Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,867
Ushauri wa bure! Usijaribu kamwe kumdhihaki mtu aliyetekwa kisha kwa muujiza tuu akaachiwa huru na watekaji wake.... Mateka wengi hupotea moja na moja
Dhana za kuteka zina viasili vingi lakini vinavyojulikana sana ni
Kwa nia ya kupata kipato
Kwa nia yake kutimiziwa mambo fulani
Kutishwa
Kulazimishwa kusema jambo fulani
Visasi
Kuzibwa mdomo
Masilahi ya kisiasa
Kule ndani kule (anapokaa chatu) kuna vyumba maalum vya mateso... Na kuna professional watesaji...hawa ni binadamu wasio na roho ya huruma... Hawa kiasili ni watu wenye roho ngumu na mbaya na huandaliwa na kupewa mafunzo maalum... Mafunzo ya kukutesa na kukuumiza ndani kwa ndani
Hawa ni watu wenye akili ya umeme wa phase moja, hawatafakari chochote, wao ni watu wa kupokea amri na kutekeleza... Basi... Wakiambiwa tesa wanatesa! Wakiambiwa chinja wala hawawazi mara mbili... Hawana fikra za familia yako ndugu zako nknk
Unaifahamu waterboard? Kuna mateso mabaya na ya kikatili huko.... Ukiona mtu karuhusiwa kufanya press conference lakini anababaika Sana na kujichanganya mno.... Usimlaumu, usimdhihaki kukutaka na makubwa