Vyoo vya UDSM vinatia aibu (95% vimeziba)

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,494
2,000
Nikiwa nimejiunga UDSM mwaka huu kwa ajili ya kuongeza Elimu toka nimeingia hapa mtu ukibanwa na haja inabidi ujifikirie mara mbili ama uende porini (Hasa Pori lile la Kuelekea Changanyikeni au ukimbilie Mlimani City.

Jana nilibanwa na haja kubwa kila choo ninachokwenda kimejaa/kuziba. Nilianza kule COET, kisha nikaja Botany, Maktaba, SRs, Mathematics, Physics vyote vimeziba/kujaa hivyo huwezi kukitumia.

Ninachojiuliza; Je, Uongozi wa Chuo Kikuu unaliona hili? Jumla ya wanafunzi zaidi ya 15,000 mlionao na hivi vyoo kujaa hamuoni ni hatari? Mnataka tujisaidie porini mpaka lini?

Bora sisi wanaume tunaweza kujistiri huko porini zaidi nawaonea huruma kina dada. Na hali zao si rahisi kusathimili MAPORINI kama sisi.
 

sokwe

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
2,027
2,000
Tatizo Hilo lipo miaka nenda rudi!!! Aisee sio kujaa tu hata wanafunzi wanachangia uchafu na kuziba kwa vyoo! Wakati nasoma nilikuwa najiuliza kuna faida gani ya kujidai wasomi hata matumizi ya kistaarabu yanatushinda, lakini pia vyoo havina watu wa kusafisha makini... Inaita aibu sana na kinyaa.
 

mckenzie

JF-Expert Member
Apr 8, 2013
344
0
Tatizo Hilo lipo miaka nenda rudi!!! Aisee sio kujaa tu hata wanafunzi wanachangia uchafu na kuziba kwa vyoo! Wakati nasoma nilikuwa najiuliza kuna faida gani ya kujidai wasomi hata matumizi ya kistaarabu yanatushinda, lakini pia vyoo havina watu wa kusafisha makini... Inaita aibu sana na kinyaa.

Ni tabu sana. Ila naomba niulize kitu kingine huwa kinanitatiza sana Tanzania....toilet paper ni shillingi ngapi? kwanini taasisi ziko radhi watu watumie magunzi na makaratasi magumu yanayosababisha vyoo kuziba na kutumia gharama nyingi zaidi kuzibua. Cry my beloved motherland.
 

Sista

JF-Expert Member
Sep 29, 2013
3,210
2,000
Chuo kinachukua wakuja hawapewi orientation ya kutumia vyoo vya kizungu. huko mmejaza pedi, magome ya miti na makaratas mnategemea visizibe!!! sio siri UDSM vyoo vichafu harufu imejaa makoridoni hadi library
 

sungura1980

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,910
1,195
Hivi nyie mnaenda Chuo Kikuu Ku.NYA au kusoma? kutwa kucha mnalalamika VYOO kwani mnasomea vyooni? Sijawahi kusikia mtu analalamika Maktaba hakuna vitabu vya kutosha, up-to date journals au upungufu wa wahadhiri. Nyie mmekalia VYOO na KANTINI tena unaweza ukakuta huyu aliyeandika hapa anasoma BA KISWAHILI na Mkopo kapata 100% sasa akili yake inawaza kula tu ndo maana muda wote anafikria wapi ataenda kubwaga uhar.o wake. Acheni Ujing.a Nyie pigeni shule pamoja ubovu wa vyoo UDSM imezalisha watu maarufu duniani ikiwemo Marais kadhaa hivyo kuendelea kulalamika vyoo vyoo hakutabidilisha kitu piga shule ukiwa na haja kimbilia Porini kama wenzako maisha yanaenda Maliza shule uigie mtaani ukifika huko jenga choo chako sasa.Hapo chuoni unapita tu

Mkuu kwa kweli tunalalamika mawaziri mizigo na mabumu,lakini wewe ni mzigo zaidi na bomu zaidi,naogopa ban vinginevyo ningekuandika matusi!Karne hii hujui umuhimu wa vyoo!Aibuuu,lizomeeni hilooo, hilooooo!
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,636
2,000
Umechukua hatua gani kutoa taarifa rasmi kwa uongozi wa Chuo au DARUSO? Au unategemea wapite humu JF kuisoma?
 

sungura1980

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,910
1,195
Nashukuru mleta uzi kulileta tatizo hili ingawa sio mara ya kwanza kuona thread hii ya vyoo UDSM!
Hata mimi nimejiunga takribani wiki 7 sasa kwa ajili ya kuongeza nondo kidogo,lakini kwa kweli tatizo la vyoo limekuwa likinishangaza sana kutokana na weledi wa chuo na aina ya wasomi wanaojipambanua kuwa hapo!
Kwanza watumiaji wa vyoo hivyo ambao wengi ni wanachuo tuonyeshe kuwa kweli ni wasomi kwa matumizi sahihi na kwa usafi ya vyoo hivyo,inashangaza unaingia chooni alafu unakuta huyo anayejiita msomi maji yapo lakini kaondoka bila kuflash,hii ni aibu kwa kweli!Najua wanachuo wengi mko humu,badilikeni!

Pili uongozi wa chuo na serikali ya wanafunzi fanyeni wajibu wenu,kuna suala la usafi ambapo wafanya usafi hawasimamiwi kiupasavyo,lakini pia liko suala la miundombinu.Vyoo vingi vimeharibika na chemba nyingi sana zimeharibika,mmeongeza ada(kwa watu wa shahada za uzamili) kutoka milioni 2.3 mpaka milioni 8.5 kwa nini pamoja na mambo mengine zisitumiwe kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu?Kuna kampuni imepewa tenda ya usafi,kama wameshindwa kufanya usafi kwa nini wasiwajibishwe ikaletwa kampuni nyingine itakayoweza kufanya usafi vizuri?Mi nakaa nyumbani kwangu lakini kila ninapowaza kwenda chuo nawaza suala la vyoo,nimechoka kwenda Mlimani City kujisaidia!
 

pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,214
2,000
Hivi nyie mnaenda Chuo Kikuu Ku.NYA au kusoma? kutwa kucha mnalalamika VYOO kwani mnasomea vyooni? Sijawahi kusikia mtu analalamika Maktaba hakuna vitabu vya kutosha, up-to date journals au upungufu wa wahadhiri. Nyie mmekalia VYOO na KANTINI tena unaweza ukakuta huyu aliyeandika hapa anasoma BA KISWAHILI na Mkopo kapata 100% sasa akili yake inawaza kula tu ndo maana muda wote anafikria wapi ataenda kubwaga uhar.o wake. Acheni Ujing.a Nyie pigeni shule pamoja ubovu wa vyoo UDSM imezalisha watu maarufu duniani ikiwemo Marais kadhaa hivyo kuendelea kulalamika vyoo vyoo hakutabidilisha kitu piga shule ukiwa na haja kimbilia Porini kama wenzako maisha yanaenda Maliza shule uigie mtaani ukifika huko jenga choo chako sasa.Hapo chuoni unapita tu

Duh huyu nae ni great thinker!!.
Kama elimu tuipatayo haitusaidii kujenga jamii bora ,ni bure kabisa!!
 

sungura1980

JF-Expert Member
May 20, 2013
1,910
1,195
Umechukua hatua gani kutoa taarifa rasmi kwa uongozi wa Chuo au DARUSO? Au unategemea wapite humu JF kuisoma?

Pale COET block A ground floor kuna ofisi ya DARUSO,opposite yake tu kuna choo sijui kimeharibika toka lini maana mwenyewe nimeanza chuo mwezi wa 10,maji machafu ya chooni yanataririka nje kote kwenye floor na hili pia wanataka waambiwe?Ukishuka pale Bondeni unaelekea COET kuna chemba mbili zimepasuka hii nadhani ni wiki ya pili au ya tatu sasa na hili nalo mpaka waambiwe?Ukisimama tu pale utawala,unapokelewa na harufu ya vyoo vichafu na chemba zilizoharibika hata hili nalo mpaka waambiwe?Hivi viongozi wa Kitanzania hawawezi kufanya kazi mpaka waletewe barua rasmi za kiofisi na maandamano?Badilikeni bwana,mnakera kwa kweli!!
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,173
2,000
Nikiwa nimejiunga UDSM mwaka huu kwa ajili ya kuongeza Elimu toka nimeingia hapa mtu ukibanwa na haja inabidi ujifikirie mara mbili ama uende porini (Hasa Pori lile la Kuelekea Changanyikeni au ukimbilie Mlimani City, Jana nilibanwa na haja kubwa kila choo ninachokwenda KIMEJAA?KUZIBA nilianza kule COET, kisha nikaja Botany, Maktaba, SRs, Mathematics, Physics vyote vimeziba/kujaa hivyo huwezi kukitumia. Ninachjiuliza je Uongozi wa Chuo Kikuu ualiona hili? juma ya 15,000 mlionao na hv vyoo kujaa hamuoni ni hatari? mnataka tukajisaidie porini mpaka lini? bora Sisi Wanaume tunaweza kujistiri huko porini zaidi nawaonea huruma kina dada. Na hali zao si rahisi kusthimili seemu yenye tatizo la vyoo.

Nikuulize Swali dogo tu? Kama Chuo Kikuu hicho Watu Wanachokipamba na Kukisifu Vyoo vyake Vinatia Aibu Unadhani Wanafunzi Wake Nao Pia Haawatokuwa Wananuka Kivyoo Vyoo? Nashukuru Mwenyezi Mungu Sijapata Shahada Yangu hapo Kwani Ningezidi tu Kuaibika! Chuo Kikongwe, Vyoo Vikongwe na Akili na Wanafunzi Wao Nazo Zina Mlengo Wa Choo!
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,636
2,000
...Ukishuka pale Bondeni unaelekea COET kuna chemba mbili zimepasuka hii nadhani ni wiki ya pili au ya tatu sasa na hili nalo mpaka waambiwe?Ukisimama tu pale utawala,unapokelewa na harufu ya vyoo vichafu na chemba zilizoharibika hata hili nalo mpaka waambiwe?!
Sasa unazungumzia nini, vyoo kuziba au chemba kutiririsha maji kwenye mifereji? Chemba kutiririsha maji kwenye mifereji ni sehemu ya solution ya kuzibua vyoo, kwa hiyo tuvumilie kwa muda hiyo harufu kwani matokeo yake yatasaidia kuwa na vyoo visafi.
 

Sir oby

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
332
225
DARUSO imeshakufa nini, hizo ndo kazi zake kuhakikisha student affairs zinatimizwa, hilo suala ni nyeti sana its better likafikishwa kwa viongozi ili wapeleke juu moja coz mkandara nae amelala sana nadhani anaandaa kauli mbiu za chama cha mapinduzi uchaguzi ujao wa 2015
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom