya Watu 53 wamebainika kuwa na virusi vya Corona ikiwa ni ongezeko la Wagonjwa wanne ambao wote wapo Jijini Dar
Amesisitiza kuwa Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa Shule, Vyuo na shunguli za michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima hivyo maeneo hayo yataendelea kusalia katika Karantini na Wanafunzi wote waendelee kubaki nyumbani