Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,638
- 220,409
Sarah alitoka kwenye familia nzuri sana, baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu alianza kazi kwenye wilaya moja. Alikuwa na mawasiliano na boyfriend wake wa tangu shuleni. Huyu alikuwa mgeni wake ambae alimtembelea mara kwa mara wakati huo akiwa chuo kikuu. Sarah alijua huyu ndiye mume wake kwani ndiye alikuwa boyfriend wake wa kwanza.
Mambo yalibadilika Sarah alipopata ujauzito. Boyfriend alishauri mimba itolewe. Sarah alikomaa na mimba yake licha ya jamaa kukata mawasiliano. Wakati wa kujifungua familia yake ilimpa msaada mkubwa. Alipata mtoto wa kike alimuita Michelle.
Sarah aliendelea na kazi na malezi ya Michelle, walipanga chumba na sebule na Sarah alijiongeza kwa kupika vitafunwa pembeni na ajira. Hawakuwa na maisha mabaya na Sarah alikuwa mwendaji kanisani kila Jumapili na mtoto wake alipata mafundisho yote ya dini.
Kule kazini kulikuwa na Mwalimu Betty ambae binamu yake alikuwa anatafuta mke. Binamu wa Betty alikuwa mfanya biashara mkubwa sana. Licha ya biashara alikuwa anagombea ubunge. Sarah alionekana kuwa chaguo bora la binamu ambae nitamuita mr P for politician.
Baada ya harusi kubwa Sarah na Michelle walihamia kwenye mji mkubwa waliishi kwenye nyumba ya ghorofa pamoja na mr P. Michelle alipata chumba chake, alipewa dereva wa kumpeleka shule na shule alisoma English Medium.
Michelle alipofikisha miaka 12 wakati huo mr P biashara zimeshamiri na sasa ni mheshimiwa alianza kum molestar Michelle akimtisha kuwa akimwambia mama yake watarudi kwenye chumba chao kule walikotoka.
Michelle alitunza siri mpaka alipopata uja uzito akiwa na miaka 15. Wakati huo Sarah na mr P walikuwa na binti wa miaka mitatu. Mr P alimkataza Michelle kusema Baba wa mtoto akimuahidi kumpeleka Ulaya kusoma baadavya kujifungua. Ni kweli baada ya kujifungua Michelle kwanza alihamishiwa shule ya bweni kumaliza shule na alipelekwa Ulaya kwa masomo ya juu.
Michelle alipata mtoto wa kiume. Mr P alimwambia Sarah akubali jukumu la kumlea mjukuu, mr P alikuwa na furaha moyoni ya kupata mtoto wa kiume. Alimhudumia kwa kila kitu.
Machoni mwa Sarah mr P alikuwa ni malaika, mwanaume gani akukute na mtoto amsomeshe na hata kumlea mtoto wake bila malalamiko.
Ninakumbusha tu vyote vinga’aavyo si dhahabu.