Vyoo vya UDSM vinatia aibu (95% vimeziba)

Achilia mbali vyoo vya UDSM, Jiji zima la Dar linatia aibu kwa jinsi lilivyokithiri kwa uchafu hadi linanuka.
 
Hata hayo mabweni yanatia aibu. Kwani kupaka rangi nje ni sh ngapi? Manake nikipita nje nachoka kuwaza ndani yamefananaje?
 
Vyoo vilivyoko jengo la cpe pale engineering ni aibu kila wakati sakafu imetapakaa maji na siku za wiki end vyoo havifai kwa uchafu.

Management ya chuo kwa kweli ichukue hatua maana chuo kinaongozwa na maprofesa ambao hata kusimamia usafi wa muhimu hawawezi.
 
Hehhe,ndo hvoo..Kajiokoe udbs ,Coict -math dept na hillpark pana afadhali...
 
Walimu wa chuo kikuu Dsm wanakesha kwenye mitandao wakictriticize serikali, kumbe wao kusafisha vyoo tu hawawezi!!!

Siyo kazi yao! yaani wewe ufundishwe na kusafishiwa choo pia? kwani serikali ipo wapi? serikali haijali mali zake!
 
Ni tabu sana. Ila naomba niulize kitu kingine huwa kinanitatiza sana Tanzania....toilet paper ni shillingi ngapi? kwanini taasisi ziko radhi watu watumie magunzi na makaratasi magumu yanayosababisha vyoo kuziba na kutumia gharama nyingi zaidi kuzibua. Cry my beloved motherland.

tUNAISHI MAISHA YA MAZOEA UKUTE HATA WANAFUNZI WENYEWE NDIO TATIZO
 
Afya ya binadamu ndio mambo yote nawashauri itisheni mgomo, mbona boom linapokosekana huwa mnagoma kwa usalama wa afya yenu (maana mnaogopa mwili kuzodhoofika kutokana na ukosefu wa chakula kizuri kwa kuwa hamna pesa) hivyo hata kwa hili la ugonjwa mnatakiwa muitishe mgomo (maana afya zitazodhoofika kutokana na magonjwa yahusianayo na kinyesi)
 
Vya kwenye Halls navyo ni balaa tu,vile vyoo vya pale karibu na ATB/ATA ni vichafu balaa,UDSM Pananuka
 
blessings Hata Chemistry Department pia? Mkuu unachukua PGD au ? ungeenda hostel za masters nyuma ya Hall 6! Ila pole kwa yaliyokusibu!!
 
Ni aibu kwa kweli. tengenezeni vyoo. Kwani Ustarabu wa mtu ni choo bora.
Uzuri wapo jirani na ARDHI University ambao ni wa masuala yanayohusiana na usafi wa mazingira especially designing sanitation facilities, ni vizuri kutumia rasilimali iliyopo jirani ili kuleta mabadiliko.

Tatizo choo kwa watanzania wengi wanakichukulia kama kitu cha mwisho na ndio maana mtu atajenga nyumba nzuri lakini mashimo ya maji machafu anajenga mwishoni kabisa au wakati mwingine hela inakata alafu anachimba kachoo ka-ajabu nje, zoezi la ujenzi liende sambamba na choo pia ikiwezekana kwenye nyumba ya familia moja chooni usiweke kandambili ili watu wajenge tabia ya kuwa wasafi pia kusafisha katika kiwango cha juu kwa kuwa anajua huwa anakanyaga bila viatu (nani kasema chooni tuingie na viatu labda vyoo vya public na vyoo vitu vile vya shimo ambavyo sakafu ni udongo)
 
vyoo vya taasisi nyingi za umma ni matatizo haswaa. huwezi kuamini mpaka ukiingia humo kwa kweli. Kwa UDSM ni delicate zaidi maana ni mkusanyiko wa watu wengi kwa pamoja na wengi wao wana makazi ya Kudumu hapo hapo chuo/campus sasa ndo mtu utashangaa hiki kweli ni chuo kikuu ama ni nini?
 
Vyoo vimeziba kwa sababu ya kuputa condoms chooni..pigeni kavu nyie why mnapenda condoms..watoto wa siku hizi jamani?
 
Ndiyo maana miti na vichaka vya UDSM vinastawi sana. Kumbe mnakunya porini! Mbolea nje nje! Hongereni kwa innovation!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom